Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,354
- 29,305
My people,
Ukifuatilia kile kinachofanywa na wanaharakati hakika utashangaa huwa wanafikiria nini?
Baada ya kupanga tarehe za maandamano na Serikali kuchomoa waya kwenye betri kila uchwao,sasa wanakuja na idea nyingine
Wanataka kuandamana siku ya sikukuu ya Krismass,sababu ni kwamba siku hiyo ni lazima watu watoke waende makanisani kwahiyo serikali haiwezi kuwazuia
Hii ni kuonyesha mbinu zote sasa zimeshindikana sasa wanataka kuzinajisi sherehe za kidini,huu ni ujinga mkubwa mnataka kufanya
Wananchi msikubali huu ujinga hata kidogo,ni wakati sasa wa kutumia akili zenu na sio kufuata au kufanya kila mnachosikia in the name of kuikomboa Tanganyika
Tukubali kwamba tumeishiwa power na hatuwezi kuiangusha serikali ya Mama Samia, sasa tujikite zaidi kupeana elimu ya katiba ili kesho au kesho kutwa mchakato ukianza basi tuwe tunajua yapi ya kuwepo na yapi yasiwepo
Haya makelele ya Maandamano hayana tija tena,sio muda wa kuleta taharuki na kupoteza amani ya nchi yetu,kumbuka mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na mbomoa nchi mwananchi mwenyewe
Kwa niaba ya Team Amani,wakiwemo Invisible Mafia
iamwangdamin
adriz
stakehigh
Na wengine aluta continua
Ni hayo tu!