Huu mtihani unahitaji busara zako kuutatua

Huu mtihani unahitaji busara zako kuutatua

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,062
Reaction score
168,725
NINI UTAFANYA? mke alimuaga mumewe anaenda kumsalimia mama yake mgonjwa kijijini. Akaondoka Ijumaa na kurudi Jumatatu na matunda kibao na vyakula vingine toka kijijini akisema ni mama kanipa kwa ajili yako mume wangu na watoto.

Mume akamuuliza kwa upole mama anaendeleaje; na mke akajibu amempeleka hospitali ila anaendelea vema, mke aliongezea kwamba mama yake amemsisitiza amtembelee tena baada ya siku chache akae naye wiki, nina hofu na afya ya mama mke aliongea kwa uchungu huku machozi yanamtoka.

Mume akamjibu kwa huruma atapona mpenzi usijali. Mume akamwambia kwa hekima ingiza vitu alivyoleta jikoni. Mke ile anaingia jikoni anamkuta mama yake mzazi akiandaa chakula jikoni. Kumbe mama ake alikuja kumtembelea tangu ijumaa yeye alivyoondoka.

Mama yake akabaki ameduwaa mlangoni mwa jiko asijue apeleke vitu jikoni au arudi sebuleni kwa mume wake.

Je! atafanyeje?

Mawazo yako ya busara yanahitajika.
 
Mke boya tuuuu. Anashindwa kumuendea hewani bi mkubwa na kumpangaaa. Hana maana. Plan kama hilo lilitaka ushirikiano toka kwa bi mkubwa wa juu.

Mi kuna siku niko home kuna mtu akanipnga bwanaa wee huyu boya anabanaaa huku afu mi nina kishtobe changu mahali buzi la maana nataka nikalichune, mi nishampanga tunaenda kwenye kigodoro kidawa anamtoa mwali yule mdogo wake huku chamazi. Akikupigia we jua utalimaliza vipi mi simu nazima namwambia chaji imeisha. Mi nikmjibu Poa.

Saa 5 nikaona boya anapiga, nikawasha kwanza mziki wa Yamoto band Nimepokelea simu kwenye speaker ya redio, Haloooo shemu, sikusikii kabisaa, huku mziki mnene naweka simu kwenye speaker ya redio kabisa, hatusikilizani, nipigie kesho, naweka tena kwenye speaker, halooo, haloooo, halooooo, nikakata.

Sijajifunga hata nukta, maana angenibana lazima tunge changanyana maneno. Maana issue yote ilikuwa uongo, hamna kidaw, hamna mwali, chamazi sikujui, manake anaweza tu kukutega chamai mtaa gani hivi ukaumbuka.
 
Huyu lara huyu??? mipango kama hiyo mpaka wakongwe lara simuombei tuition kwako ila ungekuwa mpango mzuri kama angejipanga.
 
lara 1,

Ha ha ha ha kwa ushauri uu nikigundua we ni jirani yangu aisee bora niame na wife wangu maana waweza muambukiza ulivyo fundi.
 
Last edited by a moderator:
Kweli dunia ipo ukingoni,unajisifu ujinga?assarareeee!
 
Teh teh teh,yaan kwa jinsi atakavyolowa unaeza anza kucheka badala ya kukasirika.
 
this means mwanamke hafugiki hata umpe nini milele hataridhika
 
ukiwa na mke kama huyu badilishana na mashelisheli ya matombo....... yani hata akili tu ya kuzaliwa hana?????????
 
lara 1

Wanawake zetu wa kizaramo hawa ngoma haziishi mambo yenyewe ndo haya? Bora kupotezea tu, usawa huu unatafuta mtoto half caste kwa walami tu.
 
Last edited by a moderator:
Ukiona mtu mzima analia mbele za watu jua kuna jambo
 
Back
Top Bottom