Huu ndio UNAFIKI, Hila na Ukasuku wa CHADEMA na wafuasi wake na Majibu ya Dr. Slaa

kajanks

Member
Apr 18, 2011
22
18
1. Serekali ya CCM haijafanya hata jema moja machoni mwao tangu uhuru

2. Mahakama hutenda haki endapo tu upande unaoungwa mkono na Chadema utashinda, vinginevyo husema mfumo wa mahakama Tanzania ni wakidhalimu niletegemea wangesema ni wakidhalimu hata waliposhinda kesi zao badala yake husema haki imetendeka.

3. Tume ya uchaguzi huwa huru na ya haki endapo tu mgombea wa CHADEMA atashinda, na matokeo yakiwa tofauti basi huonekana hakuna haki.

4. Mara nyingi viongozi na wafuasi wa chama hicho humtukana kiongozi wa nchi hasa Rais Kikwete kwa kumwita majina ya kejeli na dhihaka, na hii inaonesha dharau kubwa kwa mamilioni ya watanzania waliompigia kura JK kama rais wao, kumtukana raisi ni kuwatukana watanzania, siamini kama watanzania watakua tayari kukubali chama kinachowatusi kila kukicha.

5.wengi wao kujihisi kuwa ni wazalendo ilhali hata kuzilinda na kutetea jamii wanazoishi nazo hawawezi, waangalie maeneo yao ya kazi, mahali wanakoishi, wamekuwa mawakala wazuri wa rushwa, ila waandishi wazuri humu kuitukana serekali kana kwamba jukumu la kuzuia rushwa nila serekali pekee.

6. wamegeuza maandamano kama kichaka cha kuharibu amani ya maeneo ya nchi, hapa hujifanya na kuja na lugha ya naandamano ya amani, sasa jiulize maandamano gani ya amani ambayo hulazimika wafanya biashara kufunga maduka yao kwa kuhofia wizi na unyang'anyi wa vijana wavuta bangi..

7.wengi wamekua wakiponda mfumo wa elimu wa tanzania kuwa ni mbovu kwa miaka mingi sasa, cha kushangaza wengi wa vijana wao hujiita au kujiona wasomi, sasa najiuliza kama elimu ni mbovu unapataje nguvu ya kujiita msomi wakati serekali ya chama cha mapinduzi hakijakupa elimu bora? ingawa pia kwa mfuasi wa chadema kuandika sentensi za kiingereza yatosha kabisa kujihisi yeye ni Profesa.

8. siku zote wamejipa upofu wa kimakusudi kwa kushindwa kukosoa hata pale chama chao kinapofanya madudu kwa kuwa tu wanakipenda, na hapa ndio dhana ya ukweli inapojikuta inawaacha mbali hawa ndugu zetu, kwao wao chama chao ni malaika, ukitaka kulijua hili waulize wafuasi wake ni lini Chadema kiliwahi kuwakosea watanzania, bila shaka watakujibu kamwe Chadema haijawahi kuwakosea ila CCM ni sumu kali kwa watanzania.

9. wanapenda kulaumu zaidi badala ya kujenga, chama cha upinzani maana yake ni kuikosoa chama kilicho madarakani lakini pia kueleza nini kifanyike kwa makosa ambayo hufanywa na wenzao lakini hali ni tofauti kwa Chadema, hulalama bila kutoa utatuzi, mfano mzuri ni juzi tu kwenye jengo lililoanguka, watu badala ya kutoa mawazo kitu gani kifanyike kuwaokoa watu walionasa kwenye jengo hilo wenzangu wachadema wanaposti lawama kwa serekali na mfumo wa ukaguzi wa majengo, ukimuuliza wewe kama raia au kiongozi wa chama uliwahi kutilia mashaka jengo lile na kuripoti kwa vyombo vinavyohusika ili taratibu zitizamwe jibu ni hapana ila kulalama baada ya ajali ndo walichojaliwa.

