Hupendi? Mbona nawewe unafanya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hupendi? Mbona nawewe unafanya?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mapanga3, Jun 7, 2012.

 1. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 666
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 180
  Ndoa nying zinaishi maisha ya kutoaminiana kwasababu ya mienendo ya wenzio wao, na hii si kwa mwanaume wala mwanamke! Swali langu kwenu wanandoa msio waaminifu ikiwa una wanaume wa nje au wanawake wa nje, ikawa umetoka kwa mwanamke au mwanaume wa nje ukakutana na mumeo au mkeo anamwanamke au mwanaume wa nje utafanyaje? Utajisikiaje? Ni nini cha ziada unachopata kwa huyo wa nje ambacho mkeo au mumeo hana?
   
 2. M

  MKUU WA KAYA JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wewe ni mwanandoa au sio mwanandoa inawezekana hujui yaliyomo ndani.kuna mambo huko mzee ,waliomo wanatamani kutoka ingawa walio nje wanatamani kuingia!!!
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbona unauliza mambo mengi kwa pamoja?
  Pengine tofauti za maumbile (Nenda kule jukwaa la wakubwa utajioneea), pengine mambo tofauti tunayoyasikia hapa jamvini, pengine mwenzio anakunyima jambo fulani unalolitaka na huko kwengine unapewa.
  Ama hili la kufumaniana ni kuwa unapoamuwa kulifanya siri jambo basi unamjali na kumuogopa mwenzio na ukimfuma yeye unajuwa kuwa si jambo zuri na kama angekufuma wewe basi naye pia asingependa.
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hii topic yako nakumbuka tuliwahi kuijadili hapa jamvini, ni ngumu maana sababu wanazotoa wanandoa ni nyingi sana. Wapo wanaonyimwa unyumba na wenzi wao, wapo wanaonyanyaswa na kutukanwa na kukosa hamasa ya mapenzi na wenzi, wapo ambao wenzi wao wamekumbwa na maradhi ya kuwafanya wahindwe kutoa huduma nk nk.

  Lakini mbali na hayo, hoja yako ni ya msingi kuwa si jambo jema na si jambo la kufurahisha jamii mwanandoa anapotoka nje ya ndoa. Ni vyema kuwa wavumilivu na kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na migogoro ya ndoa inayowafanya watu kufikiria nyumba ndogo. Pia ni busara wanandoa kutimiza majukumu yao ya kindoa ili kuepukana na adhama hii.

  Kwenye swali lako la mwisho "mtu anajisikiaje anapofanya hayo mambo na kukutana na mwenzi wake", kwa mawazo yangu nafikiri atajisikia vibaya na huenda asiweze hata kumuangalia mwenzie usoni au pengine anaweza kuzuga kwa kumletea zawadi kuua so na kupunguza maumivu ya moyo kutokana na tendo hilo! Mweee!
   
 5. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ukikuta mwenzio naye anaye nje basi ni ngoma droo hapo! Kutoka nje kunasababishwa na mambo mengi sanaaa! Tamaa, kupata faraja nje, kutotoshelezwa kingono ndani ya ndoa au ktk mahusiano na mengine mengi mno.
   
Loading...