Humphrey Polepole awaomba polisi, CHADEMA wasilinde kura

Humphrey Polepole awaomba polisi, CHADEMA wasilinde kura

CCM bila msaada wa polisi hawana chao, si mnaona wanaomba msaada wa polisi wawazuie Chadema wasidhibiti wizi wa kuara.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakilindi kura kwani hilo si jukumu lao.
pOLEPOLE.jpg

Polepole amesema hayo leo Februari 15, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mdogo wa Ubunge na nafasi za udiwani ambao unatarajia kufanyika Februari 17 2018 na kudai kuwa mpaka sasa wamepata taarifa kuwa CHADEMA wanachukua watu kutoka mikoani kuja kulinda kura kitu ambacho hakikubaliki.

"Zipo nyumba kadhaa hapa Dar es Salaam ambazo zimehifadhi watu wasio wakazi wametoka mikoa mbalimbali kuja hapa kwa kigezo cha kulinda kura, sisi hatufanyi siasa za matukio wala kutafuta kiki baada ya kujua hili tumewajulisha jeshi la polisi juu ya nyumba hizo na watu hao, kitakachofuata ni kushugulika na watu hao ambao hawapendi utaratibu mzuri na desturi yetu nzuri ya uchaguzi"


Polepole aliendelea kusema kuwa

"Kura hazilindwi na watu wanaoletwa kwa makundi bali kura kwa mujibu wa Katiba, Sheria ya uchaguzi na kanuni mbalimbali za uchaguzi zimewekewa utaratibu wa kisheria kuhakikisha mwenye yake na anaipata hiyo, upo utaratibu wa mawakala kila chama kina wakala huyo ndiye atakayeshiriki kuhesabu, kujua hii kura yangu au si yangu sasa unapoanza kuandaa watu wasiojulikana na kuwaleta Dar es Salaam ni kuleta taharuki na mpango huo msingi wake ni kutisha wakina mama, vijana na wazee wasijitokeze kwenda kupiga kura, tumesema jeshi la polisi tafadhali tena tafadhali sana watu wasiohusika na usimamizi wa zoezi la uchaguzi ni sheria hawapaswi kuwepo wanatakiwa kuwepo kwenye maeneo yao wakafanye kazi zao za kujiletea kipato, uchaguzi haulindwi na mabaunsa, kura hailindwi bali dola ina vyombo vyake ambavyo sisi wote vyama vya siasa tumekubaliana" alisisitiza Polepole

My take:

Hapa naona polepole kaanza kucheza na akili za chadema huu uchaguzi hauko vizur kwa upande wa ccm wanahangaika sana washakabwa.
Haya ni Matokeo Chana ya Kutotatua changamoto, zingine za makusudi zinazo Tokea Kwenye Chaguzi zetu Itafika Mahala Watu Wataitafuta Haki kwa Mtutu Wa Bunduki ama kwa Mapanga Shaaa! Hivi Hatujifunzi Kwa Yanayo Tokea DRC ? We Need a Free and Fair Elections, 'Say No For Greedy Leadership'
 
Polepole ni alama ya unafiki uliotamalaki ndani ya sisiemu..
 
Kisheria Kazi ya kulinda kura ni ya wakala aliye chumba cha kura huko nje wanalinda nini? Hizo ni kazi za mawakala wa chadema au hawawaamiini?

Tuliwaambia kwamba hamkubaliki mnalazimisha, sijui mnataja miradi ya maendeleo mkidhani watu watawakubali. Mkajifanya kununua viongozi ili muonekane mnakubalika, lakini saa hii kila mtu anawaona mnavyolazimisha kushinda uchaguzi kwa mauaji na ukatili wa kila aina. Zile kelele za kutamba kwa ushindi wakati cdm wamesusia uchaguzi ndio niliwapuuza kishenzi, toka lini ufunge goli lililowazi kisha ushangalie kama sio mwendawazimu.

Umma uliokuwa hauamini kwamba ccm huwa wanashinda kimizengwe na ukatili saa hii wanashuhudia kila mnachokifanya.
 
