Hukumu ya kwanza ya kesi za EPA

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Kesho tunatarajia hukumu ya kwanza ya kesi za EPA katika Mahakama ya Kisutu. Hukumu hiyo itakayosomwa na mahakimu watatu ambao ni Saul Kinemela, Focus Bambikya and Elvin Mugata itakuwa dhidi ya mfanya biashara kada wa CCM Rajabu Maranda na Farijali Hussein wanaoshtakiwa kwa kuiba Sh 1.8bn/- kupitia akaunti ya EPA.
 
Hivi huyu kada wa CCM Farijala nae sio magamba!? Nape yupo wapi atupe jibu..
 
Kesho tunatarajia hukumu ya kwanza ya kesi za EPA katika Mahakama ya Kisutu. Hukumu hiyo itakayosomwa na mahakimu watatu ambao ni Saul Kinemela, Focus Bambikya and Elvin Mugata itakuwa dhidi ya mfanya biashara kada wa CCM Rajabu Maranda na Farijali Hussein wanaoshtakiwa kwa kuiba Sh 1.8bn/- kupitia akaunti ya EPA.

Masikini ya Mungu mweh sijui hasira ya magamba kuvulia itawaacha?
 
Hadithi ya Pwagu na Pwaguzi itaisha lini? Lipapa lenyewe liko Ikulu tena anwani inajulikana Magogoni street, nyie mnakamata vikambale tu - S t u p i d - I d i o t s !
 
Pengine inaweza kuwa mwanzo wa Tanzania mpya - Tanzania bila ufisadi. Tusubiri tuone...strange things do happen sometimes!
 
Kama waendesha mashtaka ni wale walikuwa chini ya Chenge! then waka chini ya John. Mwanyika aliye durufu miradi ya Richmond na Dowans na sasa wapo kwa F.M Werema!

Sijui.
 
Lets wait and see how professional lawyers are not helping this country because of their worries!
 
Wale akina Patel mbona kesi yao imesimama kwa muda wa miaka mingi sana? au kwa vile ni wahindi na majela yetu siyo kwa ajili ya wahindi?
 
Hao ni kutupoteza tu sisi huku wanaodhani akili zetu hazifanyikazi. Wangetoa hukumu ya Kagoda ya Billions nyingi na sio hii ya bilion 1.8 tu. Ngoja tuone kama wataendelea na hukumu zile za wizi mkubwa mkubwa
 
Hawa hawapo kwenye wale ambao tulisema wakikamatwa nchi itayumba hivvyo wamrudishie rais wetu kwa siri.
 
Haitatokea hata siku moja kada wa CCM akafungwa na mahakama inayoongozwa na kada wa CCM!! Maranda na Farijala wataachiwa huru lwa sababu ya technicality kuwa fedha hizo hazikuwa za serikali na wenyewe wenye fedha hawakuleatwa mahakamani kama mashahidi wa upande wa mashitaka!! case closed; na zitakazofuata itakuwa hivyo hivyo!!
 
Kesho tunatarajia hukumu ya kwanza ya kesi za EPA katika Mahakama ya Kisutu. Hukumu hiyo itakayosomwa na mahakimu watatu ambao ni Saul Kinemela, Focus Bambikya and Elvin Mugata itakuwa dhidi ya mfanya biashara kada wa CCM Rajabu Maranda na Farijali Hussein wanaoshtakiwa kwa kuiba Sh 1.8bn/- kupitia akaunti ya EPA.

Mkuu wametuchakachua...hukumu imehairishwa mpaka mei 21............kuna nini hapa kama sio mchezo mchafu.......
 
Back
Top Bottom