10. hawaoni kama Tanzania haina njaa, haina vita, uhuru wa demokrasia, uhuru wa habari, ni kweli ccm sio chama kizuri sana hasa kwa kuzingatia kasi yake ya kusimamia maendeleo ya nchi hii tangu kupatikana kwa uhuru, lakini kwa yale machache serikali ya ccm inayofanikisha ni vyema tukatambua na kuipongeza hata kama hatupendi.

ni hayo tu kwa leo, ukweli husemwa na ninashukuru nimesema na kwa hakika moyo wako utajibu vyema yote niliyosema.


=======================
Majibu ya Dr. W. Slaa
=======================

Kajanks,
Kuna ushabi wenye tija, lakini wako hauna tija wala kwako mwenyewe wala kwa Taifa, isipokuwa tu kama uko kwenye "payroll" au ya mafisadi au ya TISS. Ninasema hivyo kwa kuwa sasa Nina uzoefu na agents hao.

1. Siamini kwa mtu anayefuayilia hoja zetu Kama haelewibtunachosema, au anafanya hivyo makusudi, au ameamua tu kupotosha, au ni "Yule mwanafunzi wa mwisho darasani ambaye hata ufanye nini hata elewa". Ebu taja kiongozi wa kitaifa wa Chadema hata mmoja aliyewahi kusema ccm haijafanya lolote toka uhuru. Tunachosema, na ninarudia kwa manufaa ya wanaJF, tunachodai ni kuwa:

toka uhuru Tanu/ccm ndio peke yao waliokuwa wakikusanya kodi,usher mbalimbali, mapato toka misitu, madini,
Samaki, na mazao mbalimbali. Kukusanya kodi hizo ni jukumu la serikali na toka uhuru serikali iliyokuwepo madarakani ni ya
Tanu/ccm. Kama Kanjas anajua nyingine atuambie. Hata maeneo anayoita ya Chadema watendaji wote wanateuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa ccm, ni mtu anayeishi tu "mwezini tu" hajui tunavyohujumiwa kila kukicha kupitia watendaji hao.

Isitoshe misaada yote wamekuwa wakipokea wao hakuna mwingine. Vivyo hivyo mikopo tunayolipa leo Watanzania wote, kiasi kuwa kila mtanzania leo anadaiwa takriban 350,000. Tunalipa madden hayo kupitia soda,bia,sukari,nguo tunazonunua, na kadhalika, waliyojenga, hospital, shule, barabbara, bsndari etc tunayajua. Ebu watupe urari wa mapato yote na matumizi, sisi tunachodai ni change yetu, si kit kingpin, na Change yetu ipo kwenye ufisadi wa EPA, Deep Green Company ltd, Kagoda, Meremeta yenye ufisadi wa zaidi ya Billioni 155.

Kanjas atuambie watanzania Kama hatustahili kudai change yetu, ambayo ingewekezwa kwenye elimu, leo tusingelihangaika na ujenzi wa shule, zahanati, na hata barabara! Kanjas uwe mkweli kwenye nafsi yako, Kama wewe unalamba mahali wane huruma basi mama yako, bib yako, shangazi yako, wajomba zako na hata wadogo zako wanaofeli mitahani kwa kukosa waalimu, vifaa, madras yenye hadhi, au mama zako na dada zako wanaojifungulia sakafuni, au wanaoambiwa wabebevkanga, pamba na nyembe kujifungulia. Haya yote ni majukumu ya Serikali kwa kuwa tunalipa kodi, tena kubwa ajabu, direct na indirect!

2. Kanjas anazungumzia maafa, na kuwa vyama vya upinzani vimefanya nini. Ni dhahiri Kanjas, hapa pia kaamua tu kupotosha. a) si jukumu la vyama vya siasa kuokoa watu.

Kanjakas na wanaJF,

Naomba radhi tena, network ilikata na kukata nikiwa para ya pili. Naomba niendelee kutokea hapo. ...Kitengo cha Maafa kila mwaka kinatengewa mabilioni ya pesa na Bunge. lakini matokeo yak nenda kaangalie cambia ya waliopatwa na maafa Kilosa. Ni aibu tup. kanjas anataka tuisifu Serikali ya CCM kwa kutafuna hela zetu. Tena hakuna kit kibaya Kama Serikali kuamua kuwa ya watu waongo mchana kweupe. Ndugu zing machos yananitoka nikikumbuka Kilosa! kanjas atuambie Vifo vilivyotokea MV Bukoba, Meli zote mbili za Zanzibar, maafa yaliyosababishwa kwa watanzania kufa mikononi maw polisi. kanjakas, usipofanya utafiti, hun a haki ya kuzungumza, na Unafiki, hill na ukasuku mkubwa ni wa kusifia tu kwakuwa wewe na wa kind lako mnashiba.

