Hussein Bashe na group lake ni mafisadi chipukizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hussein Bashe na group lake ni mafisadi chipukizi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumishi Wetu, Mar 24, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Za hasubuhi wanajamii, waasalamu Alyekumu!

  Sijaelewa hawa jamaa wa SISIEMU Vijana (UVCCM) wanaelekea wapi na wanapeleka wapi umoja wao?

  Sasa inaonyesha wazi SISIEM hawana nia ya kukemea ufisadi, kwenye gazeti la Rai Mwema la jumatano, kijana mmoja kwa jina la Mrisho mwenye machungu na nchi hii ya Tanzania alitoa malalamiko kuwa EL na RA ndio watu waliokipotezea mvuto chama cha SISIEM. Akaonyesha wazi kabisa kuhusu kashfa za Richmond, Dowans na zingine nyingi kuwa wahusika wakuu ni hao viongozi waandamizi wa chama. Lakini cha ajabu akasimama huyo Bwn Bashe na kupinga kitu kilicho wazi na kusema waliokihujumu chama ni Mzee Six na Bwn Pombe Makufuli, mmoja akikemea ufisadi na mwingine akitekeleza majukumu ya bomoa bomoa.Kwa msimamo huo kikao chote kikaunga mkono huo upuuzi, huyo Bwana Bashe akajitambulisha kuwa yeye ni mwajiliwa wa Kampuni za RA. Wajumbe wote wakamkumbatia huyo Bwn Bashe na kumpa uwenyekiti wa kamati ya kuimalisha umoja wao.

  Wakasahau maovu ya hao mafisadi na kukumbatia vibaraka wao. Sasa Ndg zangu wameibuka vijana ambao ni maajenti wa mafisadi. Hawana uchungu na dhiki za nchi hii, wanatetea wale walio watuma!

  Sasa kwa njia hiyo SISIEMU watajinyumbua kama walivyosema na kuvaa gamba jipya?

  SISIEMU hawana nia kabisa ya kupiga vita ufisadi bali hicho chama imekuwa ngome ya mafisadi wanaofilisi nchi yetu hii ya Tanzania!

  Tufanyeje kujikomboa?

  Nawasilisha
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "acheni wafu wazike wafu wenzao"
   
 3. J

  Joblube JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Raia wa Somalia katoa mawazo yake
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni vizurii UVCCM wanapojionyeshaa vema TASWIRA yao..sikutegemeaa tofautiii...
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  UVCCM ni kama genge la vichaa, ukiwakusanya pamoja utakuta variation za uchaa, mwenye kichaa cha hali ya juu (bashe) ndiye huonekana kidume. Ikiwa unabisha nenda Hospitali ya Mirembe kwenye ng'ome ukajionee mwenyewe.
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi tutatawaliwa na wasomali
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  UV-CCM walifadhiliwa na yule mtuhumiwa wa ufisadi wa Rada Bwana Tanil Somaiya wa Shivacom mamilioni wakati wa uchaguzi wao uliowaingiza kina Malisa katika uongozi wa sasa. Tani Somaiya tuliambiwa na Mzee Mengi ni kati ya mapapa watano akiwemo na mwajiri wa Bashe. Huitaji kuwa na digrii ya hesabu kujua Bashe anawakilisha maslai ya kina nani ndani ya UV-CCM. Mzee Sitta anaposema haya waziwazi wanasema anaropoka! Majuto ni mjukuu.
   
 8. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Huyo ni kichaa plus++++++++++++ Wanajimaliza wenyewe, tutaona tuu!!!!!!!!!
   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Hili ni tishio la usalama wa nchi yetu, mpaka wasomali watatawala nchi hii.Usalama wa taifa wapowapi????????? Hakuna vetting siku hizi??????????
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Kazi yetu kubwa ni kuwafichua hata wakija kwa gia gani, tuendelee kuwafurusha tuu!!!!!!!!! Huyu Bwn nilimuona wa maana kipindi anagombea ubunge wa Nzega kumbe ni fisadi trainee wa RA, NA NI MAJIRANI. Kumbe Mzee Makamba kabla hajawekwa mfukoni alilijua hilo akamyima ubunge. Sasa amekuja na gia ya UVWCCM, kwa ufadhili wa RA, hapo lazima watu wastuke huyu ni fisadi asiye na haya analinda maslahi ya boss wake. SISIEM mfukuze Rostam Azizi kwenye uongozi wa chama, anaozesha chama kinanuka!!!!!!!!!!
   
