Hussein Mwinyi WaPemba wanakwambia hawaogopi vifaru wala Tembo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hussein Mwinyi WaPemba wanakwambia hawaogopi vifaru wala Tembo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Aug 11, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Salamu kutoka Pemba zinasema kumwambia Huseini Mwinyi waziri wa kupachikwa wa ulinzi hapa Tanzania kuwa ,hawataogopa vifaru wala tembo ,na mabomu yaliofichwa kwenye madalaja mabovu na mengine kulipuka kwenye nyumba wasizoishi watu ni mipango yake akishirikisha vyombo vya ulinzi na usalama.

  Habari ambazo zinazidi kutokeza baada ya Waziri mmoja kutamka kuwa atapeleka vikosi vyote kwenda kulinda amani Pemba na upande mwingine Husein Mwinyi akidai kuwa atapeleka majeshi ikiwa ataombwa na vyombo vya serikali ya Zanzibar kufanya hivyo.

  Kosa ambalo wamelifanya wapotofu hawa ni kutokufahamiana au kutokufahamishana ni namna gani waanze na watekeleze, katika kuhangaika kwao imetokezea kuwa majeshi na vifaru vimeonekana juzi na jana vikiranda kabla hata hawajatoa kauli zao ,kauli zimefuatilia wakati utekelezaji umeshaanza kwa maana ni mambo yaliopangwa kufanywa.

  Hayo yote hayanisikitishi ila pale nionapo CCM inatumia vyombo vya dola kama mali yao na vipo kwa ajili ya kuwaweka wao madarakani. Endeleeni hivyo hivyo mufahamu tu ,wengi wa watawala walikuwa na vyombo na nguvu kuliko mlizo nazo na leo hii hawajulikani hata walipo na wengine wapo kwenye mahakama na wengine wapo jela na wengine wanasubiri hukumu na wengine wanasubiri kukamatwa.

  Msidhanie kuwa likitokea la kutokea mtaachiwa tu kama mnavyowaachia mafisadi ,mnaangaliwa kwa jicho linalotegemea kuwa na ushahidi kamili kabisa.

  jambo jingine ambalo ni lazima muweke katika akili zenu zilizojaa tamaa kuwa Pemba ni sehemu ndogo sana mnaweza kufanya unyama kwa kadiri mnayoweza na hakuna wa kukuzuieni ila jambo moja Pemba karibu asilimia kubwa au wote ni waIslamu ,Huseini Mwinyi inasemekana ni muislamu halikadhalika na hao wa Unguja nao inasemekana ni Waislamu ,ifahamike tu kuwa hapa hapatafutwi undugu au ujamaa ,la hasha wandugu ,hakuna kul;azimishana katika kuufuata Uislamu ,hilo mulielewe kwa uwazi kabisa ,ninachokihofia ikiwa Waislamu hawa walio wengi hapo Pemba wataona wamevamiwa na kutaka kunyanganywa haki yao basi Dini ya Kiislamu inawaruhusu kufa na mtu ,Huseini analielewa hilo halikadhalika na baba yake nae pia analielewa ,hivyo hayo majeshi ya vifaru na tembo pelekeni kwa wingi sana ,kama wayahudi wanavyowafahamisha kwani vitendo hivyo ni vitendo vinavyotumiwa na wayahudi dhidi ya Wapalestina na hadi leo Wapalestina wapo na msimamo wao haujatetereka.

  Kingine ambacho kwa akili yenu potofu mnaona kupeleka majeshi ya vifaru na tembo huko Pemba ni kuzima upinzani na kuua mnasahau kuwa Pemba ni cheche tu moto ukienea basi ni Tanzania nzima na cheche haizuiliki kwa vishindo inataka akili ya mtu anaeelewa maana halisi ya cheche.Vishindo vyenu vitasababisha cheche kuenea na kurukia sehemu zingine hapo ndipo mtakapojua kuwa Pemba ni sehemu ndogo sana ya mambo ambayo mnataka kuyazima.
   
