Humphrey Polepole ‘awashukia’ Kinana na Makamba

Humphrey Polepole ‘awashukia’ Kinana na Makamba

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,298
Reaction score
38,438
Polepole amenukuliwa akiwatupia vijembe vinavyoonekana kuwalenga Makatibu Wakuu Wastaafu wa ccm baada ya kukacha mahojiano juzi huko Dodoma.

"Wakati Rais anamuagiza Waziri Mkuu kwenda kukagua makontena bandarini yupo kiongozi mkubwa wa Chama sasa ni mstaafu alikuwa ana makontena 700 Bandarini na hayajalipa Kodi, alivyoambiwa alipe kodi sasa ana korosho hivi moyoni kanuna vibaya mno" Polepole

“Ukizingua kwenye chama chetu hakuna mkubwa wala mdogo wote mnaitwa, ukikimbia huna tofauti na wapinzani tu, na watu wa hovyo kwenye chama chetu waondoke tu'' Polepole.

9512D081-25ED-4E08-8A89-E839F755D505.jpeg
373AED63-76F7-4DAD-9AE2-F2D7ABB17F12.jpeg


Chanzo: Dar Mpya

==============
NB: Kama Kiongozi alikuwa ana Makontena 700 na hakutaka kuyalipia kodi ilikuwaje haikutangazwa wakati ule, anakuja kutangazwa saizi baada ya kugoma kuhojiwa?

Je, huko CCM kuna wanachama wangapi wanamadudu lakini sababu ni watiifu hamuwatangazi mnasubiri wakikosee chama ndio muwatangaze?

Kwa uzoefu wa Utawala huu je, tutarajie hawa wastaafu kupewa kesi za uhujumu Uchumi kwa kuonekana kukiabisha chama?
 
Saizi polepole anaanza kusema rais. Yeye anavyozungumzia mambo ya chama asiihusishe serikali kuwa rais aliagiza makontena. Yeye ajikite kisema mwenyekiti wa chama. Mambo ya kumzungumzia rais ni msemaji wa serikali au ikulu.

Tudai katiba nzuri ambayo haimuunganishi rais kuwa na vyeo vingine mfano mwenyekiti wa chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haka ka chakubanga bhana....

Kalikuwa kanamwita Lowassa fisadi alipokuwa upinzani. Tena hakakuishia hapo bali alimwita mgonjwa anayejinyea.... alivyorudi CCM hatukasikii tena kakibweka...

Yaani mtu anaonekana mchafu akitoka CCM...
 
Hivi kweli Mzee Kinana awekwe kwny Kitimoto.na kina Pole pole kujibu Maswali yaliyotengenezwa na Albert Msando yule wa Gigy Money?

Hata kama ni kumtukana Kinana tutafute matusi ya hadhi yake!

Mzee Makamba ni boshen, anaetafutwa ni Jongwe Comrade Abdul rahman Omar Kinana Alhabshy!

Kazi kubwa inayowakabili kina Pole pole ni kulinda Mapinduzi ya 1964 kwny Uchaguzi huu lakin wao kwa ugen wao wa Siasa wanadhan kazi kubwa ni kumsambaratisha Mzee Kinana ambae kwa hiyari yake aliamua kuacha Ukatibu Mkuu!


Unaenda kucheza Mechi ya Fainali lakin uko busy kutuhumu na kudhalilisha Bench lako la ufundi na Kamati ya Ushindi

CCM imevamiwa na Nzige wanaohatarisha Uhai wa Chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saizi polepole anaanza kusema rais. Yeye anavyozungumzia mambo ya chama asiihusishe serikali kuwa rais aliagiza makontena. Yeye ajikite kisema mwenyekiti wa chama. Mambo ya kumzungumzia rais ni msemaji wa serikali au ikulu.

Tudai katiba nzuri ambayo haimuunganishi rais kuwa na vyeo vingine mfano mwenyekiti wa chama.
Ni ngumu kutofautisha CCM na Serikali hasa kwenye madudu yanayoendelea nchini.!
 
Back
Top Bottom