 11. Z

  Zyansiku Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona watu mna hangaika sana! Uvccm wamefanya kikao chao kwa maslahi yao sasa wewe kama unaona hawaja kukuna hayakuhusu fuata yako mbona huu ugonjwa wa kumiliki akili za watu unataka kutawala hivi? Bashe ni mfanya kazi wa new habari kama alivyo mtanzania yeyote yule! na elimu ina mruhusu kuwa hapo alipo (CEO) kuhusu suala la Uraia tayari serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani alisha toa tamko, lakini cha kushangaza sana ni kuwa mbona mpo wengi humu mnafanya kwenye makampuni kama afanyayo bashe? IPP, hali halisi nk
  kuweni makini na hasira zenu Uvccm wamejipanga na wameona ni muda muafaka wa kutete3a wanacho kiamini kuanza kufanya sasa
   
 12. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni muendelezo ule ule wa siasa za maji taka ambazo mh six aliwahi kuziongelea mjengeni, kamati ya vijana ya kurudisha uhai wa Uvccm imeundwa na wajumbe karibu nane hivi akiwemo Hussein Bashe na nadhani hiyo ni kwa mustakabali wa Uvccm sasa cha ajabu mbona kila anaye changaia humu ndani hoja yake ni bashe! bashe! bashe! mbona wapo wengi tu after all hayo ni mambo ya Uvccm sasa kama wewe ni bavicha au nani sijui unahusikaje, kwani watu hawajui hoja za bavicha juu ya kuchakachua matokeo ya kafulila? by then mbona watu hawaongelei, huu ni muda wa kufanya kazi na Uvccm wameamua kufanya kazi hawataki leeltena ndio maana hata jana vijana wa Tabora wamefanya kazi nzuri ya kuunga mkono maazimio ya Dodoma bila shaka waka ajizi, Bashe keep it up!
   
 13. H

  HADJ DROGBA Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we sio m bongo wala nini you are somalian brother,huo ndio ukweli,tunakujua toka unasoma UNUNIO ISLAMIC SECONDARY ukisoma tuition shule ya uhuru pale kwa mwalimu ADAM.
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Weka data zote tumjue huyo
   
 15. v

  victor11 Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Watakao ijenga hii nji ni sisi wenyewe watanzania, na watakao imaliza ni sisi.
  Katika harakati zetu zote ni muhimu tukahakikisha tunaweka maslahi ya nchi na watu wake mwanzo.
  Isiwe ni kusema haya ni mambo ya chama au kikundi fulani tu wengine yawahusu nini, nadhani hivyo sivyo.
  Chochote kinachofanywa na yeyote kinachohusu maisha na maendeleo ya watu kinatuhusu sote na ni lazima sote tuingilie kati. Tukikaa kimya tukaacha yanaendelea kutokea ni sawa na kuisaliti nchi na watu wake.
   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Hatuwezi kunyamazishwa kwa mustakabali wa nchi yetu. Wanacho zungumza UVCCM kinahusu maendeleo na AMANI YA NCHI YETU. Hatuwezi kunyamaza hata kama wanaweka watu ili watumike kutunyamazisha ili waendelee kuiba na kudhulumu. Kwani nani asiyejua kuwa Rostam Aziz alidhulumu fedha zetu kwa mabilion za EPA Kupitia kampuni ya za KAGODA na zingine. Kwani sasa tumesahau kirahisi hivyo???????????Anaplant watu wake ili wanyamazishe watu wanaosema ukweli, nina uhakika Mungu wetu hawezi kunyamazishwa. Watu wapige kelele pamoja na maombi, Mungu wetu atachukua hatua. Wanao dharau watapata majibu karibuni!!! TUTAPIGA KELELE TUNAPOONA MWIZI KWENYE BOMA LETU!!!!!!!

   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Bashe ni kibaraka wa Mwizi wa fedha zetu, KAGODA, RICHIMOND, DOWANS etc kwani hatuna akili, au ni wajinga tuu!!!!!Ametumwa kunyamazisha watu kina Mrisho, na vijana wazalendo wa nchi yetu wanaosema ukweli!!!!!!!!
   
 18. m

  mwanza JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 508
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Kwanza huyu Bashe si mtanzania kwa nini atusumbue watanzania tuamke
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wewe unaangalia nakuona kwelikwe, endelea kuwachunguza. Hawafai kabisa, siamini masikio yangu.:panda:, Hata bashe nae, basi tena jamani, tufwile.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...