 2. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Hakuna vyombo vya dola duniani vilivyowahi kuzidi nguvu ya umma. Maovu yao yote yatafikia mwisho, Hawa mashetani watashindwa kwani hii nchi ni yetu sote na si mali yao binafsi. Hata Makaburu Afrika kusini waliua, walitesa watu lakini hatimae kilichotokea tunakijua wote. Rashidi ktk kitabu cha KULI alisema "yana mwisho"
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wananchi wamelalamikia vikosi vya SMZ (KMKM na Mafunzo) kwamba ndio wanaowanyanyasa. Mie sielewi hili la Hussein Mwinyi waziri wa ulizi serikali ya Muungano linaingia vipi hapa? Je, hawa makamanda wa KMKM wanaripoti kwake?

  Nasikia harufu za kampeni ya uraisi Zanzibar ndani ya CCM, watatafuna wao kwa wao na hatimaye mgombea wao atatokea Dodoma!
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Husein anahusika kwani yeye ndie wAZIRI WA uLINZI Tanzania na vikosi vyote vipi chini ya wizara yake ,na wanaotumia vifaru ni JWTZ na ndio walioanza kuranda huko Pemba ,kama unavyojua hawachoki kusema uwongo eti ni kawaida na wapo kwenye mazoezi au wanajiandaa na zoezi la kulenga shabaha,ila ujumbe huu utamfika tu.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kadhalika Mwinyi afahamu kuwa hata Taylor alitumia jeshi kuingia madarakani, Milosevice alitumia jeshi kufanya unyama kosovo, Foday Sankoh alitumia jeshi kupata vijiwe vya almasi tu, Jean Pierre Bemba n.k wote hawa na wengine walikuwa na maguvu ya kutisha, kupiga, kutesa na kudhulumu haki za wanyonge wanyonge leo wapo wapi? Haki itashinda tu.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nazidi kuomba Mola yasitokee yale ya Jan 26 na 27. hakika wapemba hawataki mchezo katika kutetea haki zao.

  Mungu inusuru Pemba, zanzibar na Tz
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  We wacha tu ,mpaka Waislamu wapige mbiu ya mgambo labda ndio watafahamu kwamba hata Tanzania machafuko yanaweza kutokea iwapo uvumilivu utafikia kikomo ,angalia tu majambazi yakicharuka Dar peke yake inatisha sasa ,chukulia Waislamu wanaona haki yao na nchi yao na yawenzao inaporwa ,unajuwa inaweza kuonekana kama vile hakuwezi kutokea chochote ,hata mimi saa ingine naona kwa majeshi na mapolisi tulio nao hapa kwetu hakuwezi kutokea kama yaliotokea nchi zingine.

  Ila hujiuliza sababu zilizopelekea hayo ya nchi zingine hapa kwetu zipo au hazipo ? Naona zipo ,nikitazama ulinzi na nguvu za majeshi ya huko kwengine naona tofauti kubwa sana ,sasa huwa najiuliza hivi hawa viongozi mafisadi tulio nao wanategemea kitu gani ?

  Saa ingine unaweza usiamini kabisa ,na pengine kwa uzima uliokuwa nao unaona wewe si mtu wa kufa na itakuwaje ufe huzioni sababu hata moja ya wewe kufa ,unafuata kila ambalo linahatarisha maisha yako na kujiona upo safety kwa hali yeyote ile wewe hutarajii kufa kwa leo wala kesho ni mtu wa kuishi milele tu.Lakini mara unasikia yule rafiki yako uliekuwa nae jana mkicheza kwa furaha na kufanya mazoezi nae amefariki ,Je ulitarajia kati yenu nani atakufa ?
  Hivyo ndivyo inavyoikaribia hatari hapa Tanzania tunajiona tupo salama na hakuna jambo la machafuko linaloweza kutokea amani tuliyonayo ni sawa na rafiki ambae tunacheza nae na kufanya nae mazoezi.

