Huu mgomo unatupeleka wapi na tutafsiri nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu mgomo unatupeleka wapi na tutafsiri nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makame, Jun 28, 2012.

 1. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TASWIRA
  1.AMRI YA MAHAKAMA IMEVUNJGOMA. SASA SIJUI KAMA KUNA HESHIMA KWA VYOMBO VYETU VYA SHERIA KWENYE HILI?
  2. PINDA NA SERIKALI HAWAJATEKELEZA KWA UKAMILIFU MATAKWA YA MADAKTARI.
  3. ULIMBOKA KATANDIKWA KICHAPO AMBACHO SIJAPATA KUONA TANGU KUZALIWA.
  4. MGONGANO WA MASLAHI BAINA YA MADAKTARI NA SERIKALI UNAELEKEA KUONDOA UWEZEKANO WA MAJADILIANO.
  5. MADAKTARI WENGI SASA WANAGOMA; NA WENGINE WANAFUKUZWA KAZI.
  6.WANYONGE WANAKOSA TIBA, NA WENGINE WATAKUFA. AKINA PINDA NA WENZAO HAWAENDI BUGANDO WALA MWANANYAMALA. NDUGU ZETU AMBAO PIA NI NDUGU ZA MADAKTARI WATAATHIRIKA

  TUNATABIRI NINI?

  1. MAAFA na MAGONJWA.
  2. PENGINE SEKTA NYENGINE ZIKAJIUNGA.
  3. SERIKALI BAADA YA KUFIKIRIA MAENEO MENGINE YA KIMKAKATI, INAJIKUTA INASHUGHULISHWA NA MIGOMO

  UFUMBUZI

  BUSARA ITUMIKE. BUSARA NI BORA KULIKO VIBURI WALA JEURI. WAUNGWANA WAJADILIANE. MADAKTARI WATAFAKARI MAAFA KWA WAHANGA WA MGOMO WAO. TUDUMISHE AMANI
   
 2. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hii thread nimeinyanyua kuelezea hali

  [h=2]Watoto Zaidi ya 20 Wameuawa Hosipitali ya Amana Jana Usiku, Inatisha Jamani[/h]
  Kwa kweli yanayotendeka nchi hii yanatisha sana. Leo Dsm kuna vilio vingi kutokana na watoto wengi kufa jana hosipitali ya Amana kwa kile kinachoelezwa kunyimwa huduma ya oxygen na madaktari. Dada mmoja akibubujikwa na machozi alinieleza kuwa alijifungua jana mchana akiwa salama kabisa na mtoto akaishi kwa masaa 8. Anasema mtoto wake alikuwa amewekewa oxygen ili isaidie mapafu yake maana katika kuzaliwa alimeza maji nadhani. Anasema madaktari waliingia usiku wakachomoa oxygen kwa watoto zaidi ya 20 na wote wamefariki dunia. Naomba kama kuna watu wahusika hapa ikiwemo wanasiasa watusaidie maana kama hali ndio hii watoto wanakufa bure bila kosa. Katika kusaidia nimejaribu angalao kutafuta huduma ya postmortem hosipitali binafsi bila mafanikio angalao tungethibitisha chanzo cha kifo tugeweza kuchukua hatua zaidi.

  Inasikitisha sana jamani na kila mtu mwenye moyo wa huruma atatokwa machozi. Hii inaonekana inasababishwa na madaktari wenye frustration na Kupigwa Dr Ulimboka. Sijui nini kifanyike!

  Source: Mhusika aliyefiwa na mtoto Amana​
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hivi sasa tunaenda kuzika mtoto wa rafiki yetu amekufa kwa sababu serikali imekataa kukaa na madaktari
   
Loading...