Huu mtandao Ikulu kwanza masikini baadae CCM iliufukuza, iliona mbali kwa maslahi ya taifa

kanone

JF-Expert Member
Oct 10, 2013
6,188
1,576
Nakumbuka maneno ya mzee Butiku kuwa tangu 1993 CCM ilikuwa na mtandao ambao wenyewe kazi yake ilikuwa ni kuitafuta ikulu kwa kila namna tangu hata baba wa taifa akiwa hai lakini CCM ilimeguka vipandevipande katika harakati za mtandao huo kufikia malengo yake lakini walipouchoka mwaka jana wakaufukuza CCM ikapumua na uozo wote ukaanza kupungua.

Ulipokimbila umeanza harakati zilezile. Ukiwa CCM na ulivyoimega CCM vipande sasa unataka kulimega taifa vipande ili kufikia malengo yake ya kwenda ikulu.

Ushauri wangu:

Wale wote wenye mamlaka wapambane kufa na kupona kuliponya taifa vinginevyo litapasuka,.

Mfano mzuri ni namna harakati za mtandao huo huo ulivyoipasua CCM na sasa msipokiwa macho taifa linapasuka.
 
NAKUMBUKA MANENO YA MZEE BUTIKU KUWA TANGU 1993 CCM ILIKUWA NA MTANDAO AMBAO WENYEWE KAZI YAKE ILIKUWA NI KUITAFUTA IKULU KWA KILA NAMNA TANGU HATA BABA WA TAIFA AKIWA HAI LAKINI CCM ILIMEGUKA VIPANDEVIPANDE KATIKA HARAKATI ZA MTANDAO HUO KUFIKIA MALENGO YAKE LAKINI WALIPOUCHOKA MWAKA JANA WAKAUFUKUZA CCM IKAPUMUA NA UOZO WOTE UKAANZA KUPUNGUA
SASA
ULIPOKIMBILA UMEANZA HARAKATI ZILEZILE UKIWA CCM NA ULIVYOIMEGA CCM VIPANDE SASA UNATAKA KULIMEGA TAIFA VIPANDE ILI KUFIKIA MALENGO YAKE YA KWENDA IKULU
USHAURI WANGU,
WALE WOTE WENYE MAMLAKA WAPAMBANE KUFA NA KUPONA KULIPONYA TAIFA VINGINEVYO LITAPASUKA,
MFANO MZURI NI NAMNA HARAKATI ZA MTANDAO HUO HUO ULIVYOIPASUA CCM NA SASA MSIPOKIWA MACHO TAIFA LINAPASUKA,
unamaana wapambane ili waendelee kutunyonya auuu.... unamaanisha vile..
 
Kuna kipindi hata daktari anaweza kuwa mgonjwa hasijijue, mpaka pale anapoponywa na daktari mwenye Kujua ugonjwa wake.
Vivyo hivyo, kwa sasa "mamlaka" inaumwa gonjwa, tena gonjwa sugu, kati ya magonjwa sugu yote Duniani yani lile gonjwa la kurithishana.
Na daktari pekee kwa sasa ni wananchi walio katika tawala husika kuweza kuchukua hatua kuponya au kuepukana na gonjwa hilo la kurithi
 
..wameambiwa wakaripoti polisi tarehe 01 sept. Yaani huu wamewekewa mtego wa polisi. Maan iwapo watu wao wakiandamana tu basi wakijipeleka polisi itakula kwao
 
Bahati nzuri serikali iliyoko madarakani ni ya CCM, inaujua vizuri na hila zake zote. Watanzania tu imani na JPM ataudhibiti mtandao huo.
 
Hakika mtandao wa kuuza nyumba za serikali kwa pesa za madafu upo ccm,mnunuaji wa kivuko kibovu yupo ccm,wafungia vyombo vya habari wapo ccm ili kuficha uovu wao..
 
Tuliobahatika kusoma sanaa tushakuelewa, ila mtandao hauna nguvu tena hata hao waliouvunja walikua humohumo kwenye mitandao, wanajua Kila kitu, ni suala la muda tuu
 
Maneno haya KUNTU Na mwenye kuelewa anafahamu yaliyonenwa na ndiko Mtandao unajaribu kuanzisha kwa Plan B lakini aliyepewa Dhima ya kuilinda Nchi yupo makini kweli kweli na tabu nyingine Hesabu zao Mlinzi anazijua kabla yao.Hivyo katu Hawatafikia Azma yao
 
We mke wa mafisadi.

Hizo ngonjera zako tulishazichoka.

Sasa hivi watoto wetu wanasoma bure inatosha.
Kweli mahawara huwa mna midomo myeusi..watoto wanasoma bure huku wanakaa nje pasipokuwa na vyumba vya madarasa na huku wakijisaidia polini
 
Mleta mada ulisoma mchepuo gani? Bila shaka ni sanaa! Naona baada ya kutishiwa maneno ya uchocheza wanajamvi mmekuja kwa staili ya mafumbo kuepuka mkono wa shuruti. Tuendelee hivihivi kwa pamoja tutabomoa huo mtandao.
 
Back
Top Bottom