  Hivyo tunapoenda kulala matarajio yetu hakuna atakaetoweka tutaamka na kukutana na rafiki yetu amani na utulivu kama jana au sivyo waungwana wa JF?
  Hayo ni matarajio yetu sote pamoja na hawa mafisadi wanaotutawala ,hivyo ole wetu tukija tukiamka na kusikia maredio na matelevisheni yakitangaza kuwa yule rafiki yetu amani na utulivu amefariki.
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  1. Sasa Pemba wanalalamika nini wakati umeme wa Bara sasa unatoka Bara kwenda hata Pemba?

  2. % kubwa ya wanaolalamika wala hawako Pemba..wako nje ya nchi..wanakula kuku tu na kulalamika ktk key board! Mbona hamko tayari kuendeleza Pemba..na wengine mmewekeza sana Bara??? Nani wa kulaumiwa???
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa watu wanaisabu nazi wewe unaisabu makumbi ,kiasi ya kuwa na wasiwasi na huo uzalendo halisi.
  Mbona huhoji kwanini CCM wanajiandaa kivita huko Pemba ? Aidha kuna tetesi kuwa Pemba imeshatutoka ndio ukaona vifaru vinatembea barabarani ,niliwahi kusema hapa huenda Pemba uchaguzi wa mwakani usifanyike na ndio kama ulivyosikia waandikishaji wameshafunga virago wanamtafuta Karume wampe kisa na mkasa.
  Maji yakishamwagika tena kwenye tifutifu huwa hayazoleki tena ,kwa mwendo huu wanaokwenda nao CCM ndio kabisa chombo kinaacha gati.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..halafu wanataka kulazimisha kwamba hili ni tatizo la WAISLAMU.

  ..jamani haya ni matatizo ya KISIASA yanayowahusu WAPEMBA.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ''naona wapemba wanakikimbia kivuli chao''

  naona wapemba wanam-brainstorm rais wao mtarajiwa,bila kujua wanampigia kampeni wao wenyewe
   
 12. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili swala kubwa wakuu! Hivi kweli leo katika kunahitajika vifaru katika kuhakikisha watu wanajiandikisha kupiga kura? Kujiandikisha ni haki ya raia, anayo hiari ya kufanya au kutokufanya hivyo ikiwa wapemba wamegoma kujiandikisha kwa sababu zozote zile walizonazo jeshi linakwenda na vifaa vya kijeshi kufanya nini?

  Mmoja wa viongozi kasema zoezi lilisitishwa kwa vile watu wengi sana walikuwepo kujiandikisha kuliko walivyotegemea na hii inatishia amani!!!! Watu wengi wakienda kujiandikisha amani inatoweshwa na nini? Haya mambo yanachanganya sana kuyaelewa!
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hali tete Pemba: CUF wataka JK aingilie kati [​IMG] [​IMG] [​IMG] Wednesday, 12 August 2009 06:59 Na Reuben Kagaruki

  CHAMA cha Wananchi (CUF),kimemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw.Jakaya Kiwete, kuhakikisha anasitisha mpango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wa kutaka kutumia vikosi vyote vya ulinzi na usalama kusimamia duru ya pili ya uandikishaji wapiga kura, vinginevyo uchaguzi wa 2010 hautafanyika.

  Kauli ya CUF imekuja siku moja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Bw. Hamza Hassan Juma, kunukuliwa na vyombo vya habari, akisema SMZ itatumia vikosi vyote vya ulinzi na usalama wakati wa awamu ya pili ya uandikishaji wapiga kura itakapoanza ili kuthibiti vurugu.