Anaandika HALIMA MDEE

HILA ZILIZOPANGWA UCHAGUZI 17/2/2018 (JUMAMOSI):KINONDONI, SIHA na KATA MBALIMBALI

Makamanda wenzangu na watanzania wote wapenda mabadiliko. Naandika andiko hili nikitambua kuna kampeni zinaendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Kampeni hizi zimeudhirishia umma kwamba CCM , Magufuli na SERIKALI yake haikubaliki miongoni mwa watanzania walio WENGI. NIMESHIRIKI kampeni za nyumba kwa nyumba na kampeni za JUKWAANI... ninachokisema, ninakijua na ninakimaanisha!

HATA hivyo, kama ambavyo walifanya katika chaguzi za kata 43 , ndivyo hivyo wanatarajia kufanya kwenye CHAGUZI za kesho kutwa! NAANDIKA hapa ili SOTE KWA UMOJA WETU TUSHIRIKI KUZUIA UDHALIMU HUU KWA HALI NA MALI: MAUMIVU YA UDHALIMU HUU wa UTAWALA wa KIDIKTETA USIPOZUIWA hakuna atakayesalimika.

NITATOA MFANO WA KINONDONI ( hivi ndivyo itakavyokuwa kwenye maeneo mengine yenye uchaguzi):

1. Mchezo huu unachezwa na TUME ya TAIFA ya UCHAGUZI kwa kushirikiana na CCM , mchezeshaji mkuu akiwa ni MKURUGENZI wa Manispaa ya KINONDONI. Huyu tayari ameshatoa maelekezo kwa watendaji wa kata (makada na wasio makada) kwamba atakayemtangaza mpinzani mshindi hana kibarua . Hii UTEKELEZAJI wa MAAGIZO ya DIKTETA UCHWARA ambaye anaishi mjini kwa KODI zetu watanzania masikini. Najua hili linajulikana.. wengi walidhani mzee aliongea akiwa na FRUSTRATIONS, na kwamba anapenda sana Wanyonge... KAULI yake inaendelea kutekelezwa. Na anaisimamia

2. Wasimamizi Wasaidizi wa UCHAGUZI ni viongozi wa CHAMA Cha Mapinduzi wa wilaya za ILALA na TEMEKE wenye nafasi Zifuatazao; Makatibu Tawi, Waenezi Tawi, Wenyeviti wa VIJANA, MAKATIBU wa VIJANA, Viongozi wa Hamasa na Watumishi wa MANISPAA ya KINONDONI ambao ni MAKADA wa CCM ( ikumbukwe MKUU wa IDARA ya UCHAGUZI KINONDONI ni kada wa CCM kindaki ndaki). Kama TUME inabisha iweke MAJINA YA WASIMAMIZI WA KILA KITUO WAZI NA UTAMBULISHO WAO WAZI !

3.Karani Mwongozaji ambaye ana jukumu la kupokea wapiga kura na kusoma majina yao kwenye daftari atakuwa mmoja wa wenyeji ambaye jukumu lake litakuwa ni kutoa Siri kwamba Mpiga kura fulani ni CDM/CUF nk . Wakitoa vitambulisho vyao wanaambiwa majina yao hayako kwenye daftari. ( MAWAKALA IMARA WATAZUIA MBINU HII) Na wapiga kura imara wakikomaa kuhakiki kwenye Daftari ,watayakuta.


4.Zimepangwa mbinu mahsusi za kuhakikisha kwamba mawakala wetu wanatoka Au hawaingii vituoni mapema. Moja wapo ni hili la viapo ambalo MKURUGENZI wa Kinondoni ameendelea kuvishikilia viapo. Pili watalazimisha mawakala watoe vitambulisho ( na sio barua ya utambulisho kama takwa la sheria za uchaguzi linavyotaka na wanasema hili wakijua kwamba watanzania wengi hawana vitambulisho) Ni mbinu tu ya kuhakikisha vituoni hakuna mawakala kwa saa kadhaa ili kura ziingizwe kwenye maboksi na Masimamizi wa uchaguzi KADA.

