Mkuu vipi ukitaka kununu kitu online mfano ebay au Amazon hapo haisumbui?
Naamini haisumbui unaweza kulipa bila tatizo, tatizo linakuja katika kutumiwa huo mzigo - baadhi ya wafanyabiashara wengi kwenye Amazon na Ebay huwa hawaposti Afrika, kwa sababu wenzetu wa Nigeria wameshaharibu sana , mara waseme kitu hakijafika na huko nyuma waliwaliza wengi na fake paypal payments.
East Africa ni new territory kwa online business transactions na ina-catch up faster thanks to Kenyans, wao wakenya na wasauzi miaka michache nyuma ilikuwa kama bongo unaweza kutuma tu ama kununua kitu through paypal lakini ilikuwa huwezi kupokea lakini sasa unaweza kutuma na kupokea, bongo unaweza kutuma tu, na sio kwenye online business tu hata kama una jamaa yako unataka kumtumia hela Ulaya ama Marekani unahitaji kutumia email address tu na kumtumia hela as long as ana bank account na credit/debit card. Ni very easy na faster.
Pay-pal ni safe na inakulinda wewe mnunuzi na muuzaji vilevile through buyer/seller protection. Ukinunua kitu halafu kikawa sicho ama hukukipata unarejeshewa hela yako yote ilimuradi isizidi siku 45 tokea ununue hiko kitu. Lakini hii buyer protection haikulindi katika mauziano ya magari ama Nyumba na baadhi ya vitu vya thamani kubwa.
Transaction zote za paypal wanafanya kwa dola, wewe unatumia local currency na wanaconvert into dollar using current exchange rates.
Hio waliosema wakubwa hapo juu ya ku-deposit $1.95 ni account verification process, kwa sababu unapofungua akaunti ya pay-pal bado haijawa verified, hadi wao wajue na kukuamini na kuambatanisha pay-pal na bank account yako, huwa wanakutilia kiwango kidogo cha fedha kwenye akaunti yako mfano $0.95 na $1.70 kisha unapo- log kwenye account yako ya paypal watakwambia uingize amount waliyokutumia exactly kama inavyoonyesha kwenye akaunt statement yako, ukimaliza hapo tayari wanakuthibitisha (verified) na ndipo unaweza kuitumia akaunti yako.
I hope that helps.