Huduma Za Hindu Mandal Hospital Ni Mbovu. Kigwangalla Wamulike

kipoke KIPOKE

Member
Apr 20, 2015
54
9
Kwa masikitiko makubwa nikiwa mgonjwa leo hii nilienda kupata huduma hapo lakini majibu niliyoyapata ugonjwa ukaongezeka.

Kuna mama ambaye ndio supervisor anajibu watu utafikiri ni polisi "Kama huna namba tutapata wapi, tumesema kaa huko utaitwa" kwa sauti ya hasira.

Ukiwahi saa moja kamili kutoka ni mpaka saa sita mchana. Harafu kitu kingine.

Wale wenye watu wao mafaili yanabebwa na manesi wanaingia hapo reception wanaingiza majina ya ndugu zao na wanatoka mapema kabisa kama huna ndugu Hindu Mandal sio pa kwenda.

Kuhusu wafanyakazi nina uhakika kabisa wameletwa watoto wa ndugu na hao wazee wasifikiri wanahudumia watoto wao pale ni community wawajibu watu kwa maadili ya utumishi na wakizingatia wengi wanaoenda pale wanakuwa wagonjwa.

Upande wa wauguzi sina shaka huduma ni nzuri tatizo ni wahudumu wa nje maana mpaka kumuona daktari ni zaidi ya masaa matano.

Sasa HAPA KAZI TU wataiweza. We bank on you DR KIGWANGALA.

Niombe tu uongozi wa Hindu Mandal Hospital angalieni wafanyakazi wa hapo reception fanyeni quality monitoring on customer care wagonjwa ni waoga hawawezi kuongea mimi nimejitolea nimeongea kwa niaba yao.
 
...ni kweli kabisa. Hospitali ya Hindu Mandal imekuwa kama zile Hospital za Serikali zinazopigiwa kelele kila kukicha...

Huduma za Hindu Mandal kuzipata ni mbinde...yaani unaweza kupoteza siku nzima pale...na muda mwingi unapotelea kwenye ma file kabla hata ya kumwona dr.....

Ni aibu kwa Hospitali hii ya private....tena aibu kubwa...maana hata ma file bado wanahifadhi manually.....hawana mfumo wa kielectronic hadi leo wa kuhifadhi ma file ya wagonjwa....matokeo muda mwingi unapotea kwenye kutafta ma file ya wagonjwa...

Yaani huwezi kuamini hii ni private hospital.....wameajiri cheap labor....ili wawalipe kidogo lakini matokeo yake ni ufanisi kushuka mno....aibi aibu.....
 
...ni kweli kabisa.. hospital ya hindu mandal imekua kama zile hospital za serikali zinazopigiwa kelele kila kukicha...huduma za hindu mandal kuzipata ni mbinde...yaani unaweza kupoteza siku nzima pale...na muda mwingi unapotelea kwenye ma file kabla hata ya kumwona dr.....ni aibu kwa hospital hii ya private....tena aibu kubwa...maana hata ma file bado wanahifadhi manually.....hawana mfumo wa kielectronic hadi leo wa kuhifadhi ma file ya wagonjwa....matokeo muda mwingi unapotea kwenye kutafta ma file ya wagonjwa....Yaani huwezi kuamini hii ni private hospital.....wameajiri cheap labor....ili wawalipe kidogo lakini matokeo yake ni ufanisi kushuka mno....aibi aibu.....
sasa kali zaidi tumeuliza muda wa kutupatia mafaili mama kasema hajui inaweza hata ikafika mchana wewe tulia basi haya tutulie wapi viti vyote vimejaa BORA mwananyamala kuliko Hapa
 
Hayo mambo madogo mkuu....Kigws hawezi ingilia customer care ya private hospital, tatizo ni mindset za hawa ndugu zetu sijui huwa wanajisikiaje wakiwa kwenye madesk, sio bank teller sio receptionists sio secretary yani ni tabu tupu........ wavumilie tu mkuu, pengine yuko kwenye mwez mpevu usimuharibie kibarua maisha yenyewe mjini mshike mshike
 
Kigwangala ni member wa JF hâta kuvamia kwa Dr year chanzo hapa najua atalifanyia kazi.kaza buti kigwa tunakusubiri kesho hindu mandal kama upo dar
 
Hayo mambo madogo mkuu....Kigws hawezi ingilia customer care ya private hospital, tatizo ni mindset za hawa ndugu zetu sijui huwa wanajisikiaje wakiwa kwenye madesk, sio bank teller sio receptionists sio secretary yani ni tabu tupu........ wavumilie tu mkuu, pengine yuko kwenye mwez mpevu usimuharibie kibarua maisha yenyewe mjini mshike mshike
ndugu wizara ya afya ndio inatoa vibali vya kuendesha hospitali kwa mashart mazuri tu ya kujali wateja ambao ndio sisi wagonjwa so ninauhakika Dr kigwangala ataingila kati na hasa akizingatia hii ni fani yake anajua masharti ya huduma kwa wateja hospitalini
 
Back
Top Bottom