Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,683
- 149,887
Kumsikiliza huyu mtu kwakweli inataka moyo maana anavyojibu maswali sometimes inatia hasira sana na anadhani watanzania hatuoni usanii anaoufanya wa kukwepa maswali ya msingi,kujibu blaa blaa na kutoka nje ya maswali anayoulizwa.
Kilichonikera ni kutetea uhakiki usioisha wa wa watumishi wa umma baada ya kuulizwa swali na mtangazaji wa star tv ni lini zoezi hili litafika mwisho.
Katika jibu lake anatetea kuwa zoezi hilo linahusu idadi kubwa ya watumishi wa umma ambao amesema wanafikia 1000,000!
Je,hii ni kweli?
Watumishi wa umma wanafika milioni moja?
Kama nimesikia vibaya kuhusu hiyo idadi niko tayari kukosolewa lakini hivyo ndivyo nilivyomsikia tena karudia kama mara mbili kutaja hiyo idadi.
Nilichogundua Polepole ni bingwa wa kupotezea maswali, kujibu maswali kiujumlajumla,kutumia muda mrefu kuelezea au kufafanua mambo yaliyo nje ya swali au maswali anayoulizwa huku akiwepa maswali ya msingi.
Mtangazaji Cyprian Msiba leo kupitia Star tv umejitahidi kumbana asitoke nje ya maswali husika na umetusaidia sana kujua huyo bwana ni mjanja mjanja katika kujibu maswali anayoulizwa.
Mliofuatilia kipindi hiki bila shaka mtakuwa na mengine mengi ya kuongezea.
Mada ilikuwa ni miaka 40 ya CCM.
PolePole wewe ni member hapa JF kwahiyo kama unahisi nachosema sio hasa kuhusu hiyo idadi ya watumishi ulioitamka tunakuomba ujitokeza hapa ukanushe au utoe ufafanuzi lakini kiukweli ulivyojibu baadhi ya maswali mengi binafsi hujaniridhisha mimi kama mimi.