Huenda hii ikakusaidia siku moja ili usiibiwe hela kwenye ATM

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
HUENDA HII IKAKUSAIDIA SIKU MOJA!

Endapo utavamiwa na majambazi na wakakulazimisha kuwatolea pesa kwenye ATM, ili kuokoa maisha yako, wala usitaharuki.

Unachopaswa kufanya ni kuingiza namba ya siri kinyume. Kwa mfano kama namba yako siri ni 1234, basi ingiza kama 4321.

Ukimaliza tu kuingiza tarakimu hizo, pesa zitaanza kutoka lakini zitakwama katikati. Ikitokea hivyo, taarifa kwamba kuna uhalifu unatendeka kwenye ATM hiyo itatumwa kwa Afisa Usalama wa benki husika na Kikosi cha Polisi bila ya
m/wahalifu kujua.

Kila ATM ina mfumo huu, bahati mbaya ni kwamba mabenki hawawaelimishi wateja wao kuhusu tahadhari hii.

Wasambazie taarifa hii ndugu, jamaa na marafiki wote, huenda ukaokoa maisha ya mmoja wao.

ATM.jpg
 
View attachment 464460
Mkuu tuchukulie mfano namba ya siri ikawa 1991, kwa njia zako ulizozieleza tuingize neno la siri kinyume, huoni kama kuna exception na mtu ataibiwa kama kawaida.
 
Kwa wataalamu wa masuala ya IT wanajua hiki kilichoandikwa hapa ni uongo, PIN ya ATM Card inavyohifadhiwa kwenye mifumo ya kibenki ni tofauti kabisa na jinsi unavyotegemea, hiyo PIN huwa encrypted

e.g. 1234 inaweza kuweka kama 3u3747rudueu383828282uwuwu2828w

Na vilevile PIN nyingine inayofanania i.e. 1234 itakuwa encrypted kwa usiri tena kwa mfumo mwingine kama 3737rururueueie8384848rururu484848

Ni ngumu sana kwa hizo PIN kufanana na ni ngumu sana hata kwa mfumo wa ATM kujua kua umegeuza PIN yako i.e. 1234 kujua inauhusiano na 4321

Hii taarifa ni ya uongo na inapotosha watu ilwahi kuenezwa hata hapa kwenye hii link utajionea

PIN Reversal Hoax - Cybercrime - Advice and Support - North Wales Police

Hakuna kitu kama hicho na hakiwezekani.
 
Mkuu
Je utengenezaji wa vocha hutumia mfumo wa ENCRIPTION?
 
Kwani unafikiri majambazi ni watubaki... ni hao hao wafanyakazi wa bank ndo wezi wenyewe.....
Umesema kweli kabisa.

KUNA WIZI UMETOKEA BENKI

Jambazi akasema "wote laleni chini pesa
ni za serikali na maisha ni ya kwenu",
wote wakalala chini (HII INAITWA
DHANA ...YA USHAWISHI - kubadilisha
njia ya
kawaida ya kufikiria)

Kuna dada kwa woga akawa
amelala chini kimitego, Jambazi
akamwambia, "dada hebu kuwa
na adabu chukua kanga jifunike hili ni
tukio la ujambazi na sio la
ubakaji.? (HUU UNAITWA WELEDI -
zingatia ulichofundishwa kufanya)
Walipotoka kwenye

wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada
ya uzamili ya biashara akamwambia
mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha.? Yule
mkubwa akamcheka
kwa dharau na kumjibu, "wewe
mjinga sana hizo hazina haja ya
kuhesabu saa mbili wata tutangazia
kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi
gani. (HUU INAITWA UJUZI - Siku hizi
ujuzi ndio bora kuliko vyeti)

Baada ya majambazi
kuondoka meneja akamwambia mhasibu
wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80
tulizo iba sisi.? (HUKU KUNAITWA
KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI -
kushabihiana na mazingira magumu kwa
faida binafsi.)

Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi
ukitokea kila mwezi itakuwa burudani
sana.? (HUKU KUNAITWA KUWA NA
MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha
muhimu zaidi)
Meneja kafurahi sana

kwa kuwa sasa matatizo yake
yametatuliwa
na wizi uliojitokeza. (HUKU KUNAITWA
KUTHUBUTU-shiki lia nafasi pale
inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi
gani.

Haya usiku wake
taarifa ya habari
ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa
million 100 umetokea leo benki.
Majambazi kuskia hivyo wakaanza
kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na
milioni 20 tu.

Yule jambazi mkubwa akashtuka na
kusema, "dah! yaani meneja kaiba mara
nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli?
Bora umeneja kuliko ujambazi.? (HII
INAITWA

ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana
elimu ina nguvu kuliko chochote.)
Nice weekend
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom