frontpage
Member
- Feb 26, 2017
- 71
- 113
G4S SECURE SOLUTION ni kampuni kubwa inayojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiulinzi, Ndiyo kampuni inayolinda ubalozi wa U.S.A kwa hapa Tanzania, ndiyo inayolinda mgodi wa ACACIA geita na Nyamongo, mbali na maeneo niliyoyataja kuna mengine mengi.
.
Kampuni hii imekuwa ikiendeshwa kihuni sana, mikataba yao kwa wateja wao ni ya kiubabaishaji sana ukizingatia na gharama kubwa wanazozitoza kwa wanaoingia mikataba nao.
.
Nianze na mikataba:-
G4S SECURE SOLUTION wamekuwa wakiwatoza wateja wao gharama kubwa ukiliganisha na huduma wanazozitoa ni za kibabaishaji. Unakuta mteja anailipa kampuni hiyo milioni 2 kwa askari mmoja kwa mwezi lakini wao wanamlipa laki moja na nusu mfanyakazi anayefanya kazi hiyo ukijumuisha na over time inafika laki mbili na nusu, hivi kwa malipo hayo unadhani kuna kazi ama mzaha?, mteja hana usalama wowote maana mfanyakazi anakuwa hajalipwa inavyostahili hivyo ufanisi wa kazi haupo.
.
Pili wafanyakazi wanadhulumiwa pasipo kuwa na mahala pa kuzungumzia:-
Katika hili niseme limekuwa sugu sana, wao wanalipa kwa mfumo wa masaa, lakini masaa yao hufikia wakati hayako sawa kama mfanyakazi alivyofanya kazi zake kwa mwezi mzima, wanachokifanya ni kuiba masaa 20 hadi 30 kwa kila mfanyakazi na kuyaingiza mfuko wa wajanja kwa manufaa yao walio na jukumu la masaa na kulipa pesa za mishahara..... ushahidi upo maana ni malalamiko mengi yametolewa kwao na wafanyakazi kuahidiwa kuingiziwa kiasi hicho mwezi utakaofuata na hakuna litakalofanyiwa kazi.
.
Wafanyakazi wamekuwa wakifukuzwa kiholela pasipo utaratibu wa kisheria kwa kujivunia kwamba walimnunua mwanasheria aliyekuwa akifanya kazi mahakama ya kazi aitwa NEEMA, hivyo hata kama utaenda kuishtaki kampuni hutoweza kusimama na kumshinda mwanasheria huyo maana anafahamiana na idara nzima pale mahakama ya kazi, kesi nyingi za kampuni hiyo zimeishia kuwekwa kapuni na kupigwa kalenda.
.
Unyanyasaji wa kingono:-
Kampuni hii imekuwa chanzo cha kuvuruga ndoto za mabinti wengi kwa kupewa mimba na viongozi wao kwa kigezo cha kupangiwa mahala pasipo na usumbufu wa kazi nyingi, RUSHWA YA NGONO imepelekea mabinti wengi karibu 80% ya wanaofanya kazi kampuni hiyo ya G4S SECURE SOLUTION kuzalishwa na kutelekezewa watoto.
.
Kupitia uzi huu wahusika wa haki za wafanyakazi na haki na kibinadamu walifanyie kazi jambo hili linaloendelea ndani ya kampuni hii, Ubabaishaji kama huu umepelekea kampuni hii kuvunjiwa mikataba katika maeneo mengi waliyokuwa wakifanya kazi, hii ni pamoja na:-
.
*DANGOTE CEMENT MTWARA Hapa ulifanyika wizi mkubwa wa mashine ya karibu milioni 200 na wakasitishiwa mkataba kwa kushindwa kudhibiti usalama maana ulifanyika ushirikiano wao kutekeleza jambo hilo.
.
*HOTELI ZA KITALII ZANZIBAR hapa walitakiwa wawaongezee wafanyakazi mishahara kwa kanuni za zanzibar na matakwa ya mteja lakini wao waligomea wakitaka ongezeko la pesa kutoka kwa mteja.Malipo ya mteja ni milioni moja na nusu, mfanyakazi alilipwa laki na nusu, hebu angalia tofauti iliyopo hapo.
.
*MGODI WA ACACIA hawa waliwataka G4S waongeze mshahara wafanyakazi hadi laki 8 kutoka laki 4 maana wao ACACIA hulipa milioni mbili na nusu 2,500,000 kwa askari mmoja mshika bunduki, wao G4S waligomea na kuona ni hasara kutekeleza hilo na mkataba hautoendelea baada ya mwezi huu wa April maana ACACIA waiona ni upuuzi. Huwezi kulipwa malipo makubwa na anayehusika na kazi ukambinya kiasi hicho.
.
Kiujumla kampuni hii imekuwa ikinyonya na kukandamiza maslahi ya wafanyakazi pasipo na woga wala hofu ya kuiogopa serikali ya Jamuhuri ya Tanzania.
.
Endapo watashindwa kuyafanyia kazi haya ndani ya muda mfupi swala hili litazidi kuanikwa katika taswira za kimataifa zaidi.