Hello,
Salamu. kwa leo napenda kidogo kuzungumzia hili! Ni jinsi gani radio inaweza kukuingizia kipato zaidi katika radio yako. Kuna mambo machache ya kuzingatia kabla ya kuapply mbinu za kuingiza pesa.
1. Hakikisha radio yako inapunguza ama kumaliza kabisa porojo ili iweze kuaminika na watu wa rika mbalimbali. (Porojo ni pamoja na kuongea vitu visivyo na maana, kukosea kosea maneno, lugha ya mtaani, kuwa na matatizo ya kiufundi, kuwa na vipindi visivyokuwa na walengwa, kutokutumia script wakati wa vipindi, kukosa clock format ya radio na kutokuwa master log inayoeleweka)
2. Kuwa na watangazaji wenye general knowledge. Siyo anakuwa haelewi elewi tu, akiulizwa nini kinaendelea Libya anajibu nilishaacha kufuatilia. Wawe wabunifu wenye kujituma na kujisomea kila wakati vitabu mbalimbali. Uwezo wa kutumia computer utawasaidia sana.
3. Uwajue walengwa wa radio (Targeted audience) Ujue radio station goals&format.
4. Jaribu kubalance vipindi usiweke vya vijana tu, changanya mpaka vya watoto, viwepo vya kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kidini, nk.
5. Radio iwe na uwezo katika production ya vipindi, matangazo na mambo mengine zaidi.
Radio inashauriwa iwe na (PA) Public Audio system.
Kuna mengi ila hayo machache yanatosha kwa leo. Sasa baada kuwa na haya radio yako inaweza kukubalika na watu kuleta matangazo, vipindi, kudhamini na hata kusaidia kwa moyo wote.
IMPORTANT: Kuna vipindi vya radio au Tv makusudi kwa ajili ya commercial ambavyo vinadesigniwa kwa lengo la kuingiza income moja kwa moja! Saizi hivi ndio vinaingizia media mbalimbali kipato cha nguvu. Hapa unahitaji kuwa na producer mwenye ideas na ubunifu mkubwa!
Uliesoma ubarikiwe!
By
Radio Producer
radioproducer@rediff.com