Huu ndio wizi wa dhahabu ila ule mwingine sio wizi wala 'kupunjwa'

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
9,621
2,000
Tukio hili la ujambazi huko Iringa kwa mujibu wa ITV Tanzania (:: Majambazi Wavamia Mgodi Wa Dhahabu Iringa Wajeruhi Na Kupora Fedha Na Dhahabu) linasaidia kutoa maana halisi ya wizi wa dhahabu na makinikia yenye mikataba iliyosainiwa mchana kweupe kwa mujibu wa sheria na wasomi wenye dhamana waliopewa na sio tu wananchi bali wenye nchi pia.

Ila pia suala la kuita kwenye makubaliano halali ni 'kupunjwa' linaleta walakini. Unapunjwa vipi wakati una elimu ya kutosha, ujuzi na taarifa za kina? Sasa kama kwenye karne ya 21 bado tunapunjwa tu, je tuna tofauti gani na yule chifu Mangungo wa Msowero wa karne ya taa ya moto wa kuni?

Historia itakayosomwa na vizazi vijavyo vya karne za 40 na kuendelea kama nature haitabadilika, watakuwa wamepata fursa ya kuelewa kuwa 'umangungo' ni phenomenon ya Afrika na yaweza kuwa ni genetic!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom