Kwa kuhusu hoja zako kwamba mwakani hatutokuwa na HTC naamini unaona wazi kuwa HTC is there to stay. Kuhusu apps sijui 1000 za Nokia kama nilivyosema mwanzo kuwa Nokia kushughulika na apps ni kupoteza muda, off course wanatakiwa wawe na apps kadhaa kwa ajili ya core service zao mfano google wana apps kama 50 na apple pia idadi kama hiyo halafu uwanja wamewaachia developers wafanye mambo yao.
Rational customer haweza kuchagua simu eti kwa sababu handset manufacturer ana apps 1000, lakini watu wanachagua simu (iPhone) kwa sababu platform ina apps 1,000,000 au Google kwa sababu android na apps 700,000. Na ndio maana kuna wakati Apple walikuwa na tangazo "There is an app for that"
Angalia jinsi Windows Phone ilivyo na ukame wa apps (150,000) tena Apps muhimu kama vile Hulu au Instagram hazipatikani kwenye WP. Kwa hiyo lets hope developers wataendelea kutoa apps lakini mwaka mzima wa 2012 WP imetoa apps mpya 75,000 ambapo Android na iOS hutoa idadi hiyo katika muda wa mwezi au chini ya hapo.
Kuhusu hoja kwamba WP inakua, ukweli ni kwamba wako mashakani kupoteza nafasi ya tatu kwa blackberry (hao BB wenyewe taabani) hivyo competitor wao sasa hivi ni BB sio Android wala iOS. Yaani platform yenye kampuni moja tu BB inakwenda sambamba na platform nzima yenye kampuni kadhaa (wote wana 6% market share by OS) hapo ndio unaweza kuona WP iko dhaifu kiasi gani.