  Alienda mbali zaidi na kusema kuwa; "Wananchi wa Pemba wasishangae kuona vifaru kwa vile Tanzania tupo makini katika suala la ulinzi wa nchi, ndiyo maana tumeamua kupeleka askari wa majini katika maeneo ya Kaskazini ya Pemba.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Bw. Salim Biman, alisema; "Raia hawana chochote tunawakaribisha (askari) na vifaru vyao wawaswage na kama Rais Kikwete hatazuia mpango huo uchaguzi wa 2010 hautafanyika."

  Alisema Pemba ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano, hivyo uchaguzi kama hautafanyika visiwani humo basi hata wa Jamhuri hautakuwepo.

  Bw. Biman alisema vitisho ambavyo vimeanza kutolewa na SMZ haviwatishi wananchi wa Pemba bali vinazidi kuwaongezea ari zaidi.

  Alisema kauli iliyotolewa na Bw. Juma inaonesha wazi kuwa SMZ imedhamiria kuendeleza mauaji kama yale yaliyotokea mwaka 2001 wakati wa vurugu za kupinga matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi Rais Amani Abeid Karume wa mwaka 2000 watu 21 waliuawa na wengine kukimbilia Mombasa.

  "Kama wanataka kuleta vikosi vyote vya ulinzi na usalama na vifaru pia, basi hayo ni maandalizi ya mauaji mabaya zaidi ya yale ya mwaka 2001," alisema Bw. Biman.

  Alisema kama Rais mtaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, angekuwa amekamatwa na kushitakiwa kwa mauaji ya mwaka 2001, maandalizi yanayoendelea sasa yasingekuwepo kwani hata Rais Kikwete angeogopa.

  "Watu hawana fujo wanachotaka ni haki yao, na wataidai hadi mwisho," alisema na kuongeza kuwa nia yao ni kutaka kuona watu wote wenye sifa wanaandikishwa katika daftari la wapiga kura.

  Alitoa mwito kwa wananchi wa Pemba wasiogope vitisho kwani ni haki yao ya kikatiba kujiandikisha kupiga kura. Alipoulizwa hatua ya SMZ kupeleka vikosi vya majini ili kudhibiti watu wanaoingia kwa ajili ya kuvuruga uandikishaji, Bw. Biman alijibu;

  "Hakuna mtu anayeingia hiyo ni aina nyingine ya ufisadi, wanatumia fedha za walipa kodi vibaya."

  Alisema madai hayo yanatolewa ili kuhalalisha hatua ya Serikali ya kupeleka vikosi vingi vya ulinzi na usalama kisiwani Pemba kwa lengo la kukandamiza demokrasia wakati wa uchaguzi mwakani.

  Aliongeza kuwa pamoja na hatua hiyo wananchi bado wapo ngangari.Ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati suala hilo kwa kuwa alidai Tanzania ni moja ya nchi ambazo haziheshimu haki za binadamu. "Jumuiya ya Kimataifa iitazame Tanzania kwa jicho jingine vinginevyo uchaguzi hautakuwa huru na wa haki," alisema.

  Akizungumzia vifaru ambavyo tayari vimepelekwa Pemba na kuonekana vikirandaranda, Bw. Biman alisema;

  "Ni kweli vinaonekana na kimoja kimepinduka lakini yote hayo ni maandalizi ya vitisho."

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini pemba, Bw. Said Marekano, alinukuliwa na vyombo vya habari jana akithibitisha vifaru hivyo kuonekana mitaani, lakini alisema askari hao wa JWTZ wapo katika mazoezi ya kawaida ya kulenga shabaha kwa ajili ya kujiweka tayari katika utekelezaji wa majukumu yao.

  Aliwataka wananchi kuondoa wasiwasi kwa vile mazoezi hayo ni ya kawaida kwani wanajeshi kuonekana na vifaru ni sawa na mvuvi kuonekana na nyavu.


  MNAONA KEJELI YA MPEMBA HUYU? Huku ni kukaanga mbuyu na kuwaachia.................!


   
Loading...