Mkuu ww ni hatari kwa kujenga hoja aysee ila muelewe Mr Dua nae points zake zna mashiko mzee
Mimi sitaki kumuelewa Dua tu, nataka kuelewa ukweli.
Kuna vitu havipingiki.
Sehemu ya mapato ya kilimo kushuka, kwa mfano, ni bei katika soko la dunia. Tuna control ndogo sana katika bei. Nyerere alikuwa anaamka mapema sana anasikiliza BBC bei za mazao ya kilimo katika soko la dunia.
Kwa hivyo sitaki kutoa lawama zote za anguko hili kwa Magufuli.
Lakini pia, Magufuli ana sehemu kubwa ya lawama.
Kwa sababu, katika kitu kama korosho, zao ambalo ndilo la kwanza katika kutuingizia fedha za nje katika mazao ya kilimo, Tanzania ina some control kwenye price, kwa kuwa inaanza kuvuna korosho kabla ya dunia nzima.
Sasa sisi tumepata bahati hiyo, halafu badala ya serikali kushirikiana na wafanyabiashara kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na wafanyabiashara wanapata soko zuri nje, serikali ikaanzisha mzozo mpaka ile "window of opportunity" ikapita na dunia nzima ikaanza kuvuna korosho, kitu kilichofanya korosho zetu zisiwe na soko zuri tena.
Kwa kweli kuna kipindi bei ya korosho ilipanda sana, kwa kufuata kanuni za uchumi za "demand and supply". Soko lilikuwa halina supply, demand ikawa kubwa, bei ikapanda. Sisi tukawa tuna korosho, lakini hatuuzi kwa sababu ya mizozo ya kisiasa.
Huu ni mchezo wa kucheza na market price. Serikali inatakiwa kuwezesha wafanyabiasha kuuza korosho nje mara moja bei inapokuwa nzuri, bika kuchelewa. Inapochelewesha uuzaji wa kirosho kidogo tu, nchi nyingine zinaanza kuingiza korosho zao kwenye soko, na bei inashuka.
Huu ni mfano mmoja tu. Kuna mifano mingi kama hii ambayo ushauri wa wataalamu hauzingatiwi, serikali inajiingiza katika biashara, halafu baadaye tunakula hasara kubwa sana.
Kwa sababau mtu mmoja kutoka juu anaingilia mipango yote kama yeye ndiye anajua kila kitu.
Halafu watu tukisema maamuzi mabaya ya Magufuli, tunaambiwa kivivu tu kwamba tuna chuki binafsi na Magufuli.
Mimi Msukuma, baba yangu ana urafiki na Magufuli kipindi kirefu. Tangu kipindi cha Mkapa. Ilikuwa Baba yangu akii criticize serikali ya Mkapa kwa maamuzi yake mabaya, kwa maneno ambayo Magufuli alikuwa anataka kusema lakini anashindwa kusema, kwa kanuni za "collective responsibility", Magufuli anafurahia sana maneno ya Baba yangu. Inakuwa kama Baba yangu kasema maneno ambayo Magufuli alitaka kusema akashindwa/akaogopa. Baada ya mzee wangu kusema kesho yake ikawa Magufuli ndiye mtu wa kwanza kumpigia simu kumpongeza.
Sasa mtu kama huyo ambaye kwetu ni kama family friend nitamuwekeaje chuki binafsi?
Mimi naongelea principle tu. Its nothing personal.
Namalizia Kisukuma kwa msisitizo.
O Magufuli kokaya yise ale mnamhala wise gete gete.