Hujuma Ubalozi wa Tanzania Sweden | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hujuma Ubalozi wa Tanzania Sweden

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichakoro, Sep 11, 2008.

 1. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Ndugu wanabodi,

  Tanzania sasa tunahujumiwa hata na balozi zetu, hii sasa inatisha kisa chenyewe kiko hivi.

  Mimi ni Mtanzania ninaishi Denmark ingawa sio mwanachama rasmi wa umoja wa watanzania hapa Denmark (TANDEN). TANDEN ilifanya summer party 30.08.2008 lakini kawaida ya party zao huwa zinatanguliwa na mada za kuitangaza Tanzania na hasa utaliii kwani siku hiyo huwa inawaleta watu wa mataifa mbali mbali hivyo TANDEN hutumia wasaa huo kuitangaza nchi yetu of which is very good.

  Aliyetoa mada kuhusu Tanzania kwa kweli alinigusa na alielezea kwa ufasaha vivutio vya Tanzania na hata girl friend wangu amehamasika kwenda Tanzania. Tulipomuomba mtoa mada kuhusu vipeperushi ambavyo mtu akitaka kusoma zaidi ndipo nilipogundua hujuma yenyewe. Maelezo yake ni kama ifuatavyo:

  Ubalozi wa Tanzania Sweden kwanza uliombwa kuleta bronchure za kuitangaza Tanzania (Tanzania the Land of Kilimanjaro, Seringeti and Zanzibar) ambazo serikali imetumia gharama nyingi kuzichapisha na kisha kuzisambaza kwenye balozi zake zote.

  Cha kushangaza kila waaandaji walipojaribu kuwasiliana na ubalozi waliambiwa zitakuja wasiwe na wasi wasi. Cha kusikitisha Zaidi baadae zikaja taarifa oooh ni gharama kuzisafirisha. wakati wanasema ni gharama balozi alikuja Denmark 25.08.2008 kwa ajili ya seminar ya kuwavutia wawekezaji wa kidanish kwenda kuwekeza Tanzania, Hakuleta hakutaka hata kuonana na watanzania waishio Denmark.

  Ila alikuwa na nafasi ya kuonana na wanaCCM mimi nikiwa ni mmojawapo mike, Mzee msimbazi na wengine tuliokutana shame uponi you balozi. swali mtauliza hujuma iko wapi????

  Moja serilkali imetumia gharama kuchapisha vipeperushi ili viwafikie watu na sio vikae kwenye maboksi kwenye ofisi za balozi hivyo hela za walipa kodi hazikutumika kama ilivyotarajiwa je balozi hajahujumu uchumi?????

  Pili kama aliweza kuja hapa Denmark na delegation yake walishindwa hata kuja na vipeperushi ishirini ambavyo havifiki kilo moja wakati ni hela za walala hoi zimetumika kuwgharamia safari yao, sio hujumaa hiii????????

  Kuna tetesi kwamba anaondoka ama anabadilishwa kituo, ila habari za uhakika nilizozipata ni kwamba anastaafishwa kwa manufaa ya UMMA, lakimi je kustaafishwa ama kuhama kituo kunakufanya mtu asitimize wajibu wake???? Je ndio aliamua kufanya retaliation kwa njia hiyo??????

  Tunao mabalozi wengi wa aina Dr. Ben Moses sehemu nyingi ni muda wa kusema HATUWATAKI.

  OMBI kwa ndugu Mh. Kikwete sasa umefika wakati wa balozi zifanye kazi kwa manufaa ya watanzania wote waishio nje na wale waliopo nchini. HIVYO MTU UTKAYEMLETA KAMA BALOZI SWEDEN HAKIKISHA NI MCHAPA KAZI, MZALENDO, MPENDA MAENDELEO, ANAYEPENDA KUTUMIKIA KULIKO KUTUMIKIWA, na ZAIDI YA YOTEASIWE FISADI

  Ndugu zangu Watanzania popote mlipo tuchukue jukumu la kuitangaza Tanzania kama wenzetu wa TANDEN wanavyofanya, Tuwaumbue mabalozi wazembe bila woga wala kumuonea.

  Kilimanjaro ni yetu, Kiswahili lugha yetu na Tanzania nchi yangu,

  asante
   
 2. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Kichakoro, poleni sana...! Hivyo ndio hali halisi ya Balozi zote za Tanzania, yaani zinakera...! Mabalozi wetu wapo kwenye ubalozi kwa ajili ya kusubiri kuhudhuria dhifa na sherehe tu...! Tena, nimejaribu kufuatilia, watu wengi wanaoteuliwa kuwa mabalozi huwa ni baadhi ya maafisa wa serikali walioshindikana sasa sehemu ya kuwatupia inakua ni huko ubalozini...! Hawana taaluma yoyote kuhusu foreign policy, tourism and sovereign advertisment...!

