Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Mimi naomba kuuliza kama ni sahihi kwa mtu ku-request huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi(mobile banking) na kukatwa fedha kwenye simu yako bila kujali kama huduma uliomba umepata au hujapata.
Kwa mfano,unaweza kuuliza salio lililopo katika akaunti yako ya benki na ukiwa katikati ya process, mtandao ukakati lakini wao hela kwenye simu na kwenye akaunti wanakata bila kujali umepata huduma au laa.
Nachojiuliza jambo hili ni sahihi?
Huu sio wizi?
Kwanini system yao isikate hela baada ya mtu kupata huduma anayoihitaji?
kwakuwa wako huru kukata hela bila kujali umepata huduma au hujapata,hali hii haiwezi kuyafanya mabenki au kampuni za simu kutojali na hivyo kutoboresha huduma zao kwasababu hakuna wanachopoteza?
Kama hivi ndio vigezo na ndio mashariti yenyewe ya kuzingatia,je,wanatutendea haki wateja?
Nashauri mamlaka zinazohusika, iwe ni wizara ya fedha au Benki Kuu, kutazama upya swala la hili na ikiwezekana ziwekwe sheria,kanuni au taratbu zitakazodhibiti utoaji huu mbovu wa huduma kwa wateja na wakati huo huo wanawatoza watu fedha bila kujali wamekuhudumia au laa.