Huu ndio mtihani wa Taifa kwa JPM, vingine vilikuwa vitesti vya wiki

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,492
2,361
Nasubiri kuona hili rungu la kubana matumizi likishukia mbio za mwenge. Na nadhani huo ndio mtihani wa dhati kwa mheshimiwa mengine yote yalikuwa ni vitesti vya kila wiki
 
Hivi bajeti ya mwenge huwa inatoa serikali?Kama ndio mbona wafanya biashara huwa wanachangishwa kuchangia mbio za mwenge maeneo yao?
 
Hivi bajeti ya mwenge huwa inatoa serikali?Kama ndio mbona wafanya biashara huwa wanachangishwa kuchangia mbio za mwenge maeneo yao?
Kiasi hutoka serikalini na nyingine huchangiwa na wananchi
 
Hivi bajeti ya mwenge huwa inatoa serikali?Kama ndio mbona wafanya biashara huwa wanachangishwa kuchangia mbio za mwenge maeneo yao?
Kiasi hutoka serikalini na nyingine huchangiwa na wananchi
 
Sijawahi kuona faida yahuo mwenge,labda serikali itoe elimu zaidi kuhusu mwenge(National torch),Inamulika nini wakati kero kibao bado zipo kwa wananchi e.g,ujambazi,umasikini,njaa n.k
 
Nasubiri kuona hili rungu la kubana matumizi likishukia mbio za mwenge. Na nadhani huo ndio mtihani wa dhati kwa mheshimiwa mengine yote yalikuwa ni vitesti vya kila wiki

Ni bora JPM afute mbio hizo mapeeema kabisa kwani huko nyuma wafanyabiashara walikuwa wanachangishwa pesa za shughuli hiyo; sasa baada ya sekeseke yake hii ya fukuzafukuza na kamatakamata na kuziba mianya ya ukwepaji kodi; wafanyabiashara wengi uchumi umesinyaa; wana hasira kwelikweli; hawatachangia mbio za mwenge; jambo ambalo asipozifuta mbio hizo mapema atalazimika kuzigharimia kwa pesa za umma na hivyo kuonyesha "Ugeugeu" wa hali ya juu kwa upande wa JPM dhidi ya msimamo wake wa kubana matumizi yasiyo ya lazima! Yetu macho tusubiri tuone JPM atakavyojinasua kwenye mtego huo!
 
Nasubiri kuona hili rungu la kubana matumizi likishukia mbio za mwenge. Na nadhani huo ndio mtihani wa dhati kwa mheshimiwa mengine yote yalikuwa ni vitesti vya kila wiki
Mkuu,unamfahamu aliyeanzisha mbio za mwenge alikusudia kitu gani?
 
Dhumuni la mwenge ni kubwa na ni hitajio kwa kudumisha amani na kuleta maendeleo hata kama lengo hilo halifikiwi kwa sasa isiwe sababu ya kuufuta
mwenge ni alama ya umoja
mwenge ni inshara ya upendo kwa watanzania.
zitafutwe njia mbadala za kuuhudumia lakini sio kuufuta nitamdharau sana mkuu wa kaya akifuta tunu ya taifa
ni matumaini yangu kuwa hawezi kupata fikra mbovu za kuufuta mwenge wenye kuleta hamasa za mshikamano wa kitaifa na kuendeleza amani iliyopo masuala ya gharama za uendeshaji wa zoezi zima ndio yaangaliwe upya katika kukwepa ujanja janja unaoleta kero kwa wanamchi
 
mwenge ufutwe tuu kwa sasa hauna faida iyo timu ya mwenge wangefanya katika kilimo kwa kujikita mkoa mmoja mmoja kila mwaka na nyenzo za kisasa kwa kutoa elimu kwa vitendo huku wakiwa na mashamba makubwa trekta Mersey ferguson,fiat,ford au jonh deer sio hayo ya wapi sijui mara jembe linakatika ukiwa inalima...
 
Wakuu nani anajua faida za mwenge? Maana sio bongo tu kuna mwenge wa Olympic, kijiti cha malkia, mwenge wa kombe la dunia n.k
 
Dhumuni la mwenge ni kubwa na ni hitajio kwa kudumisha amani na kuleta maendeleo hata kama lengo hilo halifikiwi kwa sasa isiwe sababu ya kuufuta
mwenge ni alama ya umoja
mwenge ni inshara ya upendo kwa watanzania.
zitafutwe njia mbadala za kuuhudumia lakini sio kuufuta nitamdharau sana mkuu wa kaya akifuta tunu ya taifa
ni matumaini yangu kuwa hawezi kupata fikra mbovu za kuufuta mwenge wenye kuleta hamasa za mshikamano wa kitaifa na kuendeleza amani iliyopo masuala ya gharama za uendeshaji wa zoezi zima ndio yaangaliwe upya katika kukwepa ujanja janja unaoleta kero kwa wanamchi
Hivi mwenge unadumishaje amani??? Ni ushirikina tu huu
 
Moto hauwezi kudumisha amani ni ushirikina huo haiwezekani watwambie unamulika maadui ndani na nje ya nchi hiyo ni Ibadan ya masisiemu ogopeni sana mwenge wakiuzungusha watanzania wanakuwa mazuzu wanna wachagu kisha wanaanza kulia na maisha magumu magu hana uwezo wa kuufuta kama kidume ajaribu aone kitakacho mpata
 
mkuu kwa nijuavyo mwenge hautaachwa kukimbizwa maana ni mzim au tambiko fulan hvi, hum ndan kuna mada ya mwenge itafute kunamtu amechambua vzr sana, jinsi ulivyo anza kwa nn unakimbizwa mpka leo,

kama kunajambo ambalo rais ataliendeleza kwa ubora ni ukimbizaji wa mwenge..
 
Sio kwamba ufutwe.

Mwenge bado ni miongoni mwa national symbols na ni muhimu tukazienzi alama za taifa

Kinachogomba ni hii alama ya taifa ilivyogeuka kuwa kero kwa wananchi badala ya heshima

Kinachotakiwa ni hiki "kibatari" kikubwa kuhifadhiwa ktk jumba la makumbusho na "siyo kuufuta".

Hata sherehe za uhuru wa Tanganyika hazikufutwa bali tulibadilisha tu mtindo wa uadhimishaji wa kumbukumbu wa sherehe hizo

Badala ya wote kukusanyika pale uwanja wa uhuru, kila mmoja alibaki nyumbani kwake na wengine kusambaa ktk maeneo tofauti kufanya usafi

Naamini mwakani, tutasheheherekea sherehe za uhuru kwa mtindo mwingine.....labda kwa kushiriki ujenzi wa madarasa au vituo vya afya kwa kila mmoja kujitolea nguvu zake!

That will be great.
 
Back
Top Bottom