  Wengi wa mabalozi na Foreign Service officers (FSO) wanapewa nafasi hizo kwa kujuana zaidii kuliko ufanisi....! Wengi wanafurahia kwenda huko nje wa ajili ya kutembea tu na sio kwenda kufanya kazi....!

  Balozi nyingi huko nje hazina msaada wowote tena unapopata shida ukienda ubalozini unonekana kama ni mhalifu tena unadharauliwa....!

  Pole sana kaka....!
   
 3. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nami pia nampa pole zangu ndugu yetu Kichakoro.

  Lakini ndugu yangu Mhafidhina, sio kwamba balozi zote za Tanzania zina matatizo hayo.

  Mfano Balozi wa Tanzania katika nchi za BeNeLux (Kingdom of Belgium, the Kingdom of the Netherlands, and the Grand Duchy of Luxembourg) huwa anashirikiana vizuri na WaTanzania waliopo katika nchi hizo. Hata mfano ulio hai alituma vipeperushi, video za kuitangaza Tanzania na maliasili yake na hata kushiriki yeye mwenyewe sherehe za usiku wa mwafrika zilizofanyika chuoni UNESCO-IHE kilichopo jijini Delft, tarehe 15 mwezi wa 8 mwaka huu.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Majungu.....
   
 5. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Masatu Si udaku

  Mimi ni mdau hapa Denmak kwanza namshukuru mdau aliyeweka hiyo post.
  Aliyo sema ni kweli na nimewasiliana na viongozi wa TANDEN wamenihakikishia ni kweli aliyoandika huyo bwana ni kweli na kuna zaidi ya hilo ila kwa sababu si msemaji wa TANDEN na sio mwanachama nachelea kusema mengi zaidi.

  Ni kweli Balozi alikuja hapa Copenhagen kwa mwaliko wa serikali ya hapa aje kuelezea vivutio vya uwekezaji Tanzania. kwa habari zaidi soma www.um.dk/da/menu/Udviklingspolitik/Erhvervssamarbejde/PrivatSektorProgrammer/Nyheder/InformationsmoederOmErhvervsdelegationTilTanzaniaAfholdtDen13Og26August.htm
  sorry maana ipo kwenye lugha ya kigeni hii kudhirisha kweli balozi alikuepo

  Pia kuna dada niliongea naye siku ya part huyo dada anaorganise safari kwa wanaotaka kwenda kutalii nyumbani na yeye anatoa same complain.
  kwa ujumla ubazo wetu sweden ni Kero hivyo kama kweli anaondoka basi akapumzike kwa amani.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Alipewa na nafasi hiyo na si mwingine bali fisadi Mkapa akiwa amebakisha miezi mitatu kumaliza awamu yake. Kisa 'wameoa nyumba moja' juhudi kama hizi za kuwapinga mabalozi wazembe na mafisadi labda zinaweza kuzaa matunda na hatimaye kuteuliwa mabalozi wenye uwezo tu, lakini hii serikali dhaifu iliyo madarakani sidhani kama inaweza kufanya lolote kwa sababu JMK anaogopa sana kuwagusa wote walioteuliwa na fisadi Mkapa sijui sababu kubwa ya hili ni kitu gani au ndiyo udhaifu na woga ja JMK.
   
 7. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lakini suala la kujiuliza ni kuwa wanapoteuliwa wanapewa terms of reference zikiwa na majukumu gani?.....kuna evaluation yoyote inafanyika kila baada ya mwaka kujua balozi ametekelezaje majukumu yake?...manake tunaweza kuwalaumu wao kumbe hata mamlaka zinazowateua hazijui katika uchumi wa kisasa wa dunia mabalozi wanatakiwa wafanye nini.
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  deny_all,

  umeuliza swali la msingi sana......Dr Ben Moses ni kati ya ma-PS wachache waliojijengea sifa sana katika uchapaji kazi.............sijui imekuwaje
   
 9. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Ogah

  Sina uhakika na usemalo lakini jiulize ni kitu gani huyu bwana amekifanya kwenye huu ubalozi wa Sweden (scandivia and Baltic region). Kama ni kuorganise sisi wanaccm kwa kweli amefanya kazi maana tuko intouch nae kila mara kwa kila jambo na tunapata ushirikiano wa kutosha. Lakini je yupo kwa ajilia ya chama ama watanzania?????

  Weekend hii nilijaribu kudodosa kwa msiri wake mmoja hapa DK, nilichogundua ni kwamba yeye hakuna ties kubwa na mheshimiwa, so alikua anajaribu kujikita mizizi kwenye chama ili profile yake iweze kupata support kutoka kwenye chama. Pili kama mnavyojua Katibu wake ni Mtoto wa makamu mwenyekiti Msekwa, amekuwa akimtumia pia kufikisha nia yake hiyo lakini inaonekana kugonga mwamba ndio maana amekuwa akifanya anayoyafanya.

