Humphrey Polepole unaamaanisha nini kusema hivi?

Tunahangaika sana na mambo anayoyasema na mengi ni ya kufikirika/kudhania maana hana ushahidi wowote na naona kama tunapoteza muda bure.
 
Ni awamu ya sita kwa sababu kipindi cha pili awamu ya tano hakikufikia nusu ya muda wake kwa hiyo hakina sifa ya kuitwa awamu kwa maana hiyo Rais aliyepo kaanza awamu ingine ya sita
Amechaguliwa na nani kuongoza hiyo awamu unayoita ya sita?.
 
Atibiwe kwanza kisaikologia ili ajieleze vizuri, Mimi naona giza
 
Acha umbea wewe Nani anamrudisha kwenye mstari!!? Yeye mwenyewe Alishasema kuwa Yeye na maghufuli nikitu kimoja na kwakuwa Yeye alikuwa nimakamo haipaswi ajitenge na awamu 5 jambo muhimu hapa Yeye apambane kwa akili ili ayamalize makundi yariyo ndani ya serikali yake
 
Ukweli mchungu, kaondoka Magufuli, makamu wake kachukua nafasi yake chama kilekile, sera zilezile. Polepole kasema ukweli
 
Ukweli mchungu, kaondoka Magufuli, makamu wake kachukua nafasi yake chama kilekile, sera zilezile. Polepole kasema ukweli
Ulikuwa una umri gani wakati Mzee Mwinyi anatolewa Zanzibar kuja kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania?
 
Kushughulika na Katiba ni Jambo la Lazima kwa Sasa!
 
Nilisoma Katiba sehemu inasema... Makamu wa Rais ataapishwa kumalizia muhula ulio Baki sidhani kama walisema kuanza Awamu Nyingine
 
Reactions: Cyb
Codes zatosha mkuu.
 
Nilisoma Katiba sehemu inasema... Makamu wa Rais ataapishwa kumalizia muhula ulio Baki sidhani kama walisema kuanza Awamu Nyingine
Mimi nadhani hii awamu ni ya 5 na makamu akawa raisi ili amalizie muhula wake

ila kwasababu za kujipamba na kusifia ndo ikawa hvyo

kwaharakaharaka polepole anaonekana ana point.
 
tangu aondokewe na mpendwa wake akili yake imekaa tenge mazima.
 
Polepole Yuko sahihi, hapa hakuna Cha Awamu ya SITA Wala Shangazi yake! hii ni Awamu ya 5B l, na uhakika angalia Baraza la mawaziri ni Lile Lile la awamu ya 5A, IGP ni Siro yule yule, CDF ni Mabeyo yuleyule, nk watendaji ni walewale, na majuzi kawarudisha hata walowahi kutemwa na JPM kwa mfano Januari Makamba, Makame Mbarawa, Ashatu Kijaji, Sofia Mjema, Ombeni Sefue nk! hii ni awamu ya 5B msidanganyike na hawa ndio wanamuangushia gari bovu Rais! [emoji2]
 
Naona wanasiasi wanaanza kuziogopa namba witiri kwenye awamu. Hawataki ajaye aitwe awamu ya saba bali ndo awe awamu ya sita. Lakini wakumbuke hakuna awamu yenye marais wawili. Kama Polepole anataka iwe awamu ya tano asubiri mama akimaliza mhula wake amshawishi atakayekuja ajiite awamu ya sita.
 
Tuendelea kuomba uzima , tuone Tanzania itafikia wapi.
 
Polepole ana ng'ata na kupuliza ....Huyu anataka kuongea ukweli ila anasita ,(ataonekanaje na ccm)

ndo maana mnatumia nguvu kubwa kumwelewa

leo yuko mweupe ,kesho mweusi keshokutwa njano mkimfuatilia mtauumia vichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…