Watanzania kwa mamilioni wanalia. Mwalimu Nyerere alisema 1963, wala si Leo Maendelo si ya vitu. Jenga barabara. Za lami Kama hazisaidii kubadilisha maisha ya watu ni kazi bure. Nenda Buzwagi kuna barabara ya lami, upande wa Buzwagi ni sawa na mbingu lakini upande wa pili ni sawa na ahera, wakina mama wanahangaika kusaka maji nacau kuparua chini ya arch kujitengenezea visima, watoto wanasoma shule zinafanana na mahame. Wametengwa tu na barabara! Kanjaks, pleasevtembea nchi one ndugu zako wanavyoishi, isifikiri maisha ni unwell ni wa kwenye mtandao.

Ukiisha kutembea mgeukie Mungu wako kwa jina lolote unalomwita, awe jiwe, awe Mungu aliye Hai, au vyovyote vile, kisha one Kama utazungumza lugha unayotumia hapa. Ya kwako siyo tu unafiki,hill, na ukasuku bali uhaini kwa Taifa lako. Ujue upotoshaji unaua. Siamini wan awake wa mtwara wanaotembea km15 kuchota maji watakusamehe. Ah wewe unaweza knish vizuri, kwa kuwa tu kwa kuisema Chadema inawezekana Leo mfumo wako umejazwa, na unaweza kupata braid moto. Lakini ujue umewauza wangapi kwa ulafi wako. Nani mbaya zaidi Kati yako na Chadema!

WanaJF, nisameheni kwa kuwa mkali. Hakuna majibu mengine kwa upuuzi na uootoshwaji wa kiasi hiki. Nimeapa kuitetea na kuilinda Chadema, nimeaahidi watanzania tutapigania Yao. Wote wenye maslahi ya Taifa naomba na kuwashawishi tuungane na kukataa upotoshwaji wa aina yeyote, ufanywe na mpenzi tu wa CCM au na TISS. Nimewaambia hao wote hawana lolote. Tangu nimegundua wananunua maofisa wangu nimepata ujasiri wa ajabu.

Huo ni ufisadi, yaani wanatengewa bajet na Bunge tukiamini ni Usalama wa Taifa letu, tukiwemo sote, kumbe ni usalama wa baadhi ya watu. Kama ametumwa na CCM, hizo ni mbinu za mfa maji. Tumewapa ushauri wa bure wameshindwa kuutekeleza kuwa adui yen si Chadema Bali Ufisadi mkubwa mlioshindwa kuutoa Kati yenu, ni kero za wananchi mlizoshindwa kuziondoa na si Chadema kwani ahadi mlizitoa wenyewe Chadema haikuwatuma. Mkashinda uchaguzi kwa kuwadanganya, kuwanunua kwa chumvi, sabini na kadhalika. Sasa timizeni ahadi Chadema tuacheni, tukutane uwanjani, iwapo uwanje hautakuwa na milima na mabonde.


Nawatakia wote Pasaka njema kwenye sikukuu yao, na kwa wingine wote mapumziko mema. Taifa kwenza, uzando mbele naffs zetu zifuate na Mwenyezi Mungu kwa jina lolote unalomwita abariki nia zetu hizo njema manufaa ya Taifa letu.
 
