GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,216
Kwa mara ya nne ( 4 ) sasa nimekuwa nikisikia kuwa kila ziara ambazo Mheshimiwa Rais wetu JPM amekuwa akizifanya Mikoani hasa katika uzinduzi wa Miradi mbalimbali amekuwa akidanganywa ( kuingizwa mjini sana ) na wale waandaaji / wenyeji wake wa Kimkoa.
Na kibaya zaidi ni kwamba kila akienda huwa anaizindua hiyo Miradi kwa mikogo na bashasha zote lakini akirejea tu Dar es Salaam taarifa huja na kusema kuwa miradi X,Y na Z ambayo Rais JPM aliizindua ilikuwa ama haijamalizika au haijakidhi vigezo na ameingizwa tu mjini ( kapigwa changa la macho kadanganywa ).
Hii hali imenipelekea nianze kujiuliza maswali mengi ya Kitafakuri na sijapata majibu bado na naona Kichwa changu kinaniuma tu kwa mawazo juu ya Mama Tanzania.
Je mnadhani ni kwanini Mheshimiwa Rais JPM anadanganywa sana na Watendaji wake hasa katika miradi mbalimbali ya Serikali? Je ukali wake uliozoeleka machoni mwa Watanzania sasa umeanza kuonekana wa kawaida tu au? Je ni kwanini mnadhani hao Watendaji wanaomdanganya kutwa juu ya Miradi ya Serikali hawaogopi wala hawamwogopi na wanathubutu kumdanganya? Hivi kabla ya Rais kwenda kuzindua mradi fulani nini hutakiwa kutangulia kufanyika? Je hii hali ni Kiashirio cha nini hasa Kiutendaji kwa siku zijazo katika nyanja nzima za Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii?
Nitashukuru kwa michango yenu na naomba kuwasilisha.