Ukisema huu ndio 'uchawi wake' una maanisha kuna something behind mafanikio yake kiwe kizuri au kibaya. Mfano sala,ameenda kwa mganga or chochote kile,sasa hapa kwa Jide hakuna ulichotaja hivyo hiyo heading sio sahihi.
Namkubali sana huyu mdada,she is such a strong woman na mfano bora kwa kila mtu. Tusimsahau pia Gadna G Habash mtu wake wa karibu aliyempa kampani hadi leo hii. Jide amepitia mengi ila anayeyajua sana na aliyeyavumilia sana ni anayelala naye na kuamka naye kila siku so big up Gadner G. Kila nikikumbuka nyimbo ya machozi na ile album ya kwanza nashindwa kuamini kama ndio wewe the same Lady J Dee,hivi umeshindwa hata kuwa bonge kama wakina Dully,Prof J,matonya etc baada ya kutoka? Umeshindwa hata kutumia madawa ya kulevya na kupotea kwenye game kama wakina daz baba,feruzi,ray c etc? Umeshindwa hata kujiingiza kwenye skendo za kingono,picha chafu n.k? Hongera sana na all the best katika safari yako ya mafanikio zaidi.