ingawa sijasoma habari yako yote ninaomba nikujulishe haya machache yafuatayo:
1. sijui kama ulichokisema unakiamini. ueleo wako wa mambo ni mdogo kwani references zako ni kutoka hapo unapoishi!
2. kumbuka ya le machache mazuri yaliyofanywa si kwamba ni zawadi toka kwa hao waliopewa nafasi hii na watanzania, hapana ni wajibu wao. Kumbuka lengo na mategemeo ya watanzania yanafahamika. hatupo hapa kujadiri eti nimepata division 4 ya form iv au vi hivyo nimejitahidi ninaomba nijaribu tena.
3. kumbuka kuwa kama hukutimiza malengo achia ngazi. watanzania ni wengi ambao wanasubiri hizi nafasi ili waweze kujaribu kufanya wonders kwa watu wao.
4. hakuna aliyezaliwa kama mtu wa kutawala wengine. ndiyo maana performance yako ikiwa ndogo inabidi uondoke ili wengine wajaribu.

MWISHO NINAOMBA TUANGALIE UKWELI NA TUUKUBARI. KUMBUKA NCHI KAMA RWANDA ni mfano mzuri wa kuangalia perfrormance ya chama au serikali. wakati wa maneno umeisha na muda haupo tena.
 
Ahaaaa!, sawsawa, at least wewe unaweza kujenga hoja, sio kama Chris Lukosi, anaandikaga pumba kabisa.
Ntawashauri jamaa wa kukonside hata ka ukurugenzi, umejitahidi sana, subiria kidogo niongee na Liz.
 
na hapo ndipo unapodhihiri kuwa wengi ni watu wa namna gani, mmefikia hata hatua ya kudanganya vichwa vyenu, sishangai kusoma hicho ulichoandika hapo juu..
 
Mkuu na-reserve comment zangu, naamini nitakuharibia kabisa mjadala ngoja nikae kimya kwanza, kila kipengele

ulichoandika kina kasoro za mizania uwiano na katika hoja zako zote umeshindwa kutofautisha mtoto ni nani na baba ni

nani na kwanini baba alaumiwe na sio mtoto! nini majukumu ya baba na yepi majukum ya mtoto na kwa mantiki hiyo mimi

nitaendelea kusoma ikibidi nitachangia maoni yangu itakapofaa.
 
naichukia ccm na mambo yake yote, naipenda CHADEMA na mambo yake yote, haijalishi ni mazuri au mabaya! Aamin
 
ingawa sijasoma habari yako yote ninaomba nikujulishe haya machache yafuatayo:
1. sijui kama ulichokisema unakiamini. ueleo wako wa mambo ni mdogo kwani references zako ni kutoka hapo unapoishi!
2. kumbuka ya le machache mazuri yaliyofanywa si kwamba ni zawadi toka kwa hao waliopewa nafasi hii na watanzania, hapana ni wajibu wao. Kumbuka lengo na mategemeo ya watanzania yanafahamika. hatupo hapa kujadiri eti nimepata division 4 ya form iv au vi hivyo nimejitahidi ninaomba nijaribu tena.
3. kumbuka kuwa kama hukutimiza malengo achia ngazi. watanzania ni wengi ambao wanasubiri hizi nafasi ili waweze kujaribu kufanya wonders kwa watu wao.
4. hakuna aliyezaliwa kama mtu wa kutawala wengine. ndiyo maana performance yako ikiwa ndogo inabidi uondoke ili wengine wajaribu.

MWISHO NINAOMBA TUANGALIE UKWELI NA TUUKUBARI. KUMBUKA NCHI KAMA RWANDA ni mfano mzuri wa kuangalia perfrormance ya chama au serikali. wakati wa maneno umeisha na muda haupo tena.

kwa ulichojibu bado unadhirisha umazwazwa wenu, nilitegemea ungejibu hoja kwa hoja, hivi hiyo rwanda unayoisema wewe umeiona? au unasikiliza maneno ya kijiweni ndugu yangu? unahitaji sana kusoma reports mbalimbali na pia uwezo wako wa kulinganisha vitu bado mdgo sana, kamwe robo haiwezi kuwa kufanana na nusu..
 
