Nimefuatilia michango na uamuzi uliotolewa na waheshimiwa wabunge kuhusu sakata la utomvu wa nidham wa wabunge wawili Mh. Ester Bulaya (Bunda) na Mh. Halima Mdee (Kawe) lakini naomba kutoa mchango wangu kukosoa uamuzi ule mtukufu.
1. Ninaona kuwa, hisia nyingi za wachangiaji zilitoka kuwajadili wabunge hawa kama wao na sio kama wawakilishi wa majimbo yao zaidi.
2. Adhabu waliyowapa hawa wabunge baada ya kuwaona kuwa wakosefu, hauikuzingatia uwepo wa hawa wabunge pale bungeni, yaani sababu za wao kuwa pale bungeni.
3. Adhabu stahiki ni kuwafukuza ubunge kwa sababu adhabu zoote weshazimaliza (Kwa maneno ya m/kiti wa kamati yako tukufu). Hivyo, tuwarudishie wana jimbo kuwa mlio mleta bungeni hajui alicho fuata, hivyo tupeni mwingine.
4. Naomba mh. Spika, unisamehe kwa kukuambia kuwa; Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba HAKIKA ninakuheshimu, lakini siku za hivi karibuni, umeonyesha kutokuimudu sawasawa nafasi yako. Kumbuka; Wewe ni baba pale bungeni unapo kikalia kile kiti. Baba wa yule mmbabu aliye mbunge na ni baba wa yule mtoto mdogo sana pale bungeni aliye mbunge.
Sasa kama baba; Naomba nikushauri kuwa, Unatakiwa kuwa Mvumilivu, Mstahimilivu, Mpole na Mwerevu.
Ukitaka kuuma kidogo upande flani, baba spika using'ate, tumia ujanja/werevu wa panya. Uma na kupuliza. Using'ate hadi damu itokeze. Hata mlevi huamka usingizini panya akimng'ata.
Kweli, baba, leo umeonyesha kuwa wewe ni mtu wa hasira sifa ambayo sio nzuri kwa kiongozi wa watu wengi.
Yawezekana; kama wanavyo sema sema. Atii, weye upo pale bungeni kuzilinda na kuzitekeleza, sera za chama tawala. Sawa kabisa. Ila elewa kuwa, bunge lile sio la chama kimoja bali la vyama vingi. Hivyo tumia kofia yako kuiongoza serekali sio serekali ikuongoze. Utakuwa umeliyumbisha bunge.
Mh. Spika, niachie tu hapa nisije litia tembo maji.