Mimi wangu aliwahi kupata mimba, sikumrudisha kwao maana alikuwa anaendelea na majukumu yake vizuri huku akiwa mjamzito. Nilipanga kumrudisha miezi kama mi3 baada ya kujifungua maana niliuelewa ugumu wa maisha wa vijijini. Alijifungua, nikamuhudumia wakati nimeleta dada mwingine.
Baada ya wiki 2 tu, akaanza kupiga kazi kama kawaida, smtms kumzidi asiye na mtoto. Nikaamua kumuacha aendelee na kazi sikuona usumbufu mkubwa sana kwa yule mtoto wake. Baada ya miaka kama miwili hivi mtoto alichukuliwa na kaka yake. Ila yeye bado nipo naye. Trust me, kitendo cha kumuhudumia, hajawahi hata kuwaza kuondoka kwangu. shida ya maHG nazisikia kwa mashosti wangu, kwa muda mrefu sizijui.
watu wengi sana walinishauri nimuondoe, lkn nilikataa kutokana na jinsi alivyo mchapa kazi. kwani pamoja na mimba yake, kuwa na mtt, kila kitu kilikuwa kinaenda sawa nyumbani kwangu. Pia nilimuonea huruma kurudi kijijini. wale walionishauri nimuondoe, sasa wananionea donge wanasema nina bahati sana ya kupata msichana aliyedumu zaidi ya miaka mitano nyumbani kwangu. wameshasahau walivyokuwa wananishauri nimfukuze. Jamaa mwenyewe aliyempa mimba ni playboy tu wa mtaani kazi yake kuchukua maHG wa watu.
usiache watu wakuamulie maamuzi ya home kwako, kama unaona ana-worth kuendelea kukaa naye, usimuondoe