Huduma za afya vijijini na malengo ya milenia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huduma za afya vijijini na malengo ya milenia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rugaijamu, Jul 13, 2011.

 1. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF,habari zenu! Kwa uchache ninapenda kuchokoza mjadala kuhusu upatikanaji wa huduma bora za afya vijijini,ambako zaidi ya 80% waTanzania wanaishi. Kwa miaka kadhaa sasa serikali imekuwa ikifanya jitihada za kupanua mtandao wa huduma hizi nchini,kwa kuhakikisha kuwa mwananchi hatembei zaidi ya umbali wa 5KM kufikia kituo cha huduma.Pia MMAM inataka kila kata iwe na health centre,kila kijiji kiwe na dispensary...ni vema! Lakini tujiulize swali;ikiwa tumeshindwa kuimarisha hizi health facilities chache;uhaba wa vitendea kazi,miundombinu duni,uhaba wa watoa huduma,vipi tumejipanga kwa mtandao mpana? Leo hii,kama lengo la kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi(maternal mortality rate) na vifo vya vichanga(infant mortality rate),dispensary zote zinatoa huduma za uzazi na kujifungua,je dispensary hizo zimewezeshwa kutoa huduma hiyo?Huduma za kujifungua hazina muda maalum(kujifungua hakuna ratiba),lakini dispensary hazitoi huduma saa 24 na wala hazilazi wagonjwa.Zina operate kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi tisa unusu alasiri,Jumatatu hadi Ijumaa.,hakuna shift.Nyingi zina watoa huduma wachache(hawazidi wa 3)baadhi yake zinaongozwa na medical attendants,miundombinu duni(hakuna privacy wakati wa kujifungua),vitendea kazi duni. Pia watoa huduma(hasa wauguzi wakunga)hawapewi hardship allowance wala risk allowance kwa mazingira magumu na hatarishi wanayofanyia kazi ili angalau kuinua ari ya utendaji kazi.Mtoa huduma huyo anaweza kufanyakazi zaidi ya muda unaotambulika(kwa mujibu wa sheria za kazi),anaweza hata kukesha na mjamzito kituoni kwake na asubuhi awepo kazini(hana mapumziko baada ya mkesha huo),lakini hapewi extra duty allowance.Je mtoa huduma huyu atafaoya kazi moyo mweupe kweli? 1.Je kwa hali hii tutawezesha upatikanaji wa huduma bora za uzazi vijijini? 2.Je kwa hali hii tutaweza kupunguza MMR na IMR? 3.Je huyu mkunga hastaili posho/motisha kama wabunge? NAWASILISHA!
   
 2. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  safi sana mkuu,
  nimependa hoja yako na huku ndko kwenye fani yangu.
  ninapiga kazi hapa kwa muda mkidogo kisha nitarejea na kukupa details za maana na uchambuzi yakinnifu, mtu kwenye taaluma yake utamfurahia tu.
   
Loading...