  Msiri huyo anasema tatizo lake jingine ni kukaa nje muda mrefu na kusahau hali halisi ya nyumbani na hata kuamini kwamba watanzania wa leo ni sawa na wale wa miaka ya 90s wa ndio mzee kila kitu.

  kingine ni muoga ama mgumu wa kudelegate power kwa watu kufanya kazi hivyo kutaka kufanya kila kitu yeye mwenye mwishowe kushindwa kutekeleza ama kuchelewa kutekeleza. Katika yote ameshindwa kuwa karibu na watanzania waliopo kwenye nchi anazozisimamia, badala yake amekuwa akijihusha na makundi fulani fulani ambayo nayo yanachochea mgawanyiko wa watanzania waliopo katika nchi hizo.

  Swali: Je ni jambo gani Dr. amelifanyia taifa ama watanzania waliopo Scandinavia na Baltic region watamkumbuka nalo??????

  Jibu: Kwa sisi wa Denamrk ni hii hujuma sijui wa nchi nyingine watsema lipi.
   
 10. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  bowbow
  nashukuru kwa kufuatilia na soma ujumbe niliokutumia kwenye PM yako
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kichakoro,

  .......kwa kweli..............I personally understand your frustrations.....inaudhi sana kwa kweli.........it was very logic kwa Balozi na timu yake kuwaletea hivyo vitu mlivyoomba toka ubalozini..........ndio maana najiuliza hii commonsense........imekuwaje kwa Dk Ben Moses

  NOTE: kama alivyosema deny_all hapo juu...............
   
 12. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi nilizozipata hivi punde kuwa Dr. Moses sasa ameshakabidhi rasmi ofisi kwa aliyekuwa msaidizi(Bwana Msekwa) ambaye atakaimu office hadi balzi mpya atakapotangazwa.

  Swali kwa Dr. Ben, Je kwa nini usichukue wasaa huu kuwashukuru na kuwaaga watanzania waliopo kwenye nchi za baltic na scandinavia kwa kuwatumikia ama
  kuwashukuru kwa ushirikiano ulioupata kutoka kwao??????

  Tafsiri yangu ya kushindwa kufanya hivyo ni kuwa labda hukuwa na ushirikiano nao
  ama hukuwa unawatumikia wao bali......

  Nakutakia kila la kheri kwa kile utakachokuwa unafanya baada ya kuwatunikia watanzania
  kwa wakati wote ukiwa hapa Canada na huko scandinavia. Mapumziko mema
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kichakoro,

  Kwanza heshima mbele sana, hii kitu nilikuwa sijaiona kwa kweli inasikitisha sana, I promise kwamba hii post yako nitaifikisha kwa waziri Membe by Jumatatu.

  Ahsante Mkuu.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa nini unauma na kupuliza ? Hivi Tanzania kwa nini tuna hii tabia ya kusujudia viongozi hata wanapovurunda ?

  Wewe ukikutana njiani na huyo Balozi sijui utamchekea chekea na kumpongeza au utamkazia uso ? Wabongo tuache huku kujinyenyekeza kwa Wabukwa wasiotujali.

  Huyu Balozi wa Sweden ana distinction ya kutajwa Bungeni na Waziri Kawambwa wa Miundombinu kwamba arudishe nyumba mbili za Serikali alizojinunulisha kinyume na utaratibu! Hana sifa nzuri huyu. Sasa huku "kumtakia mapumziko mema baada ya kututumikia" wakati ushasema inawezekana hakuwa anatutumikia sisi mimi sikubaliani nako.
   
 15. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #15
  Oct 18, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  common sense is very uncommon!
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,667
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hapa Tanzania ukijikomba kwa rahisi(I mean rais) unapewa ubalozi siku hiyo hiyo. Believe me.
   
 17. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nyinhyi watu wa Denmark mmezidi sana uswahili. kama kuna balozi anayewajibika katika historia ya ubalozi wetu Sweden basi ni huyu mzee Ben Moses. Kama kuna Mtanzania ambaye hajawahi kumuona huyu mzee akiwajibika, basi huyo Mbongo anakimbia yeye mweneye, huyu mzee ni bingwa wa kutafuta watu wake na kuwasaidia kwa kadiri anavyoweza. Hapa Finland kwa kweli tunajivunia sana kuwa na balozi wa aina yake na tunampa bravoooooooo.
   
 18. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35

  Acheni unafiki, majina ya waliojiuzia nyumba wametajwa na Ben Moses sio mmojawao, tafuteni jungu lingine.
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Bob,

  Huyu balozi aliwahi kuwepo huko kwako mkuu, wewe ninakuaminia sana tuweke sawa hapa kuhusu record ya huyu balozi alipokuwa huko,

  maana naona yale yale ya chuki, ukabila na undugu yameshaanza hapa!
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna unafiki ni kweli Balozi Ben Boses na Dr Edna Moses "walinunua" nyumba 2 wakati utaratibu ni familia moja nyumba moja kama kiambatanisho hapo chini;

   
Loading...