Hukumi ya Sabaya viongozi wa kuteuliwa tumieni akili zenu.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,729
2,000
Utetezi wa Sabaya ulizihusisha mamlaka za uteuzi. Mazingira yanaonesha kuwa Kuna ukweli fulani kwenye madai yake hayo ya utetezi.
Ushahidi wa madai yake kwamba alikuwa anatekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi yanatiwa nguvu na uwepo wa wateuliwa wengine ambao walikuwa wakiwafanyia vitendo vibaya wananchi bila kuchukuliwa hatua na mamlaka zao uteuzi.

Kila mtu alikuwa anashuhudia namna vituo vya utangazaji vikivamiwa, watuhumiwa wa madawa ya kulevya walivyoteswa, wanaume waliokuwa wanatuhumiwa kuwatelekeza wake zao na watoto walivyokuwa wakishughulikiwa, viongozi wa upinzani walivyokuwa wakishughulikiwa, wafanyabiashara wakwepa Kodi walivyokuwa wakiadhibiwa, nk bila kuchukuliwa hatua zozote na mamlaka zao za uteuzi.

Tatizo la baadhi ya wateuliwa wetu ni kuitupa mkono sheria na kukumbatia maagizo ya mamlaka za uteuzi hata Yale yanayokiuka sheria na Katiba.

Orodha ya wateule wanaotekeleza amri haramu kutoka juu ni ndefu sana nchini, Mimi ninaamini kwa moyo wangu wa dhati kuwa Iko siku hukumu kama ya Sabaya itawakuta wengi sana kuanzia askari hadi viongozi wa serikali na siasa.

Kujiuzulu kwasababu ya kupewa maagizo haramu ya kinyume Cha sheria, katiba, kanuni, Mila na desturi na mamlaka yako ya uteuzi ndiyo kinga pekee kwenye kupata adhabu kama ya Sabaya.
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,033
2,000
Serikali imeamua kumshughulikia Sabaya peke yake utadhani ni yeye tu alifanya makosa, wapo mamia ya viongozi waliofanya maovu makubwa nao washughulikiwe.
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,729
2,000
Wateule waliofanya mabaya kaama au zaidi ya Sabaya kwa wananchi wenzao ni wengi sana. Tuwatafute na tujitokeze kwa wingi kutoa ushahidi dhidi Yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom