Hongera kwa kutafuta njia mbadala vs. kuajiriwa. Sina utaalamu wa hiyo biashara lakini kwa ujumla ukitaka kujifunza jinsi ya kuiingia biashara ni vyema kuzungumza na walioko kwenye hiyo biashara tayari. Wengi ukiwaambia unataka kufanya wanachofanya wao watakupotezea... lakini ukijifanya unahitaji hiyo huduma, unaweza kuonyeshwa sample, ukapewa bei kutegemea na kadi ilivyotengenezwa, ukauliza turn around time ili kujua kama wanachapa wenyewe au wana-outsource. Ukizunguza sehemu 4-6 bila shaka utapata sehemu ambapo aliyeajiriwa hana uchoyo wa information akakupatia gharama za uendeshaji, wewe ukipiga hesabu utajua margins etc.
Ili kuanza kupata wateja, unaweza kumchangia rafiki/ndugu yako anayeoa/kuolewa karibuni kwa kumtengenezea kadi za harusi au send off. Ukiwa creative na kutengeneza kadi nzuri sana, si chema kitajiuza? Unaweza ukazitengeneza kwa gharama tu... yaani kama gharama ya kuchapisha ni TZSH 100,000 wewe unamchaji hiyo bila faida bora kutangaza biashara. Halafu unamuomba nyuma uweke jina na namba yako kwa herufi ndogo bora kama kuna mwenye shughuli karibuni akutafute.
Kila la heri, I hope wenye experience watakutwangia data zaidi.