kkarumekenge
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 1,708
- 1,028
Ndugu zangu watanzania, msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza ilikuwa ndo kimbilio la mamilioni wa Kanda ya Ziwa na sehemu nyingine nchini. Kweli ilikuwa ikitoa huduma bora. Leo hii, huduma za hospitali hii zimefikia kiwango cha chini, chini kabisa. Utaratibu wa kupokea wagonjwa ovyo, madaktari na madaktari bingwa wamepungua sana, matandiko tu ya vitanda vya wagonjwa ni kama matambara baadhi ya mashuka wanayojifunika ama kulalia wagonjwa yana matobo utadhani nyavu za kokoro, hao manesi, mbali na lugha chafu kwa wagonjwa hawafiki wodini, dawa ndo usiseme, gharama zake je, balaa nk. Sasa hivi wale wenye bima wapo kwenye majaribu, huduma inaegemea kwa wale wanaolipa cash. Hivi niseme nini Bugando? Peleka mgonjwa wako hutaamini kama hapo ni Bugando uliyokuwa ukiisikia. Kwa mfano, unatakiwa ukabidhi dawa za mgonjwa wako kwa manesi hawa wanatuhumiwa hawawapi wagonjwa hizo dawa, huzificha na kuziuza tena. Nilipeleka mgonjwa Bugando hii ya sasa, sikuamini kama bado inayo sifa ya kuitwa hospitali ya rufaa. Wamiliki wa hospitali hii naambiwa ni Kanisa Katoliki na serikali, ni vyema waiangalie Bugando kwa jicho la tatu, iko hoooooi. Ina maana uongozi wa hospitali ikiwemo kanisa na serikali hawajaona tatizo hili? Kwa hiyo Bugando mbali na kutoa tiba hata hospitali yenyewe sasa inatakiwa ipate tiba.