Uongozi ni hekima na karama, Sio kila mtu ni kiongozi mzuri, Kuna watu wamekuwa viongozi kwa bahati mbaya ( By Default)
Humphrey Polepole aliamini ukipata nafasi ya uongozi wa nchi ni daima na milele yaani Immortal(Hakuna kufa wala kumuachia mtu nafasi) Aliamini anayekupa chakula hawezi kufa
Humphrey Polepole huyu aliaminiwa na JPM kama msemaji wa chama cha Mapinduzi CCM ambacho walikiasisi kwa jina Lao jipya yaani CCM mpya bila makubaliano yeyote na wanachama wakaita CCM kama CCM mpya
Humphrey Polepole mtu aliyeamini uchaguzi wa siasa ni kufanya fujo na vurugu, Uchaguzi wa mwaka 2020 alitamka maneno yote ya dharau kwa wana CCM kuwa atawakata mikasi wale wote watakaoenda kinyume na matamshi yake, Wabunge wengi walioshinda kura za maoni walikatwa kwa amri ya Humphrey Polepole
Humphrey Polepole aliamini mtoto anaweza kumdharau Baba yake au Mama yake aliyemzaa na kumtangulia hapa duniani kisa tu mtoto ameota sharubu kama kambare( Catfish), Kambare hata akiwa mtoto anakuwa na ndevu, Ni ngumu kutofautisha Kambare(Catfish) kwani hata kambare mtoto ana ndevu
Humphrey Polepole kwa kujiona Kambare aliwakajeli viongozi wa awamu zilizopita atakavyo, Aliwaunga mkono akina Ally Hapi na magenge yao kuwa wazee wastaafu watulie wanaweza wakawajibu lolote watakalo na walifanya hivyo
Humphrey Polepole, Huyu ni moja ya wale waliojisahau na kujiita wazalendo kuwa wanalipigania Taifa la Tanzania kwa miaka mitano 2015 mpaka 2020 wakijisahu kuwa kabla ya Tanzania walikuwepo wazalendo halisi waliipigania Tanganyika huru
Humphrey Polepole Leo amegeuka mwombaji( Beggar) ili atuletee wawekezaji toka Malawi, Kutoka mtu aliyekuwa anatamka kauli kali na za dharau kwa watanzania kama Catfish, "Unaijua Vietee, Unajua? Vieite wewe"
Ni vyema huyu mtu baada ya muda akapotezewa na akafutwa kazi ya ubalozi kimya kimya
Taifa hili halipaswi kurudi kwenye makosa ya utawala wa vijana na watu wa aina ya Humphrey Polepole wanaoamini mawazo yao na matamshi yao ndio Sheria, Wale wote wanye mawazo mbadala waliitwa wasaliti
View attachment 2289410View attachment 2289412View attachment 2289413