Huenda ikawa tatizo ni pesa ...sawa,je wanaume?

Huenda ikawa tatizo ni pesa ...sawa,je wanaume?

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Kuna siku moja niliwahi kusoma utafiti mmoja na utafiti ule ulikuwa unaonesha kuwa baadhi ya vyakula tunavyokula nyakati hizi vinasababisha wanaume kuingia kwenye ushoga,yaani ni kwamba vyakula hivyo unapovila huamsha homoni ambazo ni kinyume na jinsia na kupelekea mwanaume ambao ametoka tumboni kwa ***** akiwa salama kabisa kuanza kutamani kujiingiza kwenye kutamani ushoga au kuufanya kabisa

Nilijiuliza sana kuhusiana na ukweli ulioko kwenye uitafiti huo na bahati mbaya hawakutaja aina ya vyakula lakini walisema kuwa vyakula hivyo ni vile vya kwenye maduka au "masupamaketi"

Nilikuja nikatafakari tena kuhusiana na vurugu zilizoko kwenye kujamiiana,nyumba ninayoishi iko jirani na nyumba moja ya kulala wageni ambayo ni ya kiwango cha kati na mara nyingi kila ninapokuwa nyumbani huona watu wakipishana sana pale na wote wanaonekana kuwa wanakwenyda pale kwaajili ya short time tu na sio kulala,ilinibidi nimuulize yule mhudumu pale kwasababu namfahamu na aliniambia kuwa kwa siku moja huja watu waaina tofauti tofauti sana pale vijana kwa wazee walioolewa na wenye wake.

Nilijaribu kufanya na kautafiti kadogo kengine kwenye nyumba zingine za kulala wageni na kukuta vurugu ni zile zile yaani hakuna tofauti,hapo ndipo nilipojiuliza maswali mengi sana sababu ya vurugu na kasi hii kubwa ya watu kujamiiana hivi

Nilifikiria kuhusiana na sababu ambayo imekuwa ikitolewa sana na wengi kuwa wanawake ndio wanafanya ngono kwasababu ya pesa lakini niliona sababu hii haiko sawa na haitoshi kabisa kwenye suala hili yaani imepwaya sana.Kuna wake za watu ambao hali zao ni nzuri sana na hawahitaji kuhongwa na unakuta wanakwenda kufanya uzinzi na vijana wadogo ambao wao ndio wanaowawezesha,lakini pia kuna wengine wanakwenda kufanya mapenzi na waume za watu ilhali wao nao ni wake za watu pia tatizo ni nini?

Unaweza kusema kuwa hao wanawake hawatimiziwi mahitaji yao huko kwenye ndoa,je hao waume zao ambao wanatoka na wake za watu nao vipi?hawatimiziwi nao au kuna kingine hapa?

Kama mko kwenye ndoa na mmechokana kama wengine wanavyosema,hivi huko unakokwenda nako hutapazoea kama huko ndoani?Inamaana watu hawa hawajui hili?Kama wanajua ni kitu gani kinawafanya wanaendelea kufanya jambo ambalo linaonekana wazi kabisa kuwa halina faida?

Hawa ambao hawako kwenye ndoa nao ni vituko,vijana wa kiume wamekuwa wakiwarushia "madongo" vijana wa kike kuwa wanapenda wanaume ambao wana fedha,lakini ni kweli vijana wa kiume hawafanyi ngono hovyo?Jibu liko wazi kabisa kuwa nao wanafanya hiovyo pia,je nao tatizo lao ni nini? au ni Pesa?

Kimsingi jambo hili kudai tu ni pesa au kutokutoshelezwa ni kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu kwani wanaofanya umala.ya ni vijana wakiume na wakike ambao hawajaolewa na walioolewa pia.Wamama na wababa nao wamo kwenye hili na wanafanya ngono na vijana na wamama na wababa wenzao pia

Kama mtu yupo kwenye ndoa na haotshelezwi na mwenzake hii inamaana kuwa huyu hawezi kuwa na hawara,lakini inakuwaje anakuwa na uwezo wa kuwa na hawara wakati kwenye ndoa yake anadaiwa hamtoshelezi mwenzake?

