Mkuu hapa ndo tunakosea wengi wetu. Usimwangalie House Girl kama gatekeeper tu- kula na kulala. Hebu mtizame kama raia yeyote anayetafuta maisha achomoke. Jiulize wewe ofisini ungekuwa unalipwa mshahara mdogo (kisa unapewa lunch mfano) ingekuwaje? Would you feel valued?
My point is: Wafanyakazi wa ndani (na wengineo) lazima tujitahidi kuwalipa ujira unaoendana na hali halisi ya maisha na kadri ya uwezo wetu (by the way ajiri house helper if you can afford her/him). Kwa kufanya hivo watakuwa motivated na wataiona faida ya kazi-na hiyo kada itaheshimika. Kuhusu kulala you can as well make arrangement akajitegemea.
Ni kwa mawazo kama haya, mpaka leo migogoro ya house girls na waajiri haiishi na visa vingine vya kusikitisha. Kwa sababu kwa nia njema kabisa huwezi ukamlipa mtu 40k ukategemea kwamba atakuwa productive au athamini kazi.
Hivi kweli unaweza ukampa mtu 40K na bado ukategemea aangalie mtoto wako with full attention and dedication?
Mkuu kunradhi sina maana mbaya na tangazo lako lakini kama vijana wa leo, nasisitiza lets be different from wazee wetu. Tujue kabisa kazi ni uhai. Hata huyo house girl na yeye ana ndoto kama wewe na mimi. One day anatamani aishi kwake. awe na maisha yake independent. 40k haiwezi mfikisha huko.
NB: Mimi nilipata House helper (mshahara kima cha serikali-but all costs on me), na nilimwambia nitamwendeleza kimasomo (nimlipie karo wakati anaishi kwangu na naendelea kumlipa mshahara-kama hela ya kujikimu). Alikaa kwangu almost three years. she was part of my family. Lakini bahati mbaya mji ukamchanganya akaanza ukorofi-shule akakataa kutafuta. Alinivuruga sana. Lakini you cant believe me, I gave her second chance. Nikamwambia tafuta course yoyote nitakulipia lakini hutakaa kwangu. Sasa yuko shule namlipia karo na matumizi nampa. Ni sadaka nilitoa lakini najua utafika mda ataangalia nyuma ataona kwamba I did something for her. Hata mimi I made lots of mistakes in life and some people gave me second chance.
The point is watumishi wa ndani tuwathamini kwa kulipa vizuri. wengi ukorofi wao unasababishwa na sisi wenyewe kuwadharau yet they do so much for our families.
Masanja