Huu hapa ukweli wa sakata la kutoweka rais wa tahiliso na bugando

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,188
568
Adaiwa kutekwa.
Siasa yahusishwa.
Polisi:tunaendelea na upelelezi

Rais wa shilikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu(TAHILISO)Mussa Leonald Mdede ametoweka na hajulikani alipo wala hapatikani kwa namba zake zote mbili za simu kuanzia jana jioni jijini Mwanza,bwana Mdede ambaye pia ni rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Bugando kilichopo jijini Mwanza,inadaiwa alianza kutopatikana hewani kuanzia jana majira ya saa kumi alasili mpaka leo hii kipindi habari hii inakwenda hewani hakukuwa na taarifa za mahala alipo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Bugando Benjamini Thomas alisema kwa mujibu wa taarifa alizonazo ni kwamba bwana mdede alikuwapo kwenye viunga vya chuo hicho kabla ya saa kumi jioni ambapo inadaiwa alipigiwa simu na mara baada ya kuongea na simu hiyo aliaga kwamba anakwenda mjini kati kuonana na mtu aliyekuwa anaongea nae kwenye simu mtu ambaye hata hivyo hakumtaja kwa jina na kwamba tangia wakati huo hakuweza kupatikana mpaka sasa.

Bwana Mdede ambaye pia alikuwa amechukua upya form ya kugombea urais wa chuo hicho uchaguzi ambao umepangwa kufanyika tarehe 29/6/2014,na jana saa kumi na mbili jioni ndo ulikuwa mda wa mwisho kurudisha form hiyo kwa ajili ya kuwania urais wa chuo hicho,nae waziri mkuu wa chuo hicho bwana Thomas alipoulizwa na mwandishi wa habari ni hatua gani wameshachukua mpaka sasa juu ya sakata hilo alisema kwanza wameutaarifu uongozi wa chuo hicho,kisha jana hiyohiyo usiku walienda kituo kikuu cha polisi jijini Mwanza wakatoa taarifa,bwana Thomas anaendelea kusema leo walirudi kituo cha polisi kwa ajili ya kupewa mrejesho lakini waliambiwa warudi kesho asubuhi kwa ajili ya kupata majibu kamili,mwandishi wa habari alipotaka kujua kuhusiana na uchaguzi wa chuo hicho kama utaendelea ama utasogezwa mbele kutokana na sakata la kupotea kwa mgombea huyo bwana Mdede ,Thomas alisema kwa sasa yeye kama waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi hana mamlaka hayo bali amewasiliana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzichuoni hapo kuona nini kitafanyika pia anasubiri kusikia kutoka kwa uongozi wa juu wa chuo hicho.

Nae mlezi wa wanafunzi chuoni hapo alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hii kutaka kufahamu hatua zilizochukuliwa na ofisi yake mpaka sasa alisema"Kwanza we mwandishi nani kakupa namba yangu,nani kakwambia Mdede kwamba hapatikani na katoweka ?unajua maana ya kutoweka ama kupotea?kwa taarifa yako hapa chuoni watu hukaa hata siku 2 ama 3 bila kufika chuoni"hata pale mwandishi wa habari hii alipomweleza kwamba anataarifa rasmi kutoka kwa mkuu wa polisi mkoa wa Mwanza(RPC)juu ya taarifa hizo mlezi huyo hakutoa ushirikiano zaidi na kusema atafutwe kesho jioni.

Mkuu wa upelelezi wa wilaya Nyamagana Bendalbaho alipotakiwa athibitishe taarifa hii ya kutoonekana kwa bwana Mdede na kwamba jeshi la polisi limefikia wapi katika upelelezi wa tukio hilo alisema yeye si msemaji wa jeshi la polisi mkoa na kwamba mwenye mamlaka ya kuzungumzia masuala yote yanayohusiana na polisi mkoa,nae mkuu wa polisi mkoa wa Mwanza RPC Valentino Mlowa alipotakiwa atolee ufafanuzi juu ya habari hii alisema"taarifa hizo nimepewa na vijana wangu na zinafanyiwa kazi"alipotakiwa aeleze jeshi lake limefikia wapi katika upelelezi wa tukio hilo,alisema ndo kwanza yeye amepewa taarifa hizo leo na kwamba jeshi lake bado lipo katika hatua za awali za upelelezi wa tukio hilo.

