MTAZAMO
Platinum Member
- Feb 8, 2011
- 20,212
- 35,865
Wanabodi,
Leo nikiwa katika harakati zangu za kutafuta ugali nikapita maeneo ya Osterbay shule ya msingi kujipatia chakula cha mchana.Nikiwa pale nikamuona mtoto mdogo wa kiume akiwa amevaa uniform za shule mwenye umri kati ya miaka 10 hadi 12 akipata chakula pia.Mtoto yule alikuwa akila kwa shida sana huku afya yake ikiwa dhaifu na kuonesha kila dalili ni mgonjwa.
Ile hali ya yule mtoto ikanigusa nikaamua kumuita mhudumu kumuuliza kama anamfahamu yule mtoto na nini kinamsumbua.Ndipo nilipoelezwa kuwa mtoto yule wazazi wake walifariki kwa maradhi ya Ukimwi na yeye amezaliwa akiwa tayari ameambukizwa.Nilikaelezwa pia hana ndugu zaidi ya binamu yake anayeishi naye ambaye pia ameshindwa kumudu kumsaidia.Mtoto huyu anasaidiwa na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Osterbay.
Kilichonisikitisha zaidi ni kuwa huyu mtoto hata lishe ni ngumu pamoja na kuwa kwenye dozi ya maradhi haya na pale kwenye huo mgahawa ndio huwa sometimes wanamsaidia chakula na anapokula mchana pale ndio mpaka kesho yake avizie tena msaada wa chakula pale.Wateja mbalimbali wanaofika pale na kumuona wenye moyo wa imani humsaidia fedha kidogo kujikimu.
Nilichogundua tatizo kuu la huyu mtoto ni lishe duni pamoja na kukosa huduma za afya za kueleweka.Afya yake ni mbaya mno kama una roho nyepesi machozi yanaweza kukutoka.Walimu wanajitahidi lakini hawawezi kujikuna wasipofikia.
Naamini huyu mtoto anaweza kuishi marefu sana lakini kwa afya ile niliyoshuhudia hadi kushindwa kula kabisa huku akilalamika kuumwa huyu mtoto tutampoteza.Nimeamua kuleta uzi huu hapa kwasababu najua wapo watakaoguswa na walau kuchukua hatua zilizo ndani ya uwezo wao ili walau kwanza apate huduma ya afya kurejesha afya yake.
Majuzi nasikia aliumwa akalazwa ikabidi aombe nesi ampigie mwalimu wake amsaidie (imagine walimu ndio msaada wake wa pekee).
Kwa heshima na taadhima Watanzania wenzangu naomba atakayeguswa aende shule ya msingi Osterbay amuulize huyu mtoto aitwaye Joseph akisoma darasa la tano au kwenye mgahawa ulio hapo shule ya msingi Osterbay.
Kama kuna mashirika yanayohusika na msaada kwa watoto wa aina hii tunaweza kusaidia walau wampatie huduma mtoto huyu.Binafsi nimeona nichukue walau hatua hii kuliko kuishia kumpa elfu kumi ya kula.
Asanteni sana.
Updates..
Wakuu kwa walio Dar es salaam ukifika shule ya msingi Osterbay au mgahawa jirani na hapo utapata taarifa za huyu mtoto Joseph na bahati mbaya nimeambiwa jana hakufika shule sababu ya kuumwa.sijaweka namba kwaajili ya msaada wa kifedha kutokana na utafiti niliofanya na kugundua zinaweza kutumika vibaya.Msaada mkubwa ni kupata kituo atachopata huduma za msingi ikiwemo saikolojia,matibabu na lishe.
Kwa wenye nia njema hasa wa mikoani mnaweza kuwasiliana na mods (mkuu Invisible au mods yeyote) then ukafanyika utaratibu wa kufikisha huo msaada kwa huyu mtoto moja kwa moja.
Updates.....
Mtoto Joseph amefariki jumamosi na kuzikwa jana kwa taarifa nilizozipata muda si mrefu....nimeambiwa alilazwa Muhimbili last week ingawa kiafya alikuwa ameanza kugain na kuchangamka kidogo.........
Taarifa ya mtoto huyu iwe chachu ya jamii yetu kuwajibika kuwalinda watoto hasa walio katika mazingira magumu.....badala ya kuulizana nani kafanya nini basi tuangalie namna ya kuwasaidia waliohai sasa ......
Mungu ampumzishe Mtoto Joseph kwa amani ..............
CC Mhariri , Eiyer , amu , RGforever , Mkuu wa chuo , Sangarara , Invisible , Riwa Pasco na wadau wengine wote ...