Huu ndio utofauti wa Wanawake na Wanaume

Huu ndio utofauti wa Wanawake na Wanaume

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
828
Reaction score
2,110
Kwa utafiti wangu hizi ni moja ya utofauti uliopo kati ya Wanaume na wanawake.

1. KWENYE MSHITUKO
Mwanaume hustuka halafu huangalia nini kimemstua, mwanamke hustuka halafu huzimia. Baadae ataambiwa na mwanaume kilichostua.

2. KWENYE KUPENDA
Mwanaume huanza kutamani kisha anapenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo anaempenda.

3. KWENYE KUSAIDIA
Mwanaume hutoa msaada halafu uhuzunika, mwanamke uhuzunika baadae ndo anakumbuka kama msaada unahitajika.

4. KWENYE MAAMUZI
Mwanaume hufikiri ndipo hutenda, halafu baadae hufikiri.

5. KWENYE KUDANGANYA
Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya kumkomoa Mwanaume.

6. KWENYE UGOMVI
Wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele halafu kila mmoja hurudi kwake kesho tena.

7. KWENYE NDOA
Mwanaume hutafuta maisha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo hutafuta maisha.

8. KWENYE KUKATA TAMAA
Mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimuumize, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe.

9. KWENYE KULA
Mwanaume hushiba kwanza ndipo huanza madoido, mwanamke huanza madoido halafu baadae hujilaumu hakushiba.

10. KWENYE SIRI
Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga'ake baadae wakigombana humtolea siri zake.

#Hizi_ni_baadhi_tu_ya_tofauti
 
Kwenye wanaume umeainisha safi kabisa,wengi tupo hivyo.... Kwa wanawake umewapatia hao wa pwani
 
Back
Top Bottom