Tajiri yenu
Member
- Dec 12, 2016
- 10
- 8
Nilichokisikia leo sijakiamini kabisa, kwanza napenda niwajulishe tu kwamba hii ni handle yangu nyingine kwa sababu handle yangu inajulikana na marafiki zangu wawili watatu hivyo kwa namna moja au nyingine ningemshushia heshima mzee wangu ambaye kwao wao wanamuona kama mtu safi kabisa.
Naomba nianzie mbali kidogo kwa kuelezea familia yetu japo ntafupisha, tumezaliwa wanne na mimi ndo wa mwisho, wenzangu wote washahitimu vyuo vikuu na wana kazi zao na wengine wanafamilia zao kabisa, mimi bado nipo mwaka wa 4 chuo ukiwa ndo wa mwisho kwangu hivyo bado sijaondoka nyumbani rasmi.
Nyumbani tumebaki watatu mimi, baba na housegirl, mama alishafariki muda kidogo, mimi binafsi sio mkaaji sana wa nyumbani mara nyingi huwa nipo nilipopanga karibu na chuo ninachosoma hivyo nyumbani narudi kipindi cha sikukuu au kwa special occasion.
Baba naye bado anamalizia malizia kazi zake kwani umri wa kustaafu unamuita akiwa anafanya kazi kwenye shirika moja la kiserikali na ana position kubwa tu, kwa vile mimi sio mkaaji sana home basi siku mojamoja huwa narudi kumsalimia mzee, kufupisha nasema tu sio mara moja au mara mbili nikirudi nakuta kuna wadada sometimes wamama wanalala pale na mzee siku tofauti tofauti, kama mnavyojua kwenye familia za kiafrica sina nguvu ya kuhoji chochote zaidi ya kuwasalimia tu na kukausha kwa vile najua mzee anajisahaulisha upweke alioachiwa na mama.
Kimbembe kimenikuta leo niliporudi home na kukutana na housegirl akiwa analia, sasa kwa vile yeye ni binadamu kama wengine nikambembeleza aniambie analia nini, asee alichoniambia kilinishtua sana, ni kwamba kwa takribani week kama 3 hizi amekuwa mtumwa wa kingono kwa mzee, kifupi ni kwamba mzee anapika na kupakua hapa, akanililia sana kwamba nisiondoke kwa vile siku hio amechoka na mzee ashamtumia meseji anakuja kuendelea na kazi baadae, ile meseji niliisoma na niliishiwa nguvu kwa kweli nisijue nini cha kufanya.
Nisiwachoshe, hayo yote yamejiri leo na mpaka dakika hii bado nipo home nashindwa kuelewa nifanyeje, niwaambie mabro zangu au nifanyaje japo kwa asilimia 90% ninavojijua hili nitakufa nalo moyoni, this is too embarrassing kwa kweli na nisingependa mzee awe na hiyo image japo kumueleza ni mbinde.