How do you make your week end productive

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
587
1,000
Kwa wajasiriamali wengi huwa tunajikuta tunakuwa busy muda wote,hakuna cha week end wala week day ni mwendo wa kazi tu.

Ingawa ni jambo la kawaida ila sio jambo zuri. Mjasiriamali yeyote lazima ujiwekee muda wa kupumzika.

Sio lazima utumie ratiba kama ya watu wa kawaida yaani kupumzika WEEK END hapana, unaweza kuwa na ratiba yako ambayo umejiwekee na ukachagua angalau muda wa masaa 36 ambayo utatumia kurelax tu.

Kwa mjasiriamali kurelax kuna maana tofauti kabisa na watu wa kawaida.Kwa watu wa kawaida week end ndo siku wanayotumia kufanya usafi, kulewa, kutembelea ndugu na kujumuika.

Kwa mjasiriamali muda wa kufanya hayo unao wa kutosha kwa sababu muda wako wote uko mikononi mwako. Unao uwezo wa kutenga muda wa kufanya hayo yote wakati wowote kulingana na ratiba zako na majukumu yako ila kwa watu wa kawaida inabidi wafanye hivyo kwa sababu siku nyingine zote zimeshalipiwa na wengine.

Kama mjasiriamali, Week end yako au siku yako ya kupumzika unapswakupumzika kijasiriamali kwa kutumia muda wako wa mapumziko kuanya yafuatayo:
  1. Tafuta sehemu tulivo isiyo ghali,uwe na Kitabu cha kusoma,Diary na Glass ya juice au kama unatumia Kileo basi kileo chako Pendo
  2. Tumia muda wako kuitafakari wiki yako iliyopita kwa kina,ukiyaangalia maisha yako at 360 degrees,yaani personal and business life.
  3. Angalia mambo yote ambayo umeyafnya kwa wiki iwapo yamekamilika
  4. Tumia muda wako kuyatazama ambayo hayajakamilika na kwa nini
  5. Tumia muda huo kuweka mipango ya wiki inayokuja
  6. Tumia muda huo pia kutazama big picture ya maisha yako na changamoto unazokutana nazo
Kufanya hivyo kuna kusaidia kufanya akili yako iwe na nguvu na imaginations imara na pia inakuwezesha kuwa current katika maisha yako.

Mjasiriamali haitaji kutumia muda wake wa mapumziko bila kuwa productive,Ni lazima katika kupumzika pia tuwe productive.

Tujadili namna bora tunavyotumia muda wetu wa mapumziko kama wajasiriamali.

Karibuni
 
Top Bottom