5. Licha ya KWAMBA wasimamizi wa UCHAGUZI hawatoki KINONDONI. Wamejiandikishia ILALA na TEMEKE na hawapo kwenye Daftari la KINONDONI mkakati ni kupiga KURA. KINONDONI kuna vituo 653 , wasimamizi na wasimamizi wasaidizi kwa kila kituo jumla ni 5: 653x5= 3065 . Hizi ni KURA ambazo sio halali lakini KAILIMA NA MKURUGENZI wa KINONDONI wanasimamia utekelezaji wa Wizi Huu!! Mawakala wana Jukumu katika hili .. LAKINI kubwa zaidi sisi watanzania tuna wajibu MKUBWA wa kuzuia hili!!! Tujitokeze kwa wingi kama walinzi nje ya VITUO

6. Polisi wamewekwa standby kwa kazi maalum (Hili sitalisema HAPA nina mahali pa kulisemea)ILA kwa ujumbe huu nataka wajue tunajua kazi waliyotumwa. Haitofautiani sana na waliyoifanya KATA ya Mbweni na kata nyingine nchi nzima.

7. Katika MKAKATI wa kujiwekea uwigo wa ULINZI ili alazimishe kumtangaza MGOMBEA wa CCM. Kituo cha majumuisho kimehamishwa toka BIAFRA kwenda OFISI YA MIURUGENZI KINONDONI . Hii ni option ya mwisho kama itatokea mawakala wetu wamesimama imara na Wameweza kuwa na matokeo, MKURUGENZI katika kutekeleza amri ya BOSI wake MAGUFULI atamtangaza Mgombea wa CCM mshindi kwa nguvu chini ya usimamizi wa JESHI la POLISI kisha atoe majibu kama ya KAILIMA kwamba twende MAHAKANI. Hili nalo linahitaji kuzuiwa na WATANZANIA WOTE na sio kumuachia mgombea na wakala wa majumuisho. Huu udikteta unaopandikizwa KINONDONI, SIHA. KATA 43 , ndio utaenda hitimishwa kwenye uchaguzi wa 2019 na 2020 utatuathiri wote!!!! Uwe na CHAMA au LA... Tukiruhusu GENGE la wahuni liamue mustakabali wa MAISHA yetu, hakuna atakayepona

Niwatakie wana Kinondoni / Siha na kata mbalimbali uchaguzi mwema. Nina imani licha ya HILA ZA SHETANI. Tukisimama kwa UMOJA WETU, pasi kuogopa vitisho vya VYOMBO vya DOLA na KUWA IMARA kama askari wa miguu ndani na NJE ya VITUO!! Tutaushinda uovu huu !!LAKINI tukikaa pembeni na kufikiri kwamba suala hili la uchaguzi sio LETU ni la wanasiasa MKONO wa CHUMA utaendelea kumgusa kila mmoja wetu....kama ambavyo wengi hawakutuelewa tuliposema TUUJENGE UKUTA Kuuzuia UDIKTETA ... sasa wengine wameanza elewa.. TUSHIKAMANE TUOKOE TANZANIA YETU NA KUTUMA UJUMBE kupitia sanduku la KURA!! Tupige KURA, TULINDE KURA!! Mungu ibariki TANZANIA !
 
Tuliwaambia kwamba hamkubaliki mnalazimisha, sijui mnataja miradi ya maendeleo mkidhani watu watawakubali. Mkajifanya kununua viongozi ili muonekane mnakubalika, lakini saa hii kila mtu anawaona mnavyolazimisha kushinda uchaguzi kwa mauaji na ukatili wa kila aina. Zile kelele za kutamba kwa ushindi wakati cdm wamesusia uchaguzi ndio niliwapuuza kishenzi, toka lini ufunge goli lililowazi kisha ushangalie kama sio mwendawazimu.

Umma uliokuwa hauamini kwamba ccm huwa wanashinda kimizengwe na ukatili saa hii wanashuhudia kila mnachokifanya.
Ushindi ni ushindi uwe goli la mkono wote ushindi
 
Polepole na chama chenu acheni wananchi wa Kinondoni waamue ya nini kusumbukaaa?!
 
mi nikishapiga kura ntabaki kuilinda kura yangu mpaka ikihesabiwa!
 
