Ama kweli wenzetu wamezaliwa na mitaji!Hiyo sms tumetumiea vidume 30 kati ya hao kumi tumemchomolea wajinga 20 mkatuma,demu kaingiza 200000 chap
Unaombwa elfu kumi unaandika thread, nyie wavulana mnatuangusha sana kaka zenu.Demu alinivutia, nikamtokea akanitolea nje akisema ana mpenzi wake na anampenda sana. Kiufupi hawezi kumcheat na hawezi pia kunifanya mie mpango wake wa kando. Nikawa mpole, nikajikata kiaina.
Mara paaap!
Leo kanitext anaomba nimsaidie Tshs. 10,000 tu, amepungukiwa kwenye mishe zake. Mie nimemtumia kiroho safi tu na ameshukuru. Ila najiuliza, kama alinitolea nje, hataki mahusiano na mimi, kwanini ananipiga mzinga tena na mpenzi anaye?
Naomba mtazamo wenu wadau?