Kwenye jambo hili naweza kuandika mengi sana lakini kwa hayo tu mnaweza kuona kile ninachokifikiria kuwa ni kipi

Imekuwa ikisemwa sababu ya wanawake kuingia kwenye jambo hili lakini sikumbuki kama iliwahi kusemwa sababu ya vijana wa kiume na Wanaume kuingia kwenye jambo hili

Suala la pesa kwa wanawake linapwaya sana ukiangalia kiwango cha kujamiiana kilichopo nyakati hizi,lakini pia kwa upande wa vijana na wanaume hakuna kilichosemwa kinachosababisha jambo hili lakini nadhani ni wakati wa kufikiri na kutafakari hasa sababu ni kitu gani,Mabinti wanakuja hapa wakilalamika kuwa vijana uwezo wao umeshuka wakati huko mitaani wana mahawara kibao,hili linawezekanaje?

Kazi iupo hapa!
 
anaefanya ngono kwa pesa ni yule anejiuza[directly au indirectly]....wengine wanafanya kwa starehe[ndani au nje ya ndoa] au kutafuta watoto
 
Suala la kuendeleza uzinzi limekua kubwa sasa kwa jamii zetu, na hili naweza kusema sio kua wanawake masikini sana ndio wanafanya ili wapate hela na wala wanaume ndio hawaridhiki kua wanafanya ili waridhike zaidi, hapana ni MAOVU na kuendekeza MAOVU, nilipata kuongea na rafiki yangu mmoja kaniambia unaweza ukaona watu wa rika lako wanafanya machafu mpka ukajiona ivi mimi ni mzee wa kiasi gani? Mbona kama napitwa? Ni nafsi tu ya mtu, malezi, vijiwe, mitandao na kuiga tamthilia
 
anaefanya ngono kwa pesa ni yule anejiuza[directly au indirectly]....wengine wanafanya kwa starehe[ndani au nje ya ndoa] au kutafuta watoto

Starehe ya kasi hii ndugu?
 
Suala la kuendeleza uzinzi limekua kubwa sasa kwa jamii zetu, na hili naweza kusema sio kua wanawake masikini sana ndio wanafanya ili wapate hela na wala wanaume ndio hawaridhiki kua wanafanya ili waridhike zaidi, hapana ni MAOVU na kuendekeza MAOVU, nilipata kuongea na rafiki yangu mmoja kaniambia unaweza ukaona watu wa rika lako wanafanya machafu mpka ukajiona ivi mimi ni mzee wa kiasi gani? Mbona kama napitwa? Ni nafsi tu ya mtu, malezi, vijiwe, mitandao na kuiga tamthilia

Mkuu inawezekana ukawa unasema kweli maana hili la hela ni kama halienei hivi!
 
Kwa upande wangu naona kufanya ngono ni tamaa, mob decision na curiosity ya kujaribu vipya.

Siamini katika mapenzi ya pesa.
 
Wengi ni kwa Tamaa, kukosa hofu ya Mungu na uvivu wa kufikiri,kama maisha ni magumu hiyo nguvu na muda anaoutumia kitandani ana uwezo wa kwenda kuitumia kuzalisha kazi halali.

Tamaa tu na kukosa hofu ya Mungu,unakuta mtu anapata kila kitu kwa mumewe au mkewe lakini bado anachepuka,basi unakuta watu anaotoka nao ni aibu tu,ukimuuliza lipi analolifaidi hana hoja zenye mashiko,watu walidhike na walivyo navyo,ndo maana kuna msemo unasema utamaliza bucha zote nyama ni ile ile...

uvivu wa kufikiri,mtu amepishana na mkewe au mumewe anaona solution ni kuchepuka,huko huendi kupoza moyo bali unaenda kuongeza matatizo,tatizo linapotokea kaa chini tulia solve tatizo maisha yaendeleee,wengine wanaona fasheni kuwa na mademu wengi huku ni kukosa kufikiri,wanaiga maisha ya nje ni ulimbukeni tu.

Vijana wengine sijui hata wakoje,unakuta anafanya kazi zake kwa taabu sana lakini haishi kwenda kuhonga,hadi unajiuliza sasa huyu mtu ana shida gani si aoe atulie na mmoja? Ni wakati wa kuacha tamaa kila mmoja alidhike na alichonacho,na tutafaulu hili iwapo tuna hofu ya Mungu,tuogope dhambi.
 
Ukiondoa hofu ya mungu kutokuwepo miyoni, wengine ni kutaka kujaibu fleva mpya zaidi ya wake zao au waume zao, na hasa hii inatokana na maneno ya waliotunguuka nasi tunataka kujaribu.
lakini lingine kubwa zaidi kwa wanaume ni tamaa na ulimbukeni unaosababishwa na hali ya kifdha kubadilika kwa maana kuwa nzuri ukilinganisha hapo zamani...
 
Back
Top Bottom