Huu ndio mwanya kwa CCM kuongeza "mgogoro" wa CUF ya Lipumba na ile ya Maalim Seif

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Katika uchaguzi wa Bunge la EALA CUF imewasilisha majina manne katika uteuzi wa wabunge wa Afrika Mashariki,CUF ya Maalim Seif na Mtatiro imeleta jina moja la Wakili Taslima na ile CUF ya Lipumba na Magdalena Sakaya imeleta majina matatu na mmoja kajiengua.

Katika majina hayo manne anatakiwa kupatikana Mbunge mmoja kuwakilisha Chama chake na nchi katika Bunge la Afrika Mashariki.Licha ya upande mmoja kati ya CUF ya Maalim na ile ya Lipumba kupeleka mapingamizi ya kutokumtambua mwenzake,msimamizi wa uchaguzi huo ambae ni Katibu wa Bunge la JMT ametupilia mbali pingamizi hilo.

Mshindi wa leo katika uchaguzi huu wa EALA anaenda "kukoleza" mgogoro wa CUF kati ya Maalim Seif na Prof Lipumba.Hii ndio nafasi ambayo CCM inakwenda kummaliza Maalim Seif kwa kuwapa kura wale wa upande wa Prof Lipumba ili CUF mbili za Unguja na Buguruni ziweze kuendelea kuchanganyana.

Ni wazi kuwa Uchaguzi huu si tu uchaguzi wa EALA,bali mkakati wa CCM kukoleza kutokuelewana kwa chama hicho chenye nguvu Znz ili kufanikisha azma yake.Hapa ndio mahali CUF ya Buguruni inaenda kunyanyuka tena na kupewa "uhalali" wa kuwa ndio CUF sahihi...CUF ya Lipumba inaenda kushinda kwa kishindo pale Dodoma.

Ikumbukwe kuwa kati ya wagombea wa "CUF ya Prof Lipumba",uanachama wao ulivuliwa na "CUF ya Maalim Seif" hivyo hawatambuliki katika upande mmoja,na ile CUF ya Sakaya na Lipumba ilishawavua uongozi na uanachama hawa waliomteua Taslima.

Huu ndio "mtego" wa kimkakati na kimfumo uliotegwa na CCM dhidi ya CUF ya Maalim inayowasumbua huko Zanzibar na kusababisha uchaguzi wenye mgogoro kurudiwa.
 
CCM wako kimkakati zaidi. Always wako tayari kula/kulamba kiny. esi ilimradi azma yao itimie. Makufuri kwenye kampeni zake alisikika akilaumu mataifa ya nje kuchochea uvunjifu wa amani Barani Africa. Alitolea Mfano taifa la Libya.

Bila haya ccm wanatumia plan zile zile walizodai kuwa zinatumiwa na mataifa ya nje, kudhoofisha upinzani. Leo hii wanajiweka karibu na CUF ya Prof uchwara huku wakiiponda CUF original, wako tayari hata watu wafe lkn azma yao itimie. Tunaona hata ACT wanakuwa implemented ilimradi tu kuuvuruga upinzani. Hiyo ndiyo ccm, mbinu zao ni zile zile leo kesho na keshokutwa.
 
Kweli CCM wana fitna...Hawa jamaa bado hawaamini kuwa upinzani unaweza kujiamlia mambo yake yenyewe.Kila kitu wanataka kuwaamulia wenzao.

Hakika CCM ndio wanaoturudisha nyuma ktk nchi hii,wanaamua mambo kwa interest za chama na si Taifa,unahoji kwanini hao ni chaguo la CHADEMA?Mbona JPM hakumtaka Shyrose na akaamuru jina likatwe?Kila watu wana chaguo lao ndani ya chama

Hii ya Mnyaa,sasa imeonekana nyuma ya mgogoro wa CUF yupo nani
 
Ama kweli tatizo letu kubwa ni ccm. Bila kupambana nayo na kuishinda kama Taifa basi tutaendelea kuwa masikini milele.
 
Back
Top Bottom