HR, Waajiri walalamika wahitimu ni weupe vichwani

Nikweli kaka
 
Kuna HR mmoja fala sana,alinipigia simu haeleweki ata anahoji nini,ananiuliza ulifanya kazi wapi na wapi kwa muda gani wakati details zote zipo kwenye CV ambayo anayo!

Nilikata simu nikaona jamaa chenga sana!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
wahitim wa shahada kwenye fani ya UHASIBU na KODI niweupe kama wanafunzi wa kidato cha nne
Pia 96% ya wahasibu wa Halmashauri hawajui wanachokifanya.....naongea kama MKAGUZI hasa kuhusiana na Creditor control account
I can confirm this
 
Kila kampuni au taasisi ina malengo, wanapo kuajiri wanakuajiri as qualified candidate na uta fit malengo yao. Suala la kusema waajiri wana expetation yes , wako right, dunia ina change so wanataka candidates wana evolve na dunia, sio wanao kariri skills fulani halaf hawataki kuchange
 
Sahihi
 
Hii hoja ya msingi sana


Unakuta mtu una degree halafu mwisho wa mwezi unakula 300k au 400k. Hapo unakuwa kama mchina tu huachi ila ukiwa na 20k utapata kiswaswadu, ukiwa na 200k utapata Tecno na ikiwa na 2M utapata matolea mengine mazuri
Hehe na vijana wanaangalia maokoto kama mshahara wako ni tusenti nao watafanya kazi ya level hizohizo za tusenti
 
Unajua Watanzania tukishapata vifursa tunaona wengine mafala Sana. Kwa kifupi hata hao ma HR wanaosema hayo na wao wakati wanaanza kazi nao walikuwa weupe kabisa sema sasa washapata uzoefu wanaona wahitimu wengine kwamba hawajui kitu. Kwa kifupi mfumo huu wanaopitia wa sasa na wao walipitia huohuo
 
Jana nilipanda Bajaj na mtu mmoja nilikuja gundua anafundisha chuo kikuu. Akafungua Whatsapp kutokana na mwanga mkali wa simu yake nikawa interested kuona anafanya nini.
Akafungua groups kadhaa za wanafunzi wake mwishowe akaingia group la Registrar wa chuo, humo nadhani kuna lecturers wote. Kuna mmoja jina lake saved ni Adela ametuma mjadala eti WHO sijui UN imetangaza kuwa ujana ni mpaka miaka 50 (ni kama aliwaletea habari njema). Wakawa wanachangia kama vilaza humo huwezi jua ni wakufunzi wa chuo. Mwingine akadai eti watangaze kustaafu ni miaka 70, Adela ndio akaandika vijana watakosa ajira.

Huo mjadala ulifanya nijiulize kama hawa ndio wanafundisha, wanaofundishwa ndio itakuwaje? Hii nchi kumejaa vilaza kila idara, alafu sasa ajabu wana alama kubwa za ufaulu. Hata hao HRs wanaolalamika wamejaa vilaza kwelikweli.
 
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Hamasa ya kusoma pia imepungua kutokana na nchi ilivyo connection Kila uchochoro na mtu alishaaminishwa kusoma ni kutoba maisha(apate kazi nzuri)

Watu wamebaki kusoma Ili kuchukua boom ajichoshi sana akili na wakufunzi nao huwenda wanalisongesha tu.
 
Sikatai unachosema, ila maneno yote yasiwe katika kutoa majibu ya moja kwa moja... na kila mtu kuona hoja ya mwenzake haifai...

Nimefanikiwa kufanya kazi na maboss wa wawili tofauti... Tena wote ni ngozi nyeupe, mmoja alikuwa yupo poa, anakupa uhuru wa kufanya kazi ila tu usitoke nje ya lengo lake, unafanya kazi unakuwa na amani na hata ikitokea unafanya vibaya wewe mwenyewe unajistukia... Boss anasikiliza ushauri wako tena anaufanyia kazi ipasavyo

Huyu mwengine hafai hata kidogo, sababu ni much know, kila kitu anajua... hataki ushauri wa namna yoyote ile... analolifanya yeye ndio linafaa... ana standard zake hazieleweki na ukijaribu kumjulisha hapo hatuendi hivi... Hakuelewi, mwisho wa siku unafuata standard zake zikifeli anajua mwenyewe...

So si 100% kwamba wahitimu hawapo vizuri... Mpe mazingira mazuri ya ufanyaji kazi uone matokeo yake
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ yani vilaza ndio wanafundisha eti ujana mwisho 50 hahaha
 
wahitim wa shahada kwenye fani ya UHASIBU na KODI niweupe kama wanafunzi wa kidato cha nne
Pia 96% ya wahasibu wa Halmashauri hawajui wanachokifanya.....naongea kama MKAGUZI hasa kuhusiana na Creditor control account
Kuna vituko halmashauri utakuta wanakununilia lunch samaki mkubwa unabaki kuuliza shule mlisomea ujinga ni vituko tu, wanakimbia kimbia juu chini maswali yasiyo na msingi,eti mkaguzi umepata breakfast ?umefikia wapi ?,nilikwenda halmashauri moja nikamkuta mwanafunzi wangu niliyewahi kumfundisha miaka kumi na moja kabla ya mimi kuwa mkaguzi nilisikitika sana.The girl by that time aliongoza bookkeeping form four pia form six kitaifa akiwa Weruweru very intelligent.Kawa na akili za kilevi ,vitu vidogo hawajui kabisa.Tuna tatizo kubwa kwenye nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…