Huu ndiyo ukweli kuhusu mabomu

Huu ndiyo ukweli kuhusu mabomu

Ndugu wana JF, ni mejitahidi sana kunyamaza lakini sasa naona niongee maana najisikia kama vile moyo wangu unataka kuripuka kwa jinsi hali inavyoonekana. Kwanza kabisa napenda kutoa pole kwa wana-Arusha kwa tukio baya hili lililowapata. Pili nawapa pole CHADEMA kwa hili lililotokea katika mkutano wenu. Tatu natoa pole kwa watanzania makini ambao nia yao ni kuona Tanzania yenye amani ambayo inatoa haki kwa watu wote na wanaofaidi matunda ya uhuru wa Nchi yao.

Ndugu zangu, yapo mambo kadhaa ambayo inabidi wewe na mimi tujiulize. Hivi ni nani aliyepanga mpango wa Kurusha bomu katika mkutano waCHADEMA, na je ? Kunauhusiano wowote katika ya bomu la mkutano wa CHADEMA na lile la OLASITI? je CCM inahusika na jmabo hili au la?

Ndugu zangu, naomba nianzie kwenye hili la uhusiano wa bomu la mkutano wa CHADEMA na la OLASITI. Napenda watanzania niwafungue macho juu ya jambo hili. Kwanza mjue kuwa uchaguzi huu ulishapangiwa tarehe za kufanywa mapema hata kabla ya mlipuko wa pale Olasiti. Huku ikijulikana wazi kuwa Arusha ni ngome Kongwe ya CHADEMA na CCM inapahitaji sana , kumekuwa na mbinu za kila namna za chama Tawala CCM kuhakikisha inaimarisha hadhi yake katika jiji hili la Kitalii.

Kama ilivyo kawaida CCM inatabia ya kufanya tathimini ya mapema katika maeneo inahofia hata pale ambapo hakuna upinzani mkali maana haijiamini sana baada ya watu kuongezeka uelewa. Mahesabu yote yamekuwa yakionyesha wazi kuwa katika kata za Arusha CCM haina chake kabisa. Swali walilokuwa wanajiuliza ni namna gani CCM ishinde kata za ARUSHA?

Jibu lilipatikana: MBINU ILIYOTUMIKA MWAKA 1995 kwenye uchaguzi mkuu kwa JIJI LA DAR ES SALAAM lazima itumike kuhakikisha kuwa uchaguzi unahairishwa Arusha huku ikijiaminisha kushinda katika maeneo mengine. Hii ilipangwa kuwa baada ya matokeo ya maeneo mengine kutangazwa huku CCM ikijihakikishia Ushindi basi itawakatisha tamaa wakazi wa Arusha kwa kuona kuwa CHADEMA si kama walivyokuwa wanadhani kuwa inakubalika. Hii mbinu ilisaidia CCM kuchukua majimbo ya DAR baada ya watu kukatishwa tamaa na matokeo ya mikoa mingine. WENYE AKILI MNAELEWA.

Swali liliofuata ni je? tutafanyaje ili uchaguzi uhairishwe? Jibu lilipatikana kuwa ni kwa njia ya kuandaa mtadao utakao vaa sura ya ugaidi kwa kufanya mashambulizi ya mapema kabla ya uchaguzi ili litakapotokea ionekane kuwa ni mwendelezo wa matukio ya kigaidi katika jiji la Arusha. Mpango ulisukwa ukasukika, ndipo bomu la Olasiti lilionekana kuwa ndilo jibu huku wakijua kuwa yuko wa kubebeshwa lawama za awali yaani waislamu kutokana na matukio yaliyokwisha tangulia. Hii ndiyo maana mrusha bomu pamoja na kuwepo Polisi hakuweza kukamatwa. Ni mpango shirikishi wa CCM na POLISI.

Bomu la jumamosi lilikuwa nilakumamilisha mpango uliokusudiwa pale Arusha, ndiyo maana uchaguzi ulihairishwa kwa malengo maalum.
kwa wafuatiliaji wa mambo mtakubaliana na mimi kuwa mazingira ya bomu la Olasiti na la jumamosi kwenye mkutano wa CHADEMA yanafanana kabisa hasa kuhusu namna polisi kwa maana ya serikali inavyoshindwa kukamata mrushaji wa bomu. Hebu jiulize, kulikuwa na sababu gani Polisi kurusha mabomu ya machozi na hata kutumia risasi za moto zilizosababisha kifo badala ya kumkamata mhalifu.

