Humu tunajifunza mini?

Humu tunajifunza mini?

eity 4

Senior Member
Joined
Dec 7, 2014
Posts
147
Reaction score
211
Jukwaa hili lililenga zaidi kuiimarisha jamii kwenye masuala ya ndoa, uchumba au mahusiano. Rakini ukisoma asilimia zaidi ya 90 ya thread humu zianachochea, zinashawishi na kusifia uzinzi, uasherati, usaliti katika mahusiano na kadharika kinyume na lengo la kuanzishwa kwake.
Sidhani kama kuna mtu kati yetu humu ambaye anaweza kumkubalia mke, mume, mchumba au mpenzi wake ajiunge na jukwaa hili kirahisi kutokana na mambo yalivyo humu. Humu hakumjengi mtu kuwa mke, au mume bora.
Tumeliharibu jukwaa limekuwa kitu kingine kabisaa, mambo mengi humu ni ya kijinga kuliko ya kujenga.
Naomba kuwasilisha
 
HUKU WATU WANAJIVUNIA TU KUWA WAZINZI NA KUWAPATA WANAUME/WANAWAKE KIULAINI,sasa hivi hamna cha kujifunza kilichobaki huku ni KUJISIFIA TU.
 
  • Thanks
Reactions: sab
Binafsi najifunza mengi tu humu mkuu, kuna mazuri na mabaya chukua mazuri mabaya yaache binadamu wote sio sawa usitegemee uwazacho wewe wengine wanawaza hichohicho wengine wanawaza ujinga.
 
Mkuu wakulaumiwa ni nyinyi wenye busara mkikaa kimya ndio mnawapa nafasi wenye mawazo potofu kutawala.

Anzisheni nyuzi zenye kufundisha ,kuonya na kuelimisha. Na sio kulaumu kuwa jukwaa limeharibika.


We miss the old jf....
 
Hakuna mambo ya kijinga kama mtu anapoandika Rakini badala ya Lakini.
Weeee mbona mchokozi rakini rafiki.... Huyu jamaa ni riporisi atakuweka sero mpaka 26 / 4 / 2020
 
Huku ndo kunapatkana elimu uliyoikosa shulen, ukiona hapakufai si unajikataa jaman
 
Wewe mwenyeji humu hebu fikiria anapoingia humu mgeni anaweza kudhani haya ndiyo maisha halisi tunatakiwa kuishi
 
Mkuu wakulaumiwa ni nyinyi wenye busara mkikaa kimya ndio mnawapa nafasi wenye mawazo potofu kutawala.

Anzisheni nyuzi zenye kufundisha ,kuonya na kuelimisha. Na sio kulaumu kuwa jukwaa limeharibika.


We miss the old jf....
Tunafanya hivyo, but nyuzi za kuharibu mnazichangia kuliko za maana
 
Binafsi najifunza mengi tu humu mkuu, kuna mazuri na mabaya chukua mazuri mabaya yaache binadamu wote sio sawa usitegemee uwazacho wewe wengine wanawaza hichohicho wengine wanawaza ujinga.
Lakini jukwaa hili lililetwa kujenga mahusiano, urafiki, na mapenzi katika mwelekeo unaojenga jamii, sasa hivi humu thread nyingi zianaharibu zaidi kuliko kujenga. Humu sasa hivi watu tuafundishana punyeto
ilivyo tamu, mtu alivyomcheat mke au mume kwa kutembea na x wake au house girl, nk mambo ambayo hayahusiani na jukwaa.
Naheshimu Uhuru wa watu kutoa maoni yao but ni lazima tuyakatae mawazo yanayoharibu.
 
Hii ni elimu ya mtaani.
Ya kuambiwa changanya na yakuzaliwa nayo.
 
Mi sijawahi kuona nyuzi zako za maana.
Inaezekana, maana hata Mimi niliambukizwa nikaambua ugonjwa wa Ku enjoy mambo ya kijinga sasa nimepata akili, so Yale ya kijinga nilipost nisamehe, nimeamua kurudi kwenye mstari
 
Back
Top Bottom