Anajidanganya na kuwadanganya wajinga. Maana ya Sera ama bajeti siyo process ya mtu mmoja bali mchakato mrefu na mgumu kuamuliwa. Kama Sera siyo nzuri hasa iliyoanzishwa kupitia Cabinet, huwa ni ngumu kupita kwenye tanuru la Inter-Ministerial Technical Committee (IMTC) kutokana na Wataalamu kuhusisha vigezo vingi.
Mbunge angepinga kitu kimoja hapo utasema ni sawa IMTC hawakuliona kwa mapana yake. Lakini Mbunge akikosoa kila kitu lazima ujiulize, huyu anataka Serikali ibadilishe kila kitu ama lengo lake ni kuiangusha Serikali?
Ukisema kazi ya Mbunge siyo kuitetea Serikali, sasa atatetea muda gani Chama chake? Je, anadhani Serikali ikionekana haifanyi vizuri, watakaoumia ni viongozi pekee ama na Chama pia? Bashe asijidai anajua sana siasa ukilinganisha Serikali, ni bora ajiondoe agombee upinzani ili akaikosoe kwa uhuru Serikali. Aone aibu kwani kwenye demokrasia ya Kibunga tunayofuata, kitu cha muhimu ni msimamo wa Chama na siyo uwezo wa mtu mmoja mmoja.
Ukimtoa Zitto Kabwe (ambaye hata hivyo ni mpinzani), Hussein Bashe na Nape Nnauye ndio wanaoongoza kuutangaza upinzani bungeni kuliko Wapinzani wenyewe.
Wana-CCM ni bora wamtake Bashe ajiuzulu ubunge maana alikuwa akijigamba (kama alivyofanya Edward Lowassa kuwa) kuwa, hawezi kuhama CCM. Anakumbusha jinsi Lowassa alivyowaambia wana-CCM kuwa, wanaotaka ahame CCM wahame wao.