Ujinga uleule..kwa akili yako hutambui uozo uliopo ktk sekta ya elimu?duh..utumwa na posho vitawafanya mje jutia maisha yenu.pasaka hii..mnalipwa bado?
 
naichukia ccm na mambo yake yote, naipenda CHADEMA na mambo yake yote, haijalishi ni mazuri au mabaya! Aamin

angalau wewe umejaribu kuwa mkweli kuwa pamoja na yote hayo mabaya na mazuri ni chuki tu inayokufanya uichukie ccm, bahati mbaya wenzio hawataki kuweka wazi, wacha na ccm nao watuilinde sisi wananchi dhidi ya hizo chuki zenu, kuichukia ccm iliyoko madarakani ni kuwachukia watanzania walioiweka madarakani, naliomba jeshi la polisi litulinde na hayo maandamano yenu jaman dah!
 
Ngoja waje wenyewe usikie mitusi


Kiongozi siyo matusi wewe umeyasoma aliyoyaandika na umelidhika na hoja zake hasa ulinganifu, utetezi na uhalisia

wa mambo ukizingatia majukumu ya serkali na uwajibikaji kwa wananchi wake kwa mujibu wa sheria, haki ya mtanzania

kupata huduma stahiki na haki ya kweli isiyo na mashaka wala chembe ya unajisi kama katiba inavyoelekeza?

Matusi nimatokeo ya kero na kukereka kwa mwanadamu anapopewa kisichostahili tunaita propaganda.
 
Ujinga uleule..kwa akili yako hutambui uozo uliopo ktk sekta ya elimu?duh..utumwa na posho vitawafanya mje jutia maisha yenu.pasaka hii..mnalipwa bado?

ningekuona mwenye akili angalau ungepangua hoja moja baada ya nyingine, kumbe mtu mwenyewe mwepesi hata karatasi ina uzito..embe kaandamane kule...
 
mr. au dr. kajanks nafikiri kuwa na mawazo madogo na pia horizontal yako kuwa ndogo siyo kosa ila ni upungufu wa kila binadamu. cha muhimu ni kukubaliana na mapungufu yako. sitaki nikueleze mimi na nani ila jua sina dr. wala sitakiwi kuitwa mr. ila kumbuka performance yangu katika nyanja mbali mbali zinajionyesha zenyewe. sitakiwa kwenda kupiga magoti kwa mtu fulani ili nipewe kile au la. kwa hiyo jawabu unalijua mwenyewe.
 
Chukulia ungeiongelea ccm, ungepata umaarufu gani?
Pia nakushauri umtukane na dr Slaa, utafahamika na kila mtu humu.
 
Kwa kijana yeyote anayejifanya ana mapanzi na CCM ukimfuatilia utagundua vitu viwili either
1.Anajipendekeza ili apewe cheo baadae/apate viposho ili ajikimu kimaisha.or
2.Ukifuatilia historia yake wazazi wake ni sehemu ya chama kwa hiyo na yeye anasubiri arithi uongozi kwa kuuaminisha umma kuwa yeye ni mzalendo kuliko wengine kwa sababu wazazi wake ni sehemu ya serikali au chama.
Wito wangu wote tufanye kazi tuache kujikomba na kudharilisha utu wetu
 
Kwa kijana yeyote anayejifanya ana mapanzi na CCM ukimfuatilia utagundua vitu viwili either
1.Anajipendekeza ili apewe cheo baadae/apate viposho ili ajikimu kimaisha.or
2.Ukifuatilia historia yake wazazi wake ni sehemu ya chama kwa hiyo na yeye anasubiri arithi uongozi kwa kuuaminisha umma kuwa yeye ni mzalendo kuliko wengine kwa sababu wazazi wake ni sehemu ya serikali au chama.
Wito wangu wote tufanye kazi tuache kujikomba na kudharilisha utu wetu

kamwe kijana mwenye akili hatosihi kwa ndoto za kufikirika, badala kuhimiza watu wafanye kazi wao wanaishia kuwatengenezea mazingira ya vijana kuwa kizazi cha malalamiko, timiza majukumu yako nchi iende mbele, wengi wa nyinyi mnaojifanya kuisapoti chadema hata kuondoa taka iliyokaa barabarani bado hamjaweza unafikiri unamapenzi ya dhati na nchi yako kweli? au unafikiri utanzania ni kupiga kelele dhidi ya serekali?
 
Back
Top Bottom