Ushindi ni ushindi uwe goli la mkono wote ushindi

Nimeshukuru cdm wameamua kushiriki na kudhibitishia umma kwamba ndio chama kinachokubalika. Sasa ni dhahiri ccm inang'ang'ania madaraka na wala haikubaliki. Lengo kubwa la kushiriki cdm kwa sasa ilikuwa ni kuweka rekodi sawa kwamba ccm haikubaliki. Jengeni SGR, sambazeni maji, jengeni barabara, nunueni viongozi wa upinzani lakin umma hauwakubali. Hamna kitu kigumu kama kulamisha kuvuta riziki kwa kamba.
 
Ccm bila kuiba kura na kutumia polisi wasiojua wajibu wao hawawez kushinda hata jimbo moja
 
Polepole na chama chenu acheni wananchi wa Kinondoni waamue ya nini kusumbukaaa?!

Hawawezi kuacha kutumia nguvu maana wanajua hawakubaliki na wanaona aibu kukataliwa, hivyo wako radhi kulazimisha ushindi wa fedheha. Hii inadhibitisha kwamba hao viongozi wa upinzani wanaohama kwenda ccm wananunuliwa na sio kwamba ccm na Magufuli wanafanya vyema.
 
Nyie magamba leteni uduwanzi wenu, safari hii mtaonana na muumba kwa njia rahisi sana.
 
Nimeshukuru cdm wameamua kushiriki na kudhibitishia umma kwamba ndio chama kinachokubalika. Sasa ni dhahiri ccm inang'ang'ania madaraka na wala haikubaliki. Lengo kubwa la kushiriki cdm kwa sasa ilikuwa ni kuweka rekodi sawa kwamba ccm haikubaliki. Jengeni SGR, sambazeni maji, jengeni barabara, nunueni viongozi wa upinzani lakin umma hauwakubali. Hamna kitu kigumu kama kulamisha kuvuta riziki kwa kamba.
Karibu sanduku la kura karibu sana tukutane kesho kutwa uone mziki wa CCM baada ya matokeo nakungoja hapa jamii forums ila ushauri wa bure uwe na namba karibu ya daktari wako wa magonjwa ya presha usije kutufia tukakosa mchangia mada jamii forums kwa kufariki kwa presha baada ya mshituko wa tangazo la matokeo ya uchaguzi
 
Polepole wa Katiba mpya na huyu wa sasa ni sawa na mbingu na dunia.

Kabudi wa Katiba mpya na huyu wa sasa Waziri wa Sheria ni sawa na mbingu na dunia.

Madaraka ni mwana malevya
 
Chama hakina hatia ila waliomo ktk chama ndo mwiba,me cjui km wanaendaga ibadani,mana mioyo yao haina chembe za utu na upendo,nakereka na kaul zao sn...natamani Lumumba waambulie 20% ya kura zote wactafute vucngzio.
 
Karibu sanduku la kura karibu sana tukutane kesho kutwa uone mziki wa CCM baada ya matokeo nakungoja hapa jamii forums ila ushauri wa bure uwe na namba karibu ya daktari wako wa magonjwa ya presha usije kutufia tukakosa mchangia mada jamii forums kwa kufariki kwa presha baada ya mshituko wa tangazo la matokeo ya uchaguzi

Hamuwezi ushindani kila mtu ameona jinsi mnavyofanya hujuma za wazi. Mnaweza kutangazwa washindi lakini sio kushinda. Roho yangu ingeniuma na kufedheheka iwapo ccm ingeshinda kihalali. Lakini mpaka sasa nafurahi hata kama ccm itatangazwa washindi nimejiridhisha kwamba wananchi hawarubuniki kwa kuwa wanajitambua. Kesho kutwa mnaweza kutangazwa hata kushinda kwa asilimia 95% lakini ukweli uko wazi kwamba watu wamewachoka. Zile kelele za kwamba cdm wamesusia uchaguzi kwa kuogopa kushindwa rasmi zimefutika kwani sasa mko wazi kuliko wakati mwingine wowote. Bigup sana cdm.
 
Back
Top Bottom