Nae rafiki wa karibu wa bwana Mdede aliyeongea na mwandishi wa habari hii Joseph Michael,alisema" moja kwa moja nalihusisha tukio hili na hujuma za kisiasa,hujuma ya kwanza ni kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chuo ambao hicho ambao waliapa kamwe watahakikisha hamalizi chuo,na asahau kurudi kuwa rais katika kipindi cha pili,bwana Mdede alikuwa mwiba sana kwa uongozi wa chuo kwani alikuwa anawabana sana katika masuala mbalimbali yanayohusiana na haki za wanafunzi,hujuma ya pili ni kutoka kwa chama fulani cha siasa ambacho nao walijiapiza kufanya lolote ilimradi asirudi madarakani,ndugu mwandishi nakwambia huyu jamaa katekwa na hawa watu wa chama hicho,lengo ni kutaka kumzuia ashindwe kurudiha form kwa wakati na hivyo kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho ili watu wao wapite kirahisi"bwana Michael aliendelea kusema tangia Mdede alipodaiwa kuchukua form ya kugombea ubunge kupitia CHADEMA kwenye uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga amekuwa akiandamwa sana na watu mbalimbali na hivi karibuni kunawatu walikuwa na mpango wa kumkatia rufaa kutokana na hatua hiyo ya kutaka kugombea ubunge jimboni kalenga,
Nae mwanafunzi mmoja wa chuoni Bugando ambae aliomba hifadhi ya jina lake alisema "ndugu mwandishi nakwambia rais wetu ni mzima,sema atakuwa katekwa na kafichwa mahala,lengo likiwa ni kumzuia asirudishe form ya kuwania urais vhuoni hapa,kwani jamaa alikuwa anainfluence sana kwa wanafunzi"
Mdede ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 4 akichukua shahada ya udaktari chuoni hapo,
mara nyingi alikuwa akiandika katika ukurasa wake wa facebook kwamba kuna watu wanamhujumu juu ya urais wake,mpaka sasa kuna hali ya sintofahamu miongoni mwa viongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo na wanafunzi wote kwa ujumla.
mwandishi wa blog hii nicholauskilunga.blogspot.com,ataendelea kuleta taarifa kadili zitakavyokuwa zinapatikana.

Updates

Nimetoka polisi na Hospitalini,kote huko hakuna taarifa zake wala haifahamiki yupo wapi mpaka sasa,bt naendelea kufuatilai na nitatoa taarifa zaidi
 
Nina amini kwa chuki hii dhidi ya c.c.m na matendo yao ni hatari kubwa kwa taifa hili lililo lelewa na nyerere kwa mitindo ya kunyamazishana,wasijue kuwa huu ni wakatia mwingine kisiasa.
 
Ndio maana mimi nikiona mtu yuko Upinzani kwa namna yeyote ile namheshimu sana maana najua anakutana na majaribu makubwa sana kwenye siasa zake.
 
Hakika nimeamini kuwa chadema ni mpango wa mungu.
-na ili mpango wa mungu uweze kutimia lazima damu na maji vitoke kwa kila mwanaukombozi.
 
Huu ni uhuni unafadhiliwa na c.c.m taifa.
-tunaposema chama hiki kimeishiwa sera na hoja zenye mashiko kwa umma ni ukweli usiopingika.
 
Bwana Mdede alishajua anahujumiwa na wabaya wake kisiasa ndani na nje ya chadema.
Anapigiwa simu na kuamua kwenda bila tahadhari. Inawezekana alihadiwa milioni akaona heri aende peke yake.
Huyo rafiki yake kuna vitu anavijua. atoe maelezo ya kina kusaidia upatikanaji wa Mdede
 
Nimebaini mengi sana mkuu wakati nafatilia suala hili,bt wakati wa uchaguzi mgombea humtii kila mpiga kura na mwana mkakati
 
Na mimi sasa inabidi niseme. Mimi ni kile chama hasimu na mke wangu wa chama kingine hasimu na changu, lakini tunapendana sana. Sasa mke wangu hajarudi nyumbani mpaka sasa hivi, na kulikuwa na tetesi kuwa wazee wa chama chake hawataki mama anihudumie kwa sababu za chama changu, hii sio haki uhasama wa kisiasa kuingia mpaka kwenye ndoa za watu, kwa watoto, kazini, na hata kwenye mapenzi. Amini usiamini, kama ilivyo dini, itabidi sasa nitafute mpenzi toka chamani kwangu, nimechoka, na sitaki tena wapenzi kutoka chama hasimu. Ni ngumu kuamini lakini kwa ushabiki wetu naimani tutaamini tu.
 
mkuu msalani hawa watu wa kadima wanamatatizo sana. wanajiteka ili ku-creat attention. wapuuzi kabisa hawa.
we dogo uitwaye nicholaus l kwa taarifa ---- tu, kadima kuingia madarakani ni vigumu kuliko UDP ya cheyo au DP ya Mtikila. hat mkijiteka mara milion. mark my words.

Hii tabia ya kutekana CHADEMA naona inashamiri siku hadi siku.

Back
Top Bottom