HUNDI za akina-MKULLO zachanwa...

HUNDI za akina-MKULLO zachanwa...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Sasa wataambulia mishahara ya Mei tu.Zile hundi zilizokuwa zikiandikwa kwa ajili ya kuwashukuru Mawaziri waliotemwa kwa utumishi wao uliotukuka zimechanwa.Hawatazipata tena 'gratuity' zao.Serikali imeshtuka.Imekimbia fedheha. Hatahivyo,nimearifiwa na chanzo changu cha kuaminika kuwa Mawaziri hao watalipwa mafao ya kustaafu nyadhifa zao wizarani.Mambo yaleyale tena. Hapo je ni halali?
 
Wanaruka majivu wanakanyaga moto. Serikali ilitakiwa kutowalipa chochote na kuwafungulia mashtaka ya wizi wa mali ya umma.
 
Sasa wataambulia mishahara ya Mei tu.Zile hundi zilizokuwa zikiandikwa kwa ajili ya kuwashukuru Mawaziri waliotemwa kwa utumishi wao uliotukuka zimechanwa.Hawatazipata tena 'gratuity' zao.Serikali imeshtuka.Imekimbia fedheha. Hatahivyo,nimearifiwa na chanzo changu cha kuaminika kuwa Mawaziri hao watalipwa mafao ya kustaafu nyadhifa zao wizarani.Mambo yaleyale tena. Hapo je ni halali?
Labda mimi ndio sielewi au upeo wangu ni mdogo kwenye swala hili, ningeomba mwenye uelewa anijurishe ni nini maana ya neno mstaafu?

Inawezekana ndugu zetu wengi ni wastaafu ila sisi tunadhani walifukuzwa kazi, sasa tuambizane hili tuweze kufuatilia mafao ya ustaafu ya ndugu zetu ambao tulikuwa tunaamini wamefukuzwa kazi kumbe sheria inawatambuwa kuwa ni wastaafu.
 
Point taken!
 
Kodi zetu zinaliwa kipumbavu yani mtu kafukuzwa kazi kwa ujambazi halafu bado analipwa mafao for what purpose mtu kajiuzuru kwa kashfa nae analipwa mafao kwamba alichotenda ni kizuri na wanathamini mchango wake wa kuiba mali ya umma.NONSENSE
 
Kama ni hvyo basi warudishe hayo matrilion waliyoiba la sivyo hawastahili kulipwa hata shilingi moja.
 
Jamani mlio karibu kwa upatikanaji wa hizi taarifa muhimu mtujuze wakilipwa tu hayo wayoyaita mafao ya kustaafu tuandae maandamano makubwa ya kulaani hicho kitendo nchi nzima.
 
Labda mimi ndio sielewi au upeo wangu ni mdogo kwenye swala hili, ningeomba mwenye uelewa anijurishe ni nini maana ya neno mstaafu?

Inawezekana ndugu zetu wengi ni wastaafu ila sisi tunadhani walifukuzwa kazi, sasa tuambizane hili tuweze kufuatilia mafao ya ustaafu ya ndugu zetu ambao tulikuwa tunaamini wamefukuzwa kazi kumbe sheria inawatambuwa kuwa ni wastaafu.

Aliyepaswa kutangaza "kuwafukuza kazi" hakufanya hivyo na badala yake akawaacha kwenye "Baraza la Mawaziri", tatizo ni lile lile "koleo haliitwi koleo."
 
Wakati China wanawapiga risasi, TZ tunawazawadia. tutakufa masikini tu.
 
Yaani nilishakuwaga demotivated kulipa KODI kitambo kwa mambo ya kishenzi kama haya
Mtu ametuliza alafu leo unamwongezea mahela badala ya kurudisha aliyochota
 
ndio tanzania hii isiyo na aibu ukiiba mamillion unashukuriwa na ukifanya kosa ndogo unafungwa lakini wakubwa hawafatiliwi
 
  1. Wamestaafu au wamefukuzwa?
  2. Kuna mafao gani zaidi ya pension zao ambazo watalipwa baada ya kumaliza muda wao bungeni!
 
kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo,ni madudu juu ya madudu.just an additional question to this issue,hivi na lowassa naye analipwa mahela kama waziri mkuu mstaafu au?mwenye taarifa tafadhali tujuze
 
Hivi hamjui tofauti ya mlalahoi na mlalaheri?
 
Nadhani ukifuatilia zaidi utaelewa mengi zaidi ya haya.. keep it up!! hawa jamaa wanaweza lipwa mafao na gratuity hata kwa njia za panya..nchi hii inawashenzi ni balaaa
 
Back
Top Bottom