WATANZANIA NAPENDA NIJIWEKE WAZI KUWA MIMI NI MWANA CCM KABISA ila naomba niwaweke wazi kuwa adui wa wawatanzania siyo chama kingine bali ni CCM yenyewe. Je ulishajiuliza swali hili? Hivi kwanini fujo utokea katika maeneo ambayo CCM inakozidiwa na siyo wapinzani wanakozidiwa? Itakuwa ajabu washabiki wa timu inayoongoza kwa mabao kurusha chupa au mawe uwanjani huku wakijua ushindi ni wao. Itakuwa ni jambo la ajabu watu wenye matumaini kuvuruga uchaguzi CCM ndiye mwanzirishi wa vurugu zote katika chaguzi.

CCM inahitaji kuadhibiwa kwa gharama zozote lakini si kwa kumwaga damu, kwanza ni kuhakikisha uchaguzi wa Arusha ukifanyika isipate kiti hata kimoja nawaomba na wana CCM mlioko Arusha msiichague CCM maana ni maadui wa maslahi ya watu na ustawi wao. Huu siyo wakati wa kufurahia vi t-shirt na vikofia na vilemba huku ndugu zetu wanakufa.

Baada ya Arusha, watanzania wote tujipange CCM iondoke madarakani ili wananchi wapate radha mpya ya utawala wenye malengo ya kuwakomboa watu na kujali maslahi ya watu.

ANAYEPINGA NA APINGE LAKINI NAWAACHIA SWALI HILI: KAMA UPINZANI ULIOPO SASA USINGE KUWEPO HALI YA TAIFA INGEKUWAJE?

Rubbish!
 
mnapojadili mambo mazito msiingize mizaha na upuuzi. amani aliyoiweka mwalimu, leo mmeibemenda, ndiyo maana mnafaidi maovu haya ya mabomu, vita na ujinga wote. mwalimu atabaki mwalimu-ni kiongozi pekee aliyeiacha nchi katika amani. laana ya kumpuuza ndo inawatafuna sasa watanzania. mmejifanya wajuvi wa kumponda ilhali hamna weledi. laana ya kupuuza maono ya wazee sasa inawatafuna.
Mwanzo wa mwisho wa CCM
ulianza 1999 aliporehemika mwanzilishi,kwa vyovyote vitu hivi
MUUNGANO,UJAMAA,CCM,CHAMA KUSHIKA HATAMU,USAWA et.al vilipaswa viondoke
na wenyewe wanaojua mizengwe waliyotumia kuvianzisha.Viongozi wa CCM
siyo wachambuzi wazuri wa Historia:IKO WAPI DOLA YA RUMI,YU WAPI
NAPOLEONI,YU WAPI RAIS WA MAISHA WA UGANDA,YU WAPI MFALME WA
AFRIKA-KHADDAFI?I WAPI DOLA YA OOTOMANN ULAYA?IKO WAPI USSR?YU WAPI
SADDAM?IKO WAPI KANU YA KENYA?hawa wajiandae kupisha historia na
wasijisikie vibaya.Sasa wasitafute kuongeza umri wa kuishi kwa kuanzisha
majanga!Yatapita,tutaona,kwa sasa tukubali maumivu kma vile mwanamwali
anavyokubali utungu ili kuitwa mzazi!Analysis imetulia!
 
kwa jinsi ulivyoandika unajipambanua wazi kuwa wewe ni mwanachadema ingawa unajiita kuwa ni mwana ccm. njaa hizi zitatumaliza kabisa

