Hukumu ya Mdude Nyagali hatma ni leo

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,685
3,549
Mungu wa Ibrahimu, Isaack, Yakobo hata Yusufu, asubuhi leo nasogea mbele ya kiti chako kwa unyenyekevu, lakini kabla ya kusogea mahali patakatifu pako naomba kutibu maovu yangu ya kuwaza, kuona, kutamani, kusikia, kunena kwangu na kuonja kwangu kinyume na mapenzi yako.

Mungu wangu ni Mungu mkuu sana mwenye kuogofya, mwenye utisho mwingi wa rehema ikiwa maji ya Bahari ya Shamu yaliogopa ukuu wako na kuacha njia watumishi wako wakapita kwani Leo utabadilika? Ikiwa Joshua alikuomba jua lisimame hata Vita iishe kwani leo wewe ni Mungu wa tofauti? Ikiwa wayahudi walifunga bila kunywa Wala kula Hadi wahakikishe Paulo kafa kinyume chake ulimtembelea Paulo na kumwambia ikiwa umeweza kunitangaza hapa Basi huna budi kusimamia mbele ya kaisari kwani leo wewe Mungu umebadilika?

Nakuita kutoka kwenye kiti cha enzi simama na geuka na kusikiliza maombi ya mtumwa wako asubuhi ya leo, nakuadhimisha eeh Mungu wangu daima siku zote fanya hima kumtoa mtumishi wako kwenye kinywa cha shetani na ukamweke huru daima nami nikashuhudie matendo yako makuu.

Ikiwa Mungu kwangu nilikuona kwa viwango vya ajabu hata huwa mpaka leo nabaki kushangaa matendo yako endelea kunishangaza Tena leo hii juu ya mtumwa wako Mdude Nyangali.

Nasimama kutubu kwa ajili yake Mdude, natubu kwa Raisi wangu mama Samia na wasaidizi wake wote, natubu kwa jaji Mkuu, natubu kwa hakimu anaesimamia kesi ya Mdude, natubu kwa wakili mtetezi wa Mdude najua ni watu wako japo nao ni binadamu Wana makosa hivyo wasamehe daima.

Baba nasimama kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth, ikawe kinyume na nguvu zote za giza na kushindwa kama shetani ulivyomshinda pale msalabani.

Kwa jina la Baba na la mwana na roho mtakatifu ameen!
 
556.jpg

Atatoboa kweli?
 
Anatoka lakini somo alilojifunza kila mkubwa atamuamkia hata watoto atakuwa anawapa shikamoo ujinga wote umemuisha; alikuwa anajuwa kila mtu wa kutukana hovyo hakuheshimu mamlaka aliona ni kama anaongea na Mbowe hapo harudii tena na iwe fundisho kwa vijana wote wenye mawazo kama yake.
 
Wameenda kumpokea bingwa wa matusi, yaani inaonyesha ni kiasi gani chama kilivyo cha kihuni mtu kama huyo mnaona ni shujaa yaani mlivyo wajinga mnaweza kumfananisha hata na mandela ni lichama la kihuni sana Chadema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom