Umkondo wa Swize
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 282
- 89
Jana mwanangu alizidiwa usiku alikuwa anatapika nikamwahisha kituo cha afya cha serikali Sinza Palestina, kufika pale nikapata huduma kama kawaida kwa daktari akaniambia nimpeleke mwanangu maabara akachukuliwe vipimo ili wajue tatizo ni nini.
Kufika maabara nikakuta watu wengi wanamsubiri mtaalamu wa maabara ilikuwa mishare ya saa 4.30 usiku basi tulisota kwenye benchi pale mpaka saa 5;45 usiku jamaa hajatokea huyu wa maabara.
Hili Tray kama linavyo onekana ndipo unapaswa kuweka form au daftari kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo tulikaa pale mpaka saa 6.00 huyo jamaa wa maabara alikuwa hajatokea na mimi mwanangu alikuwa anatapika bado kumuuliza mlinzi akasema alikuwepo atakuwa katoka kidogo, fikiria toka saa 4.30 mpaka saa 6.00 usiku mtu wa kuchukua vipimo hayupo na haijulikani alienda kufanya zinaa au kulewa na kuacha kazi pasipo taarifa yoyote kwa wenzie, kuona hivyo mi nikaamua kuondoka na kumpeleka mwanangu kituo binafsi pale Manzese darajani St. monica na tukapatiwa matibabu. Serikali inabidi ianzishe patrol kwenye vituo vya afya kusudi kuwabana wale wafanyakazi wenye mtindo wa kusign na kuondoka kwenda kuendelea na shughuli zao binafsi. Usipo kuwa makini unaweza poteza mwanao/mgonjwa wako hivi hivi.
Sijui hao wenzangu nilio waacha walipata muda gani huduma. Wizara ya Afya liangalieni hilo.