Lizaboni, basi kama unaona kuna ukweli au uongo jadili katika muktadha huo, kudai kuwa ni mwanachadema kuwa njaa zinatumaliza haisaidii. Sijui nikueleze vipi unielewe. Mimi ni mwana CCM mwenyekukereketwa na mstakabali wa taifa na watu wote bila kujali itikadi. Kama huamini subiri ipo siku nitakupa taarifa za vikao vya ndani vya CCM hasa nitavyoona kuwa vinataka kuangamiza au kubaka demokrasia na uhuru wa watu ndipo utatambua nisemayo. Mimi ni mzaliwa wa kijiji cha Makunda kilichoko Kata ya Kyengege tarafa ya Kinampanda, siwezi kuwa mnafiki na kuugeuza uovu kuwa haki. Mwigulu ni mbunge wangu huko nyumbani lakini mimefika mahali najihisi kutapika kila ninapomuona hata kusikia matamshi yake.
Hivi Lizaboni kama siyo mnafiki naomba useme ukweli kama mtu huru, mwenye mawazo huru ambaye angalau amesoma kidato hadi cha pili kama umezidi hapo nashukuru, hebu nieleze katika haya yote yanayoendelea wa kulaumiwa ni nani? Je ni kama alivyosema Nape CHADEMA wanaweza kujirushia bomu wao wenyewe kweli kama huo si ukichaaa ni nini. Kuwa mwenezi siyo kuwa kama debe tupu, ni muhimu kutafakari kabla ya kusema huku ukijiuliza wasikilizaji wangu watapata ujumbe gani.
:heh::heh::heh::heh::heh::heh::heh::heh::heh::heh::heh:
 
!!

...Ngoja nikaongee na Mbunge wangu kodi yangu ianze kukatwa JF badala ya sehemu nyingine...

...Asante sana Mkuu dot mpaka wavuni......
 
Kuna kitu cha msingi ambacho kwa mzalendo wa taifa hili unakipata bila kujali itikadi za kisiasa. Ni busara kutafakati mara mbili au zaidi juu ya maelezo haya.
 
I see, ukishangaa pumba za Lipumba, utaziona za Nape, eti anadiriki kusema kwamba CHADEMA ilihofia kushindwa Arusha hadi wakaamua kujilipua na bomu kwenye mkutano wao, Yaani CHADEMA ihofie kushindwa Arusha mjini hadi wajilipue na bomu, teh teh teh!, kuna watu sasa aibu hawana kabisa.
 
nilipoingia hapa nilikua nimepanga kuja kubeza hizi post za mabomu tumezichoka lakini nimejikuta nasoma mpaka mwisho na kupata point zote za msingi tupu yani hadi raha.
Mtoa mada na hakika tukikaa mi na wewe pamoja tutafanya makubwa sana
naomba nikutafute kwa ridhaa yako mkuu

Muda ukifika tutaonana tu, asiye kinyume nawe yuko pamoja nawe. Adui yetu ni mmoja CCM kwa matendo yake.
 

Rubbish yourself. Shame upon your face. You must understand that this is from a person who is well informed than you. I am a senior member of CCM holding some key positions in the party, I wrote something which I am sure of. CCM is a calamity.

You must repent otherwise God's judgment is coming soon.
 
Rubbish yourself. Shame upon your face. You must understand that this is from a person who is well informed than you. I am a senior member of CCM holding some key positions in the party, I wrote something which I am sure of. CCM is a calamity.

You must repent otherwise God's judgment is coming soon.

So you are holding key POSITIONS IN THE PARTY??? How many positions? hahahahahahahahaha! Duuuuuuh! And how sure you are to say you are well informed than me??? You do not know me, you do not know what I do for a living, how could you tell that you are capable of knowing things than others when you do not know them?? you better write sense and be reasonable. That said, I still insist that what you wrote is utter nonsense and wishful thinking. And from what you write, it appears to me that you are a very emotional person with no stable mentality. I am not going to be emotional and unreasonable like you to the extent of placing my self higher than others by boasting about the position I hold in this country but rest assured that I am not just like another person you know. I am someone else and I really mean it.
 
Position kwenye ccm inatuusu nn sisi! Au unataka kutuambia mkishakua viongozi huko Ccm ni viongozi serikalini sio!!

Sent from my BlackBerry 9800 using Jamie
 
Uchambuzi mzuri. Na sasa ninaweza kuanza kuelewa kauli ya Kadinali Pengo baada ya bomu la Olasiti kuwa ameambiwa na watu anaomini hawawezi kumdanganya kuwa tukio hilo halihusiani na udini. Wkt huo sikumwelewa, but time is always the best teacher. Yamkini alikuwa sahihi maana sasa inaanza kujidhihirisha kuwa hilo nalo lilikuwa tukio la kisasa!!!!
 
CCM wanadhani wako peponi kumbe wako motoni ni swala la muda tu na kila kitu kitakuwa kama ambavyo kinatakiwa kiwe. only time will tell
 
Back
Top Bottom