Huu ndiyo Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Articles of Union)

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Wapendwa JF, mtandao uletao mabadiliko nchini,

Kwa miaka mingi watanzania tumekuwa tukijadili mengi juu lakini hatukupata fursa pana ya kujadili Mkataba wa Muungano yaani Articles of Union uliosainiwa na Nyerere na Karume.

Haijapita miaka mitatu tangu baadhi ya wazanzibar walipoadhimia kuupata mkataba huu wakaambiwa hauonekani, na nadhani wakajaribu waupate kule United Nations ila sikumbuki huku waliambiwaje huko.

Tundu Lissu mwaka jana alipowasilisha Hotuba ya Kambi ya Upinzani alielezea dai la Serikali ya Tanganyika lakini akatamka wazi kuwa "hatutaki kuona picha za Nyerere na Karume wakichanganya udongo, tunataka Mkataba wa Muungano".

Kumbuka, miaka miwili nyuma, ni hapahapa JF wenzetu wengi walitafuta cha Julius Nyerere kiitwacho "Uongozi wetu na Hatima ya Tanganyika". Nilipokimwaga humu jamvini kulikuwa na chereko kibao.

Leo tena, nawaletea Mkataba wa Muungano yaani Articles of Union. Wapo wanaosema Mkataba huu ndiyo mama wa katiba zetu mbili yaani ya Muungano na ya Zanzibar. Wapo wanaosema yale mambo 11 ya Muungano yameongezwa kadhaa. Sasa mkataba huu tuuone ukweli wake.

Ni nafasi yetu leo Jamii Forumn, tuendelee kunoyesha kuwa sisi ni "never dry thintank, tunatafiti and we dare talk openly". Vilivyojificha tuna uwezo wa kuvifurumua vikawekwa hadharani.

MODERATOR

Nakumbuka thread ile ya Kitabu cha Hatima ya Tanzania iliwekwa kama "Sticky" na hivyo ikajadiliwa kwa mapana bila kupotezewa.
Ningeomba tuwasaidie hivyohivyo wana-JF wengi kwa kui-stick hii pia, kwani naamini asilimia kubwa itakuwa ndiyo mara yao ya kwanza kuuona.

Mkataba ni kama ifuatavyo:

MKATABA WA MUUNGANO BAINA YA JAMHURI YA TANGANYIKA NA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR

Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinafahamu uhusiano wa muda mrefu watu wake na mshikamano na kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Afrika, zimekutana na kutafakari Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Na kwa kuwa Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, zinapendelea ya kwamba Jamhuri hizi mbili ziungane kuwa Jamhuri moja huru moja kwa amasharti ya makubaliano yafuatayo:

Kwa hiyo IMEKUBALIWA baina ya Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar kama ifuatavyo:-

I) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri huru moja.

II) Katika kipindi cha kuanza kwa Muungano mpaka Baraza la Kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (Kuanzia hapa kitaitwa kipindi cha mpito), Jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka ya (vi).

III) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:

a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano

b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar.

c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano.

d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.

IV) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-

a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Mambo ya nchi za nje
c) Ulinzi
d) Polisi
e) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
f) Uraia
g) Uhamiaji
h) Mikopo na biashara ya nchi za nje
i) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
j) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
k) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu

V) Bunge na Serikali vilivyotajwa vitakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kuongezea mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanganyika.

Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-

a) Masharti yoyote yatakayowekwa na chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria.

b) Masharti yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.

c) Mabadiliko yoyote kama yataonekana yanafaa au kuhitajika ili kufanikisha Muungano na mkataba huu.

a) Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano atakuwa ni Mwalimu J. K. Nyerere na ataongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kufuata masharti ya mkataba hu na kwa kusaidiwa na maofisa wengine atakaowateuwa toka Tanganyika na Zanzibar na watumishi wa Serikali zao.

b) Makamo wa kwanza wa Rais kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kwa kufuata marekebisho kama yalivyoelezwa na ibara ya 3, atakuwa Sheikh Abeid Karume.

VI) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar

a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.

VII) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na abeid Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe Ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964.

Umepitishwa na Bunge siku ya tarehe Ishirini na Tano ya Aprili, 1964.

Pius Msekwa, Karani wa Bunge

Adam Sapi Mkwawa, Spika

25 Aprili 1964


SOURCE:

1: Author: Aboud Jumbe,

2: Author: Ali Shaaban Juma
 
Asante sana kwa hii nondo! JF kweli kiboko; nimo katika kundi la wale akina Thomas wasioamini-i thought kweli document hii haipatikani!
 
Asante sana kwa hii nondo! JF kweli kiboko; nimo katika kundi la wale akina Thomas wasioamini-i thought kweli document hii haipatikani!

Asante Mkuu,

Sorry utaona reply yako nime-edit. Si kubadilisha content, bali ni kwa sababu nimeitayarisha kwa kui-type kwenye document nyingine nikapata matatizo wakati naikopi kwenye browser ya JF online.

P'se bear with me that.
 
Asante sana kwa hii nondo! JF kweli kiboko; nimo katika kundi la wale akina Thomas wasioamini-i thought kweli document hii haipatikani!

Mkuu kuquote post ndefu namna hii ni usumbufu kwa wasomaji hasa ambao wako via mobile.
 
Bunge lililopitisha mkataba tar 25/4, lilikuwa la Tanganyika peke yao au lilihusisha wazanzibari? Sijaona sehemu spika wa Zenji akitajwa.
 
Ndiyo kwisha habari hapo? Duh, inabidi kutafakari kweli uhalali wa huu muungano aka "bomu la muungano"
 
Tatizo sio mkataba wenyewe, tatizo ni kwamba mkataba haukufwatwa tangu mwanzo wake. ulichokiweka hapa ni mkataba ambao ulijadiliwa na bunge la Tanganyika. mkataba ulitaka pia bunge la Zanziba liujadili na kuupitisha ndipo usainiwe kuwa sheria rasmi ya kuanzisha Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar. kwa upande wa Zanzibar hawakupata fursa hiyo kwani hata bunge halikuwepo. na pia hakuna ushahidi wowote kwamba bunge la Zanzibar liliwahi kukaa na kupitisha mkataba huo, hivyo hata kama mkataba ni mzuri kiasi gani - unakosa uhalali wa kisheria.
 
Aliyeleta hio ametoa kwenye kitabu cha aboud jumbe mwinyi 'the partnership - thirty turbulent years of the union'

kisheria hio sio document yenyewe kwa kuwa:-

1. Hau jatiwa saini na spika wala katibu wa bunge.

2. Haujatiwa saini na yeyote mwenye mamlaka anayewakilisha jamhuri ya tanganyika na jamhuri ya zanzibar

wanasheria wataongezea
 
Nashukuru kukiona kile kinachoitwa mkataba wa muungano sijapatapo kuuona kabla wala sikufikiria siku moja ningeuona.
Ahsante sana jf. Ahsante sana mleta mada!
 
Japokuwa sio ndio mkatba halisi, lakini mambo yote muhimu yapo, naamini utaamusha ufahamu wa wahafidhina mgando wa muungano huu batili!
 
Alaaaah!!Kumbe ndiyo maana kila kukicha wimbo ni ule ule wa kero za muungano!Kwakweli viongozi wetu hawajatutendea haki hata kidogo!!Nitaendelea kuwalaumu hata huko huko makaburini walipo!
 
Back
Top Bottom